Polisi kuanza kuwashughulikia wanaoharibu miundombinu ya Reli

Polisi kuanza kuwashughulikia wanaoharibu miundombinu ya Reli

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiowahaminifu kwa kuhujumu miundombinu ya reli jambo ambalo linaiingizia serikali hasara kubwa kutokana na uwekezaji unaofanywa.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika wilaya ya Kipolisi ya Mlandizi mkoani Pwani ambapo amesema vitendo hivyo vya kutaka kuhujumu miundombinu ya reli vimeanza kuchukuliwa hatua kali huku akimuagiza Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Boaz kufanya operesheni ya kukamata wahalifu hao pamoja na msako kwa wanaojihusisha na biashara ya vyuma chakavu.

naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini Masanja Kadogosa amesema kuwa wao kama shirika wataendelea kushirikiana na vyombo vya dola pamoja na kuimarisha mifumo ya usalama ili kuhakikisha miundombinu ya reli ahiwezi kuhujimiwa.
 
Wanachoweza ni Kuwazuia na kupambana na CHADEMA.

BANGI GONGO NA Dhami zimejaa mjini na vijijini HAWAZIONI.

rubish
 
Hiyo Reli ipo nchini zaidi ya miaka 100 na hujuma kubwa mpaka dola wanagutika hatujawahi sikia lakini inakuwaje intelgensia ya Polisi haikuweza kutambua wananchi Awamu ya Tano wataanza kuhujumu reli? Intelgensia ya Polisi imesifiwa sana kwa kutoa taarifa za vyama vya Upinzani kwa wakati wanapotaka kufanya maandamano yanayoadhiria uvunjivu wa amani na Polisi kuchukua hatua kabla ya amani kuvunjika, ilikuwaje uhali huu haukujulikana wa mapema? Labda swali la kujiuliza ni: kwa nini sasa IGP Sirro akiwepo?
 
Hawa wahujumu ni wapenzi na wafadhili wa "Saccos"
 
Back
Top Bottom