DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Mkama, amewataka wananchi kupuuza wito wa maandamano unaosambazwa mitandaoni kwa kueleza kuwa ni kinyume cha sheria na unaweza kuvuruga amani ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa Oktoba 24, 2025 wakati wa hitimisho la mazoezi ya pamoja ya majeshi yote ya ulinzi na usalama yaliyofanyika Manispaa ya Morogoro, ikiwa ni maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Aidha, Kamanda Mkama amewahimiza Maofisa na Askari wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama kutekeleza majukumu yao kwa weledi, kwa kuzingatia sheria na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.