Polisi kuwapiga raia huu ujeuri wanautoa wapi? Naomba mwenye ushahidi wowote wa raia wa Tanzania kupambana na Polisi auweke hapa

Kwa jinsi anavyohangaika asipokuwa makini yatamshinda.
Yatamshinda kwa sababu amekataa kupelekeshwa na tantalila za Chadema?

Polisi wamekuwa hivyo miaka mingi toka enzi za Mkapa, Kikwete na Magufuli.

Na si Tanzania peke yake. Kwani kilio cha "defund the police" huko Marekani unafikiri ni kwa sababu gani?

Au kule Nigeria na "end SARS"?

Kama ni kudeal na police incompetence na police brutality msitake kuchanganya na mambo yenu ya siasa.

Police ni taaluma na ishughulikieni kitaaluma. Basi.
 
Tatizo wanachapwa ni wale wanakulitafuta.

Ndio maana hampati sapoti kutoka kwa wananchi wote.
 
Tatizo wanachapwa ni wale wanakulitafuta.

Ndio maana hampati sapoti kutoka kwa wananchi wote.
Mawazo ya kipumbavu kama haya yanasababishwa na ujinga ambao ni mtaji mkubwa wa CCM. Polisi kufanya mazoezi mtaani ni ulimbukeni na ukimtazama huyo afande anayetishia kuwapa raia kipigo cha mbwa koko, unaona moja kwa moja kwamba hana tofauti na kibaka wa mtaani ni vile tu kavaa magwanda.

Upuuzi kama huu huwezi kuuona popote pale isipokuwa hapa Bongo. Bahati yao ni kwamba Watanzania wana uvumilivu usio na mfano. Polisi aliyeiva kimafunzo hawezi kufanya ujinga huo, ni vile tu wengi wamefika walipo kupitia UVCCM. Kama alivyowahi kuonya Baba wa taifa, aliyeonja nyama ya mtu haachi.

Polisi wa namna hiyo ni sadists, wengi wao ni wagonjwa kiakili...bila kumwaga damu hawapati usingizi na hata sura zao zinaonesha walivyo na hamu ya kuumiza. Ukatili na kuumiza raia kunawapa raha!
 
Una mizigo mingi kichwani ipunguze,upumue kidogo.

Adui wa chadema sio polisi,sio ccm,sio rais,wala si katiba.ni mtazamo wao.
Kudhani tu polisi ni watii kwa ccm sababu hawana akili ni sehemu tu ya ugonjwa mkubwa mlio nao.
Polisi hawakatazwi popote kukimbia mtaani,maana hata ofisi zao ziko mtaani pia.
Swala la umasikini wao bado ni mtambuka,maana kuna polisi bado wanakuzidi kipato pamoja na kuitumikia kwao ccm.

Mtambueni kwanza adui yenu kiundani,mtapata kuungwa mkono mpaka na mawe.
 
We don't fight with "Trained Fools" yaani ni mwendo tu wa kuwasaidia "majukumu" ya nyumba zao! Ukifika unapikiwa, unakula ukimaliza unakula na mpishi! Wakati huo yeye kaenda Lindo Bank ya NMB au CRDB huko anapigwa baridi
 
Una hakika mimi sielewi? Jaribu tena kusoma OP na conclusion aliyofikia utajua maana ya nilichoandika. Video niliyoweka ni mwananchi naye aliyechoka uonevu wa polisi akaamua potelea mbali. Liwalo na liwe. Yalimtokea umeyaona.
Kama unaelewa maana ya hilo neno, basi unayoandika hapa unajichanganya mwenyewe, sijui kwa manufaa gani.
 
Jeuri wanaipata kutokana na nafasi zao walizo nazo ,na hii inachagizwa na katiba mbovu iliyopo!

Kwaharaka kabisa hatusahau kwamba wanateswa na kiburi Cha uzima!
 
Watanzania majoka ya kibisa kabisa. Sasa tunangoja nini? Polisi wanajivunia umoja na silaha zetu. Si Wana ndugu na watoto hawa? Tit for tat
 
Taaluma ya kuonea badala ya ulinzi WA mali na raia? Ngojea kidogo weka haya akiba polisi watapigwa na raia waliochoka
 
Mkuu shukrani mingi sana
 
Ngoja waendelee kutujaza sumu raia, siku tutalipuka zaidi ya Tsar Bomba.. na hawata amini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…