SIMU YA TOCHI
JF-Expert Member
- Dec 12, 2014
- 1,385
- 894
Ikiwa ni muendelezo wa taharuki na hofu ya serikali, jeshi la polisi mkoani Mara limeingia kwenye jaribu jingine la kutumika na serikali kuwashughulikia wanachama na viongozi wowote ambao wataonekana au watahisiwa wanaratibu zoezi la UKUTA kuelekea Sept1.
Hali hii imejitokeza baada ya mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mara Mh Vincent Nyerere akitokea Butiama kwenye mazishi kuelekea nyumbani kwake Musoma Mjini, vijana wa bodaboda walipomuona walilazimika kuunga msafara na kumsindikiza jambo hili lilimchefua moja wa afisa wa jeshi la polisi na ikapelekea kuagiza kikosi maalumu ili walishughulikie suala hilo, kutokana na Mh Nyerere kupata taarifa hii mapema kutoka kwenye chanzo cha jeshi la polisi moja kwa moja ilimlazimu asiingie katikati ya mji wa Musoma na kuamua kurudi kata ya bweri Musoma mjini anapoishi ili kuwaokoa vijana ambao walikuwa wanatakiwa kuja kushughulikiwa na jeshi la polisi.
Ikawa ni kauli mbiu kila muda atapotoka nyumbani kwenda mahala popote ililazimika polisi kufuatilia nyendo zake ili wajue ametoka kwake kwa sababu gani na huko anakoenda anaenda kufanya nini
Ikumbukwe katika kipindi cha uchaguzi ni hawahawa baadhi ya wakubwa wa polisi walikuwa wakiwalazimisha polisi wadogo kupiga mabomu wanachadema waliokuwa wakitembea kumsindikiza mgombea baada ya mikutano, ni hawahawa wakubwa wa polisi walishiriki na kutumia baadhi ya watu kutega vilipuzi ndani ya gari ya mgombea ili kummaliza, ni hawa hawa wakubwa wa polisi walikuwa wanawaachia vijana wa CCM waliokuwa wanawashughulikia kwa mapanga wafuasi wa CHADEMA, ni hawahawa wakubwa wa jeshi la polisi waliahidiwa kupewa milioni 40 endapo wataisaidia CCM kushinda jimbo la Musoma Mjini.
Yapo mengi sana ya kusema ila kwa leo tuishie hapa ngoja tuone movie itavyoendelea.