Polisi mnataka kutuaminisha Panya Road wamewazidi kete?

Polisi mnataka kutuaminisha Panya Road wamewazidi kete?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Habari wakuu,

Inasikitisha na kutia hasira kuona tumefikia huku na tunasema kila siku jeshi letu ni kiboko. Kweli Panya Road ndiyo wameshindikana kiasi hiki mpaka kufikia mtu anapoteza uhai na nyie mpo?!

Ama huu ni mchongo wa mtu unaoibuliwa kila akitaka kupata maslahi yake anayoyajua mwenyewe?! Polisi na Wizara husika mnatuangusha, na mpaka sasa hakuna aliyewajibika kwa tukio la jana, aaaah Tanzania yangu!

"Ingekua ni watu fulani wangeshatulizwa dakika 0", alisikika mlevi akirudi kwake asubuhi.
 
Kwamba:

"Ingekua ni watu fulani wangeshatulizwa dakika 0"

Ni dhahiri kuwa wana ubaguzi kinyume na viapo vyao. Hapo ni sisi mabosi wao kufanya maamuzi magumu.

"Wakale wanakopeleka mboga."
 
Ama huu ni mchongo wa mtu unaoibuliwa kila akitaka kupata maslahi yake anayoyajua mwenyewe?! Polisi na Wizara husika mnatuangusha, na mpaka sasa hakuna aliyewajibika kwa tukio la jana, aaaah Tanzania yangu!
Shida ni hao wahusika wa hilo eneo waulizwe vizuri tatizo limeanzia wapi, huo unaitwa msako wa nyani sio panyaroad kuna shida pahala alafu kabla hauja-conclude jambo jaribu kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi wa kina ujiulize nini shida chanzo ni nini?

Kwanini washambuliwe wao na sio vinginevyo?

Pia kingine mlinzi namba 1 ni wewe, ndio maana kukiwa na tukio lolote lenye kuhatarisha maisha ya raia unaripoti kituoni kulinda usalama, je wewe umechukua hatua gan kabla ya kuwalaumu polisi?
 
Naona uzembe wa watu wa dar umezidi Sasa wale wananchi wenye hasira kali walikufa vitani
 
Shida ni hao wahusika wa hilo eneo waulizwe vizuri tatizo limeanzia wapi.. huo unaitwa msako wa nyani sio panyaroad kuna shida pahala alafu kabla hauja-conclude jambo jaribu kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi wa kina ujiulize nini shida chanzo ni nini?
Kwanini washambuliwe wao na sio vinginevyo?

Pia kingine mlinzi namba 1 ni wewe, ndio maana kukiwa na tukio lolote lenye kuhatarisha maisha ya raia unaripoti kituoni kulinda usalama, je wewe umechukua hatua gan kabla ya kuwalaumu polisi?
Nimesikitishwa na mchango wako.Kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao,kitendo cha raia kuvamiwa wakiwa majumbani hakikubaliki,ni dhahiri kuwa jeshi letu imara la polisi linatakiwa kulichukulia jambo hili kwa tahadhari kubwa.

Vyombo vyetu vinuse hatari na kuzishughulikia kabla hazijaleta madhara kwa wananchi
 
Panya road ni majirani zenu ni watu mnaoishi nao mitaani intelijensia inaanzia kwenu nyi nyi mkikaa kimya Polisi kazi yao itakuwa ngumu kataeni wahalifu from the roots kamata wakateni koo muone kama kutakuwa na hao panya road
Jibu lako hili hapa ☝️maana naona huelewi Girland
 
Ukikutana na kadhia ya hawa madogo aisee sio nzuri.

Kumbuka ni ambush!
 
Matukio haya yamekuwa yakiripotiwa kila kukicha,tatizo liko wapi? Chanzo chake ni nini?
Chanzo ni nyinyi wananchi wenyewe WAOGA WAOGA ndio maana mnaonewa na vitoto vidogo bila kuchukua hatua yoyote, hamna ushirikiano mnasubiri tukio litokee mpate story za kuandika mtandaoni.. ulinzi wa raia na mali zao unaanza na wewe.. yaan wewe usikie kelele za mwizi mwizi alafu ukae tu hauchukui hatua yoyote kisha baada ya tukio uanze kulaumu polisi hawafanyi kazi za kulinda raia na mali zao huo ni uzwazwa
 
Wanakuaga na AKILI za kipuuzi mnooooo kuwakamata Wapinzani kwa kisingizio Cha "interejensia ya Geshi Ra Porisi"
 
Chanzo ni nyinyi wananchi wenyewe WAOGA WAOGA ndio maana mnaonewa na vitoto vidogo bila kuchukua hatua yoyote, hamna ushirikiano mnasubiri tukio litokee mpate story za kuandika mtandaoni.. ulinzi wa raia na mali zao unaanza na wewe.. yaan wewe usikie kelele za mwizi mwizi alafu ukae tu hauchukui hatua yoyote kisha baada ya tukio uanze kulaumu polisi hawafanyi kazi za kulinda raia na mali zao huo ni uzwazwa
Umekula maharage ya wapi mkuu?
 
Elimu na malezi bora kwenye jamii vimepungua.

Utandawazi umezidi kuuwa tamaduni za jamii.

Matatizo ya kiuchumi na migogoro katika familia inachangia hili
 
Back
Top Bottom