Polisi: Madereva wa Serikali wana kiburi sababu ya Namba za Magari yao

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kamanda Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema baadhi ya madereva wanavunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za Serikali kama STK, STL, SM, PT na kulindwa na viongozi wanaowaendesha.

Amesema baadhi ya madereva hawafuati taaluma zao na wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema " Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwani dereva akiwa wa hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,”.

=======================

Kamanda Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi amesema wapo baadhi ya madereva wa Serikali ambao wanaendesha kwa kiburi magari yao huku wakivunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za STL, SM, PT na viongozi wanaowaendesha na sio taaluma.

Amesema baadhi ya madereva hao wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya madereva wa Serikali ili kuwakumbusha utii wa sheria za usalama barabarani na udereva wa kujihami utakaosaidia kupuza ajali.

“Sisi madereva wa Serikali ndio wenye matatizo, baadhi yao wengi wanafanya vizuri. Yaani wao kinachowafanya waendeshe magari na kile kiburi cha kuvunja sheria ni kwasababu wanamuendesha kiongozi fulani au ofisa fulani,” amesema.

Kamanda Bukumbi amesema jeshi hilo litaendelea kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria za usalama barabarani bila kujali anamuendesha nani.

“Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa kwanza unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwa sababu dereva anafanya hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,” amesema Bukumbi.

Amesema kama dereva anavunja sheria na kiongozi wake anamuona lakini hachukui hatua maana yake anaidhalilisha nafasi yake, taasisi na idara anayofanyia kazi.

Awali, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoani Iringa, Mosi Ndozelo amesema hakuna dereva aliye juu sheria.

Amesema madereva wa Serikali wanapaswa kutii sheria zilizopo na kwamba wanaamini mafunzo hayo yatawabadilisha mtazamo.

“Wanaojiona wapo juu ya sheria kupitia mafunzo haya wataweza kubadilika, tunataka kuwabadilisha wenye mawazo mgando kwamba wakiendesha viongozi au magari ya Serikali basi wapo juu ya Sheria,” amesema.

Kwa upande wao baadhi ya madereva walisema sio wote wanaovunja sheria za usalama barabarani japo baadhi yao wamekuwa wakifanya hivyo kwa kivuli cha viongozi au namba za magari wayayotumia.

“Binafsi najua natakiwa kuwa kioo na kwa kweli huwa sipendi kuvunja sheria, natumia udereva wa kujihami ambao naweza kuepusha ajali kwangu na wanaonizunguka,” amesema Mohamed Maghembe, derva wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini.

MWANANCHI
 
Asisahau na magari yenye namba za PT.
Polisi, jeshi na viongozi wengi na hata magari ya Mahakama na Majaji, wote wanaongoza kutoheshimu sheria za barabarani.
Sasa kuna hata magari ya viongozi wa Uhamiaji UT,Zimamoto ZM, UWT na mengine mengi, wote sawasawa na bodaboda na Bajaji.
Hawaheshimu sheria za barabarani.
 
Suluhisho ni simple. Watuambie tuwe tuna submit video za fujo wanazofanya huko mabarabarani. Tutafunga Dashboard camera kwaajiri ya hawa mabwege. Ili zirekodi na kuwe na ushahidi ambao hawawezi kukataa hata wakipelekwa kwenye vyombo vya sheria.

Kinachotokea hapa tz ni kuleana na wala si swala kwamba taarifa hazipo au pengine labda kuna ugumu kudeal nao.
 
Comment yangu Bora ni hii....
 
Huyo polisi akae kimya tu, wao ndio huwa wanaagizwa kusimamia wizi wa kura. Kama wanashiriki kuwaingiza hao viongozi madarakani kinyume na sheria, wanategemea wakishaingia madarakani watatii hizo sheria?
 
Amesema baadhi ya madereva hawafuati taaluma zao na wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.
Acha hao madereva wawndelee na kiburi ili hawa walaji wa tozo wateketee kwa ajali.
 
Kamanda Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema baadhi ya madereva wanavunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za Serikali kama STK, STL, SM, PT na kulindwa na viongozi wanaowaendesha.

Amesema baadhi ya madereva hawafuati taaluma zao na wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema " Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwani dereva akiwa wa hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,”.

=======================

Kamanda Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi amesema wapo baadhi ya madereva wa Serikali ambao wanaendesha kwa kiburi magari yao huku wakivunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za STL, SM, PT na viongozi wanaowaendesha na sio taaluma.

Amesema baadhi ya madereva hao wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya madereva wa Serikali ili kuwakumbusha utii wa sheria za usalama barabarani na udereva wa kujihami utakaosaidia kupuza ajali.

“Sisi madereva wa Serikali ndio wenye matatizo, baadhi yao wengi wanafanya vizuri. Yaani wao kinachowafanya waendeshe magari na kile kiburi cha kuvunja sheria ni kwasababu wanamuendesha kiongozi fulani au ofisa fulani,” amesema.

Kamanda Bukumbi amesema jeshi hilo litaendelea kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria za usalama barabarani bila kujali anamuendesha nani.

“Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa kwanza unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwa sababu dereva anafanya hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,” amesema Bukumbi.

Amesema kama dereva anavunja sheria na kiongozi wake anamuona lakini hachukui hatua maana yake anaidhalilisha nafasi yake, taasisi na idara anayofanyia kazi.

Awali, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoani Iringa, Mosi Ndozelo amesema hakuna dereva aliye juu sheria.

Amesema madereva wa Serikali wanapaswa kutii sheria zilizopo na kwamba wanaamini mafunzo hayo yatawabadilisha mtazamo.

“Wanaojiona wapo juu ya sheria kupitia mafunzo haya wataweza kubadilika, tunataka kuwabadilisha wenye mawazo mgando kwamba wakiendesha viongozi au magari ya Serikali basi wapo juu ya Sheria,” amesema.

Kwa upande wao baadhi ya madereva walisema sio wote wanaovunja sheria za usalama barabarani japo baadhi yao wamekuwa wakifanya hivyo kwa kivuli cha viongozi au namba za magari wayayotumia.

“Binafsi najua natakiwa kuwa kioo na kwa kweli huwa sipendi kuvunja sheria, natumia udereva wa kujihami ambao naweza kuepusha ajali kwangu na wanaonizunguka,” amesema Mohamed Maghembe, derva wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini.

MWANANCHI
Dawa ni moja tu serikali itoe tamko kwamba gari ya kiongozi yeyote itakayovunja sheria za usalama barabarani pamoja na kiburi cha madereva hiyo gari ikamatwe tu ikae kituoni alafu kiongozi huyo yeye ndio atajua namna atakavyotekeleza majuku yake ya kazi.
 
Ili wasivunje hiyo sheria ni suala la kuirekebisha ili wapewe upendeleo. Very simple.
 
Vifo vitokanavyo na ajali vitawatia adabu, wala wasihangaike na hao madereva, kama wanajiona miungu watu kwa kuvunja sheria za barabarani bila kuogopa polisi, wajue tu vifo haviwaogopi wao.
 
Kamanda Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema baadhi ya madereva wanavunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za Serikali kama STK, STL, SM, PT na kulindwa na viongozi wanaowaendesha.

Amesema baadhi ya madereva hawafuati taaluma zao na wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema " Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwani dereva akiwa wa hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,”.

=======================

Kamanda Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi amesema wapo baadhi ya madereva wa Serikali ambao wanaendesha kwa kiburi magari yao huku wakivunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za STL, SM, PT na viongozi wanaowaendesha na sio taaluma.

Amesema baadhi ya madereva hao wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya madereva wa Serikali ili kuwakumbusha utii wa sheria za usalama barabarani na udereva wa kujihami utakaosaidia kupuza ajali.

“Sisi madereva wa Serikali ndio wenye matatizo, baadhi yao wengi wanafanya vizuri. Yaani wao kinachowafanya waendeshe magari na kile kiburi cha kuvunja sheria ni kwasababu wanamuendesha kiongozi fulani au ofisa fulani,” amesema.

Kamanda Bukumbi amesema jeshi hilo litaendelea kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria za usalama barabarani bila kujali anamuendesha nani.

“Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa kwanza unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwa sababu dereva anafanya hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,” amesema Bukumbi.

Amesema kama dereva anavunja sheria na kiongozi wake anamuona lakini hachukui hatua maana yake anaidhalilisha nafasi yake, taasisi na idara anayofanyia kazi.

Awali, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoani Iringa, Mosi Ndozelo amesema hakuna dereva aliye juu sheria.

Amesema madereva wa Serikali wanapaswa kutii sheria zilizopo na kwamba wanaamini mafunzo hayo yatawabadilisha mtazamo.

“Wanaojiona wapo juu ya sheria kupitia mafunzo haya wataweza kubadilika, tunataka kuwabadilisha wenye mawazo mgando kwamba wakiendesha viongozi au magari ya Serikali basi wapo juu ya Sheria,” amesema.

Kwa upande wao baadhi ya madereva walisema sio wote wanaovunja sheria za usalama barabarani japo baadhi yao wamekuwa wakifanya hivyo kwa kivuli cha viongozi au namba za magari wayayotumia.

“Binafsi najua natakiwa kuwa kioo na kwa kweli huwa sipendi kuvunja sheria, natumia udereva wa kujihami ambao naweza kuepusha ajali kwangu na wanaonizunguka,” amesema Mohamed Maghembe, derva wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini.

MWANANCHI
Ni kweli kabisa na kinachagizwa na viburi vya madaraka vya viongozi wa serikali, umma, majeshi, wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa na mabalozi ni balaa iwanajiona barabara ni za kwao spidi zaidi ya 180Km kwa saa, wana over take popote, mlimani, kwenye kona, kwenye mteremko na kwenye makzi.

Wako juu ya sheria polisi wa trafiki akiashiria mkono kusimama anawashiwa taa kisha mwendo unaongezeka; hawasimami kamwe.

Gari za serikali hazina bima na kuna baadhi ya wananchi huwa wanadanganywa sana na watu kupanda magari hayo wakati wanasafiri ili wafike haraka na matokeo yake wanafikishwa haraka kuzimu na hakuna fidia
 
Kamanda Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema baadhi ya madereva wanavunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za Serikali kama STK, STL, SM, PT na kulindwa na viongozi wanaowaendesha.
Juzi hapa nilitaka kugongana na Land Cruiser STL uso kwa uso kule Mbezi Beach karibu na BOT flats. Ilikuwa mida ya saa moja na nusu usiku, kuna foleni jamaa akaamua kutanua huku anaendesha kwa kasi. Kufumba na kufumbua nakuta STL iko mbele yangu upande wangu. Nilishika breki za ghafla lakini gari ya nyuma yangu ikanigonga nyuma. Nashukuru gari yangi ilipata michubuko kidogo tu kwenye bampa. Jamaa wa STL wala hata hakusimama, katimua mbio

Kuna mtu alisema kama una bima ya hakika na hauko kwenye mwendo mkali usimkwepe, acha mgongane, hasa kama una gari kubwa. Sasa natafuta gari ya zamani iliyochoka niwape fundisho! Kwa hiyo mkisikia nimegonga gari ya Katibu Mkuu, sijui Mkurugenzi iliyokuwa inatanua msishangae, ni mimi!
 
Vifo vitokanavyo na ajali vitawatia adabu, wala wasihangaike na hao madereva, kama wanajiona miungu watu kwa kuvunja sheria za barabarani bila kuogopa polisi, wajue tu vifo haviwaogopi wao.
Shida ni kwamba wanatuua na sisi tusiokuwa na hatia kupitia kiburi chao.
Hongera kwa Kamanda Bukumbi kuliona hilo na kulisema hadharani, pengine na wengine wataamka na kuchukua hatua ili kupunguza ajali na vifo vya barabarani.
 
mwisho zinawasokota wote dereva na boss wake wanatupa kazi yakupasua ayo mav8 na shoka kuwatoa
 
Kamanda Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema baadhi ya madereva wanavunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za Serikali kama STK, STL, SM, PT na kulindwa na viongozi wanaowaendesha.

Amesema baadhi ya madereva hawafuati taaluma zao na wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema " Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwani dereva akiwa wa hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,”.

=======================

Kamanda Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi amesema wapo baadhi ya madereva wa Serikali ambao wanaendesha kwa kiburi magari yao huku wakivunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za STL, SM, PT na viongozi wanaowaendesha na sio taaluma.

Amesema baadhi ya madereva hao wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya madereva wa Serikali ili kuwakumbusha utii wa sheria za usalama barabarani na udereva wa kujihami utakaosaidia kupuza ajali.

“Sisi madereva wa Serikali ndio wenye matatizo, baadhi yao wengi wanafanya vizuri. Yaani wao kinachowafanya waendeshe magari na kile kiburi cha kuvunja sheria ni kwasababu wanamuendesha kiongozi fulani au ofisa fulani,” amesema.

Kamanda Bukumbi amesema jeshi hilo litaendelea kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria za usalama barabarani bila kujali anamuendesha nani.

“Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa kwanza unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwa sababu dereva anafanya hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,” amesema Bukumbi.

Amesema kama dereva anavunja sheria na kiongozi wake anamuona lakini hachukui hatua maana yake anaidhalilisha nafasi yake, taasisi na idara anayofanyia kazi.

Awali, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoani Iringa, Mosi Ndozelo amesema hakuna dereva aliye juu sheria.

Amesema madereva wa Serikali wanapaswa kutii sheria zilizopo na kwamba wanaamini mafunzo hayo yatawabadilisha mtazamo.

“Wanaojiona wapo juu ya sheria kupitia mafunzo haya wataweza kubadilika, tunataka kuwabadilisha wenye mawazo mgando kwamba wakiendesha viongozi au magari ya Serikali basi wapo juu ya Sheria,” amesema.

Kwa upande wao baadhi ya madereva walisema sio wote wanaovunja sheria za usalama barabarani japo baadhi yao wamekuwa wakifanya hivyo kwa kivuli cha viongozi au namba za magari wayayotumia.

“Binafsi najua natakiwa kuwa kioo na kwa kweli huwa sipendi kuvunja sheria, natumia udereva wa kujihami ambao naweza kuepusha ajali kwangu na wanaonizunguka,” amesema Mohamed Maghembe, derva wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini.

MWANANCHI
Okay
 
sio namba tu.
kuna uzi humu nilieleza kuhusu aina za gari za serikali wanazotumia ukimiliki mtu binafsi utaishi bila shida.

Ila nahisi Mod aliufuta japo tunaeleza uhalisia
 
Juzi natoka morogoro kuja dar njiani nimekutana nao wengi sana wapo rough sana. Nadhani sheria za usalama barabarani tulitungiwa sisi walala hoi.
 
Back
Top Bottom