Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiowahaminifu kwa kuhujumu miundombinu ya reli jambo ambalo linaiingizia serikali hasara kubwa kutokana na uwekezaji unaofanywa.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika wilaya ya Kipolisi ya Mlandizi mkoani Pwani ambapo amesema vitendo hivyo vya kutaka kuhujumu miundombinu ya reli vimeanza kuchukuliwa hatua kali huku akimuagiza Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Boaz kufanya operesheni ya kukamata wahalifu hao pamoja na msako kwa wanaojihusisha na biashara ya vyuma chakavu.
naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini Masanja Kadogosa amesema kuwa wao kama shirika wataendelea kushirikiana na vyombo vya dola pamoja na kuimarisha mifumo ya usalama ili kuhakikisha miundombinu ya reli ahiwezi kuhujimiwa.