Polisi: Madereva wa Serikali wana kiburi sababu ya Namba za Magari yao

Polisi: Madereva wa Serikali wana kiburi sababu ya Namba za Magari yao

Hili jambo la madereva wa serikali lina ishushia heshima serikali yenyewe na viongozi wanaondeshwa. Huwezi kuwa kiongozi wa serikali alafu unachekelea dereva aki-overtake kwenye mlima au kona kali. Akili za hao viongozi zipimwe.
 
Kamanda Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema baadhi ya madereva wanavunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za Serikali kama STK, STL, SM, PT na kulindwa na viongozi wanaowaendesha.

Amesema baadhi ya madereva hawafuati taaluma zao na wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema " Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwani dereva akiwa wa hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,”.

=======================

Kamanda Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi amesema wapo baadhi ya madereva wa Serikali ambao wanaendesha kwa kiburi magari yao huku wakivunja sheria za usalama barabarani kwa sababu ya namba za STL, SM, PT na viongozi wanaowaendesha na sio taaluma.

Amesema baadhi ya madereva hao wanajiamini kuzidi kiwango huku wakifanya makosa licha ya kujua wazi kwamba wanavunja sheria za usalama barabarani na kuhatarisha maisha ya wengine.

Kamanda Bukumbi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya madereva wa Serikali ili kuwakumbusha utii wa sheria za usalama barabarani na udereva wa kujihami utakaosaidia kupuza ajali.

“Sisi madereva wa Serikali ndio wenye matatizo, baadhi yao wengi wanafanya vizuri. Yaani wao kinachowafanya waendeshe magari na kile kiburi cha kuvunja sheria ni kwasababu wanamuendesha kiongozi fulani au ofisa fulani,” amesema.

Kamanda Bukumbi amesema jeshi hilo litaendelea kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria za usalama barabarani bila kujali anamuendesha nani.

“Kwa kuendesha gari bila utii unakuwa kwanza unamdhalilisha kiongozi unayemuendesha kwa sababu dereva anafanya hovyo hovyo hata kiongozi tunamtafsiri kwamba na yeye ni wa hovyo hovyo kwa sababu anapaswa kumsimamia dereva wake,” amesema Bukumbi.

Amesema kama dereva anavunja sheria na kiongozi wake anamuona lakini hachukui hatua maana yake anaidhalilisha nafasi yake, taasisi na idara anayofanyia kazi.

Awali, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoani Iringa, Mosi Ndozelo amesema hakuna dereva aliye juu sheria.

Amesema madereva wa Serikali wanapaswa kutii sheria zilizopo na kwamba wanaamini mafunzo hayo yatawabadilisha mtazamo.

“Wanaojiona wapo juu ya sheria kupitia mafunzo haya wataweza kubadilika, tunataka kuwabadilisha wenye mawazo mgando kwamba wakiendesha viongozi au magari ya Serikali basi wapo juu ya Sheria,” amesema.

Kwa upande wao baadhi ya madereva walisema sio wote wanaovunja sheria za usalama barabarani japo baadhi yao wamekuwa wakifanya hivyo kwa kivuli cha viongozi au namba za magari wayayotumia.

“Binafsi najua natakiwa kuwa kioo na kwa kweli huwa sipendi kuvunja sheria, natumia udereva wa kujihami ambao naweza kuepusha ajali kwangu na wanaonizunguka,” amesema Mohamed Maghembe, derva wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini.

MWANANCHI
Kidogo Jeshi la wananchi wao hujitahidi kufuata sheria za usalama barabarani ingawa nao wana ushamba fulani barabarani na kaubabe ka kijinga, mimi Dereva wao mmoja niliwahi kumfundisha adabu maeneo ya Masika Morogoro akiwa na vile vibasi vyao viashok vifupi, ili ajifunze kuwa naye ni raia kama walivyo wengine katika matumizi ya barabara., nisisimulie ilivyokuwa naweza kudisclose ID yangu.

Ukija kwa hawa PT mh kufuata sheria za usalama barabarani kwao ndo kama wenzao Tiss ambao nao wanajikutaga miungu watu kwa barabara, bahati nzuri chuma yangu ni Prado iliyoapgrediwa to LX imekula ngao mbele ngao nyuma, huwa sikwepeshi ukija njoo tu!

Ambao hujitahidi kidogo kufuata sheria ni magereza, fire na uhamiaji. Hawa huwa wana hofu kidogo ya kuchukuliwa hatua hivyo hufuata sheria.

ST( K,L, na M), hawa SU, SM ndo wa hovyo sana huko barabarani hasa hawa ST! Ila kwangu wanaisomaga namba! Afu tunamalizana huko huko juu kwa ju, ukileta utabe ndo tunafikishana kwa maboss zako ambao wananywea na kukuachia msala uusolve mwenyewe
 
Back
Top Bottom