Polisi kuendelea na ukamataji usiozingatia taratibu: Hawajasikia maagizo ya Simbachawene? Wanafuata maagizo ya nani?

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Majuzi Waziri Simbachawene alitoa maagizo akiwataka Jeshi la Polisi kukamata raia kwa kufuata taratibu na sheria, kwa kutokamata raia kihuni. Wawe wanavaa sare, na waache kuvaa kininja.

Itakuwa Simbachawene si lolote si chochote, maana toka atoe maagizo hayo bado watu wanakamatwa kihuni, mara tusikie wamevamiwa usiku, mara wavamie sehemu za kazi huku wakiwa hawana sare rasmi, mara waende kumkamata mtu wakiwa na magari ambayo hayana plate number, yaani tafrani!

Kama hawasikilizi maagizo ya waziri, wanasikiliza ya nani? Kuna nani mwingine anayetoa maagizo kwa Jeshi la polisi kuendelea kufanya kazi kihuni kama watekaji na majambazi?

Halafu tukisema nyie ndio 'Watu Wasiojulikana' mnakataa vipi sasa? Wakati kila siku mnatuthibitishia kutokana na uhuni wenu?🤔
 
KUELEKEA X MASS HAKIKISHA UNAJIEPUSHA NA MAKUNDI YANAYOCHOCHEA VURUGU , LINDA AMANI YA NCHI NA LINDA UHAI WAKO
 
Hili laonesha kuna.systemic failure kama waziri anaongea script ingine na wao.wanaendelea kuteka watu. Kukamata watu saa nane za usiku. Kukamata viongozi wa chadema..

Hii mifumo inajengeka taratibu lakini inaweza ikawasumbua hata wanaoijenga. Investor gani atakuja kuwekeza sehemu kuna utekaji.
 
Usiyaamini sana maagizo ya hawa mazafakas. In public wanaagiza one thing na in private wanaagiza another thing!
 
Kwani Simbachawene na Samia nani mkubwa? Kikosi kazi kinachoteka na kuua watu kinapokea maagizo toka kwa Samia kupitia mwanawe Abduli
 
Sema Kutekana tekana ni habari za kishamba sana.

Ni vile tu mjinga kapewa cheo na kaamua kutumia nguvu kama njia ya kutatua changamoto.

Mtu hana hata bunduki, silaha kubwa aliyokua nayo ndani labda kisu na umma, unaenda na difenda halina hata namba.

Watu wanaingia kininja hata uniform hawana yaani kama sinema vile. Yote ya nini haya jamani??? Sisi sote ni ndugu. Jamani
 
Back
Top Bottom