Polisi kufunguka leo kuhusu kilichomkuta Dk Ulimboka

Wadau
Naomba yule mwenye taarifa kuhusu kilichojiri kwenye hii Press Conference ya Kova kuhusu maswala ya Dr Ulimboka leo atuhabarishe ili tujue nini kimezungumzwa. Nimejaribu kutafuta humu jamvini nimekosa
 
Tumsubiri Pasco
Atakuwa amehuhuria,
 
Mi ndio kwanza nasikia kuwa kuna conference!
Police wanaitisha conf. ya nn? Sisi tunataka tusikie watuhumiwa wote wako ndani kama si mahakamani!
Hii ndio shida ya siasa kuingizwa kwenye majeshi.
 
Mi ndio kwanza nasikia kuwa kuna conference!
Police wanaitisha conf. ya nn? Sisi tunataka tusikie watuhumiwa wote wako ndani kama si mahakamani!
Hii ndio shida ya siasa kuingizwa kwenye majeshi.

Mkuu Mwananchi la leo limeandika ukurasa wa mbele kabisa kuhusu hii Press conference ya Kova
 
ishafanyika?

Kova ana tabia ya kufanya mikutano yake na wanahabari saa saba kamili mchana na sasa ni saa kumi kasoro, lazima itakuwa imekwisha KAMA TU KOVA HAKUPATA MSHAURI MZURI NA KUMWAMBIA AACHANE NA HIYO CONFERENCE ALIYOITANGAZA TANGU JANA
 
kova huyu huyu ninae mjua mimi ama mwingine? hakuna litakalo zungumziwa hapo ni uzushi na porojo tu
 
Watu wengine bana, wewe mbona hivo lakini??

Wenzio bado wako studio na wewe kazi ni kutaka tu kuwaharibia stimu ya jinsi gani watoke vipi vile huku Dr Ulimbomboka 'AKIPATA KUZALIWA UPYA KWA MTINDO UTAKAOWACHUKIZA SANA WENGI' sawa na Nikodemo wa kwenye Biblia alivyopata kuzaliwa upya nje kabisa ya mipaka y ufahamu wake jinsi gani mtu mzima kaka yeye angeweza kuingia tumboni kwa maama yake kuzaliwa upya tena.

Hakika haya yote, kwa mujibu wa nyepesinyepesi tulizo nazo hadi hivi sasa, ni katika kutafuta kuliokolea sura jeshi lililonusurika kumtoa roho; wewe vipi mkuu!!!!!!!!!!!! Bahati mbaya tu ni kwamba Umma wa Tanzania siku hizi HATUDANGANYIKI kitu hapa!!!

Na picha bado itaendelea;
kumbuka siku zote STERINGI kwenye filamu huwa hafi isipokua anaweza tu kubadilishiwa majukumu tu kulingana na hali halisi iliopo na jinsi gani MSIMAMIZI WA KI-CHINA anavyotamani picha hii ya KI-HINDI ionekane kwa HADHIRA MBUMBUMBU anayoifahamu vema miaka yote.
 

Wewe kutaja jina lako halisi tu unaogopa halafu unamsakizia mwenzako aingie kwenye vita na dola!!! Nyinyi watu mko very ridiculous...
 
Bado tu hiyo press conference?Nina uhakika kutakuwa na comments nyingi sana mara baada ya hiyo conference.

Nasubiri tu kusoma btn lines nipate context kabla sijatupa madongo.
 
PRESS CONFERENCE YA LEO NI FURSA YA TAIFA KUFAHAMU MBIVU NA MBICHI ZA DR ULIMBOKA NA MASHAIBU YA 'LANGO LA KUZIMU MABWEPANDE'

Sote tuko gado hapa tunasubiri tulitazama hili ONYESHO LA NNE na jinsi gani Jeshi la Polisi litakavyoliunda ki-ufundi zaidi na Dr Ulimboka mwenyewe akishiriki kwa mara ya kwanza tangu aliporejea nchini akitokea matibabuni Afrika ya Kusini.

Nasema tuko hapa leo hii kutaka kujua MBIVU na MBICHI juu ya Dr Ulimboka tuliomuombea sana dua njema ya kumtaka Mwenyezi Mungu akamnusuru uhai wake ili aje APATE FURSA YA KUMUMBUA SHETANI wa kule MabwePande bila huruma.

Wakuu tuendelee tu kuandika nne hapa au Afande Mhina keshasema chochote kutoka kwa Mzee Kova??
 
hivi Kova alikuwa wapi?nilidhani unaumwa au umepewa kazi maalumu? haya ngoja tuone mwendelezo utakuwaje, kama umetengeneza sinema na Ulimboka, uwe mwangalifu zaidi, maana yanaweza kuwa kama ya mkenya na mchungaji..ngoja tusubiri,hivi KOVA bado hajazungumza tu?
 
haya ni majibu ya tume iliyoundwa au ni issue tofauti kabisa? Movie ikigoma Tunaweza ambiwa mambo ya sensa...
 
Nimekumbuka maneno ya mjomba tunasoma tupate kazi ili tupate pesa,sasa kama unacheza picha kama hili unapigwa unavuliwa mpaka nguo za ndani ukilipwa vizuri unakaa kimya
Naamini wapo wenye kujua kama nae alilazimishwa au nae alipelekwa msitu wa pande. Wajitokeze bac watujuze.
 
Pesa ni lazima watajaribu kumpa,hilo halina ubishi kama unaielewa bongo vyema.Na kama amefanya hivyo,yani kuzipokea,tutajuwa tu.Tusi rush kwenye conclusion.

Kama anapita hapa,comments zetu zinatakiwa zimu encourage ili tusije kuendelea kupeana lawama za unafiki.He doesn't have to feel like he's alone,kwahiyo tusifanye kosa la kumu alienate.Ni mtu amabaye pande zote zinamuhitaji kwenye mustakabali wa Taifa.Mafisadi wanamtaka and so as wanaharakati na wazalendo,kila mmoja kwa nia yake.Ni juu yake kuchagua upande sahihi wa historia ili isije muhukumu tofauti.Akumbuke hilo tu.
 
zomba pamoja na ugamba wake aliwahi kuhoji hapa, swali nililojiuliza alfajiri ambayo Uli aliokotwa Mabwepande. Ilikuwaje akaenda kuonana na mtu wa state house peke yake tena usiku, kuongelea mgomo wa madaktari?

Ajieleze ili nae ajibu maswali ya watu. Still hai_justfy kuteswa na dola, lakini hii inaweza kuwa muendelezo wa mambo mengine tusiyoyajua wala kutaka kuyahoji!
 
Last edited by a moderator:
Kaka-shemeji, ni kweli he doesn't have to feel he is alone. Lakini ameanza kutu-isolate. Haeleweki eleweki hivi! Na hajui tukimaliza kutumia akili zetu kumtafakuri tutaanza kutumia sub-concious minds.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…