Watu wanne ambao ni wanachama wa Taasisi ya Wanafunzi wa CHADEMA(CHASO) wamekamatwa na wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kukutwa wakipanga na kuhamasisha watu kufanya vurugu.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema wanaoshikiliwa kuwa ni Noah Mwalwange, Mwenyekiti vijana wa CHADEMA vyuoni (CHASO) Mkoa wa Mbeya, Gwamaka Mboka ambaye ni Katibu CHASO Mkoa wa Mbeya, Agustino Wasinyo, Mwenyekiti wa CHASO tawi la CUOM na Rojas Mpwani mwanachuo CUoM.
Watuhumiwa hao walikamatwa Julai 04, 2026 majira ya saa 10 jioni katika eneo la Mafiati lililopo Kata ya Maanga, Jijini Mbeya.
SACP Kuzaga amesema ushahidi unakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria zifuatwe dhidi ya wanne hao.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa limetoa wito kwa wananchi kuacha kujiingiza kwenye vitendo vya kupanga na kuhamasisha uhalifu katika mkoani Mbeya kwa maelezo kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.