Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Malalamiko ya baadhi ya wananchi na taasisi kuhusu mali zao kuchukuliwa na Jeshi la Polisi wakati wa kukamatwa yameibua mjadala kuhusu mipaka ya mamlaka ya polisi katika kushikilia mali zinazodaiwa kuwa sehemu ya ushahidi wa uchunguzi wa makosa ya jinai.
Malalamiko ya hivi karibuni yametolewa na mwanamke anayejitambulisha kwa jina la Pipytida kwenye mitandao ya kijamii, anayesema simu yake yenye thamani ya Sh3.5 milioni ilichukuliwa baada ya kufika Kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa maelezo yake, alifika kituoni baada ya kuhojiwa kuhusu maudhui anayoweka kwenye mitandao ya kijamii. Anadai polisi walimweleza kuhusu aina ya mavazi aliyokuwa akitumia katika picha na video zake, lakini baadaye simu yake ikachukuliwa.
Tukio hilo limeibua swali: Je, polisi wanaweza kushikilia simu au mali nyingine ya mtu kwa muda gani kwa madai kwamba inahitajika katika upelelezi?
Malalamiko ya aina hiyo yamewahi kutolewa pia na watu wengine waliokamatwa na polisi.
Miongoni mwao ni aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Joseph Mwasote, ambaye alikamatwa Tunduma, Mkoa wa Songwe, Novemba 25, 2025, na baadaye kushikiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Mwasote, ambaye sasa anaishi mafichoni, amedai kuwa wakati wa kukamatwa kwake alinyang'anywa simu zake pamoja na fedha zaidi ya Sh500,000.
Aidha, mwanasheria maarufu mkoani Iringa, ambaye jina lake limehifadhiwa, anadai kuwa alipokamatwa na polisi Novemba 2025, walichukua simu zake zaidi ya mbili na laptop moja kwa madai ya kuzifanyia uchunguzi.
Mwanasheria huyo alidai kuwa hatua hiyo ilihusishwa na madai ya ushiriki wake katika makundi ya kisiasa na utetezi wa watu waliokuwa wakikabili mashtaka ya uhaini yaliyohusishwa na matukio ya Oktoba 29, 2025.
Anasema hadi sasa hajarejeshewa simu na laptop hizo, licha ya shauri lake kufutwa.
Sheria inasemaje?
Sheria Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), Sura ya 20, kifungu cha 41 kinatoa mazingira ambayo polisi wanaweza kumpekua mtu na kukamata kitu kinachohusiana na kosa.
Miongoni mwa mazingira hayo ni pale upekuzi unapofanyika kwa mujibu wa waranti, wakati mtu anachukuliwa katika ulinzi kwa mujibu wa sheria, au kwa mujibu wa amri ya mahakama.
Sheria pia inatambua mazingira ya dharura. Kifungu cha 42 kinaruhusu polisi kufanya upekuzi na kukamata kitu kinachohusiana na kosa bila warrant pale wanapokuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hatua hiyo ni muhimu kuzuia kitu hicho kupotea au kuharibiwa, na mazingira yana uzito na uharaka unaohalalisha hatua hiyo.
Hivyo, ukweli kwamba mtu amekamatwa hauleti moja kwa moja mamlaka ya polisi kuchukua kila mali yake.
Mali inaweza kushikiliwa hadi lini?
Kifungu cha 45(1) cha Criminal Procedure Act R.E. 2023 kinasema kuwa kitu kilichokamatwa na kuletwa mahakamani kinaweza kushikiliwa hadi mwisho wa kesi au uchunguzi, huku kikitunzwa kwa uangalifu unaostahili.
Endapo kuna rufaa au mtu amepelekwa kwenye trial, mahakama inaweza kuagiza kitu hicho kiendelee kushikiliwa kwa ajili ya rufaa au kesi hiyo.
Kifungu cha 45(3) kinasema kwamba pale ambapo hakuna rufaa au hakuna mtu aliyepelekwa kwenye trial, mahakama itaelekeza kitu hicho kirejeshwe kwa mtu ambaye kilichukuliwa kwake, isipokuwa kama mahakama inaona kuna sababu nyingine au sheria inaelekeza kitu hicho kishughulikiwe kwa namna tofauti.
Hii ina maana kuwa dhana ya “ni kizibiti (exhibit)” haipaswi kuwa sababu ya mali ya mtu kubaki mikononi mwa mamlaka bila kikomo.
Simu si lazima iwe ushahidi kwa sababu tu inatumika kuingia mtandaoni
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa, anasema changamoto ya kushikiliwa kwa mali za watu waliokamatwa imekuwepo kwa muda.
Anasema wakati mwingine polisi huchukua vifaa vya kielektroniki, magari na mali nyingine kwa madai kwamba vinahusiana na upelelezi.
“Vifaa wanavyopaswa kukaa navyo polisi ni vile ambavyo vitatumika kwenye kesi mahakamani,” anasema.
Olengurumwa anatoa mfano wa simu, akisema iwapo mtu anatuhumiwa kwa kufanya jambo fulani kwenye mitandao ya kijamii, inapaswa kujiulizwa kama simu yenyewe ndiyo iliyotumika kutenda kosa na kama ina umuhimu wa moja kwa moja kama ushahidi.
Kwa mtazamo wake, kuna haja ya kuwa na utaratibu unaotofautisha vifaa vinavyohitajika kama ushahidi wa kesi na mali nyingine ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na kosa linalochunguzwa.
Kunyakua mali na kuifuta kabisa umiliki si kitu kimoja
Sheria pia inatofautisha kati ya kushikilia mali kama sehemu ya mchakato wa jinai na kutaifisha (forfeiture au confiscation), yaani mali kunyang'anywa kwa amri ya mahakama.
Chini ya kifungu cha 351 cha Criminal Procedure Act, mahakama inaweza kuamuru mali ifanyiwe forfeiture au confiscation pale mtu amepatikana na hatia na mahakama imeridhika kuwa mali hiyo ilitumika au ilikusudiwa kutumika katika kutenda au kuwezesha kutenda kosa.
Kwa hiyo, kuchukua simu, laptop, gari au mali nyingine kwa ajili ya uchunguzi si sawa na kuinyang'anya kabisa mali hiyo.
Swali linalobaki
Malalamiko haya yanaibua swali pana zaidi kuhusu uwiano kati ya mamlaka ya polisi kufanya uchunguzi na haki ya mtu kulindwa dhidi ya kunyimwa mali yake bila sababu ya kisheria.
Katika kesi ambayo simu, laptop au mali nyingine inahitajika kweli kama ushahidi, sheria inaruhusu utaratibu wa kuendelea kuishikilia kwa mujibu wa masharti yake.
Lakini pale ambapo uchunguzi umekamilika, shauri limefutwa au limekwisha na hakuna amri nyingine ya mahakama au sheria inayoruhusu mali hiyo kuendelea kushikiliwa, suala la kuendelea kuimiliki linahitaji maelezo ya kisheria.