Hakuna maskini anaeingia kwenye siasa ili awatetee wanyonge kabla ya kutetea maslahi (tumbo) lake kwanza. Khulka ya Watanzania hata anapokwenda kusomea somo fulani, kwa jinsi bado tulivyo nyuma ki maisha, huwa kwanza unafikiria usomeee nini kinacholipa zaidi. Hatujafikia stage ya kusema nasomea "udaktari" ili nibadilishe maisha ya watu kwa taaluma yangu. Simply kwa sababu ni masikini tuliofunguliwa minyororo na kuonjeshwa raha za kuwa nacho.
Vizazi vitano baadae, tutapokuwa na warithi wa mali wasizozijuwa chanzo chake tutaanza kuwa na wimbi la vijana wataojituma kwa faida ya wengi kwa kuwa tu, wanazo, hawana jipya katika anasa linalowastuwa au wanalolitamani amabalo hawajalikuta ayari, hapo ndipo tutapata vijana wanaoinhia kwenye fani yoyote waipendayo kwa kuweka "impact" na "legacy" zao kwa kutenda mema mengi kwa ajili ya wengi.
Mifano hai, ni waliozaliwa na kuuukuta utajiri wa vizazi japo viwili au vitatu nyuma, ni tofauti na wale wanaozaliwa na kuukuta utajiri unaotengenezwa na wazazi wao na huku wanaujuwa vyanzo vyake.
Si Ulimboka, si vitajiri uchwara vingine vyovyote vyenye kisomo kilichotokana kwenye umaskini wawe na muono wa kutumikia wengi kabla hawajafikiria kutumikia matumbo yao kwanza na kuonesha wanawazunguka kuwa wao wamefanikiwa.
Tofauti na mtu kama Sabodo, aliyezaliwa na kukuta tayari mali kede kede kwao na yeye hakuwa na shida lakini kila alilolifanya kama yeye nalo likawa linamzalishia mali kwa wingi zaidi na anaendelea kuzalisha akiba alizozirithi za vizazi vitatu au vinne nyuma, mtu kama huyu huwa anataka kuweka legacy kwa kunifaisha wengi kwa mali zake na si kunufaisha tumbo lake.
Ulimboka bado ni kichumia tumbo tu na Watanzania wengi bado tunamuona bora na alieweza maisha yule mwenye nacho.