Polisi mnataka kutuaminisha Panya Road wamewazidi kete?

Polisi mnataka kutuaminisha Panya Road wamewazidi kete?

Mkuu unasikitisha sana kuandika mambo ya kufikirika. Katika mazingira kama hayo ya ambush tena vibaka 30 waliopinda kwelikweli, mnajiorganise vipi na kila mtu yuko ndani kwake. Ukitoka mmoja mmoja ni halali yao, wengi kwao jela ni nyumbani. Acha utani na waambie Polisi wawajibike. Mpaka uwapigie simu hao panya road bado wanawasubiri tu. Usichukulie mambo kiuepesi hivyo
Hivi mkuu ngoja nikuulize swali la darasa la pili 30 na 100 ipi kubwa?
 
Mkuu unaandika mambo mengi ya kufikirika, kiuhalisia hao watoto ni hatari sana na ni kikundi kamba mbwa mtu. Lakini pia wewe ndiye umetumia neno zwazwa dhidi yetu, ndo maana nikakujibu nilivyokujibu. Tumia Lugha ya staha ili mjadala uwe na tija, tushapoteza mtanzania mwenzetu.
Sawa nmeshakuelewa mkuu..
 
Hivi mkuu ngoja nikuulize swali la darasa la pili 30 na 100 ipi kubwa?
Hao 100 wamevamiwa ghafla na ni kazi ya madakika tu, wanajiorganise vipi na wapi? Kumbuka huo mtaa waliovamiwa juzi kuna walinzi na wanalipwa na kila kaya kwa mwezi.
 
Hao 100 wamevamiwa ghafla na ni kazi ya madakika tu, wanajiorganise vipi na wapi? Kumbuka huo mtaa waliovamiwa juzi kuna walinzi na wanalipwa na kila kaya kwa mwezi.
Km kuna walinzi na ulinzi unaanza na wewe daaah sijui nikuelezeeje unielewe au basi wewe baki na kile unachokielewa maana hata nikikueleza hautaweza kunielewa
 
Ninachoona sahihi wakati jeshi likihangaika kutatua hili tatizo la hawa washenzi ni vizuri wananchi kuchukua hatua stahiki kabla ya tukio. precautions.
Au kama unaona wewe hauwezi chochote na haupendi vita au ugomvi basi wakija usifanye chochote, waache wakumalize tu.
Ila kwa wale wanaotaka kujihami basi unaweza soma hapa. Ni survival of the fittest. The weak will be eradicated.

Mimi usiku huwa nalala nikiwa macho yaani hata mtu akipiga chafya nje naamka. hivyo cha kwanza hakikisha usiku haulali kama umekufa.
Kwanza ongeza komeo kwenye mlango, kitasa pekee hakitoshi. unataka kufa? kama hautaki kufa basi weka komeo nzito zaidi ya nne.
Kuwa mtu wa mazoezi ya kujaza misuli na kuongeza nguvu ikiwemo boxing na kujifunza matumizi ya silaha za kawaida ikiwemo stick za chuma (kama hujasikia basi nakwambia kuanzia sasa tupo somalia officially)
Kuwa na namba za polisi na namba ya nyumba yako na majina ya mtaa wako uyajue vizuri.

Ukisikia kelele zozote nje basi tafadhali usitoke nje bali haraka chukua kitu chochote kizito na uweke mlangoni iwe sofa, kochi au meza zile nzito na ushikilie hapohapo mlangoni kama watoto waende chumba cha wazazi na mama yao au iwe kawaida kuanzia sasa kuweka kitu kizito mlangoni. baba atafanya yote hayo.
Na kwa wakati huo hakikisha una silaha mkononi iwe panga au nondo na hakikisha mwili uwe fit sio mfuga kitambi au imekula kwako na kingine wale wapuuzi hawana nguvu sababu ya mlo duni na uvutaji wa madawa na bangi bali wanategemea wingi wao na silaha.

Wakati wewe unafanya hayo basi mama au watoto kwa wakati huo wanatakiwa wawe wameshapiga simu polisi na kutaja eneo husika kwa uhakika ikiwemo namba ya nyumba. kwa muda utakaoweza kushikilia mlango basi kuna uwezekano wataacha sababu muda unaenda au wataendelea lakini kizuri kwa wakati huo polisi watakuwa njiani.
Na sema kwa nguvu kwamba nimeshapiga simu polisi wapo njiani.

Likitokea la kutokea na wakafanikiwa kuingia ndani basi kumbuka kwamba hawawezi kuingia ndani kwa pamoja hivyo utachagua ukimbilie ndani kwa mkeo au kwa wale wasioogopa kufa watasimama hapo hapo mlangoni na kumuwahi yoyote atakayetanguliza fuvu. au utarudi nyuma huku ukiwa umesimama na kusubiri atakayekuanza au utaawambia wachukue wanachotaka ila atakayesogea utakufa nae na utawaambia tayari nimeshapiga simu polisi.

Kwenye situation au hali kama hiyo mwili unakuwa kwenye adrenaline rush au wanaita adrenaline momentum maana yake mwili utakuwa unatetemeka hasa miguu na jasho linavuja haswa kwa uoga wa kufa na mapigo ya moyo kukimbia faster zaidi ya engine ya formula 1, kuna mawili wale wenye moyo na roho dhaifu na nyepesi wanaweza kuishiwa nguvu na kwa wale moyo wa chuma na roho za simba kama mimi mwili unakuwa na nguvu kuliko kawaida. mimi nikiwa kwenye hali ya kuhatarisha maisha yangu nakuwa sio muoga tena bali hasira za ajabu na mwili unakuwa na nguvu mara mbili. nakuwa beast siangaliki mara mbili ni zaidi ya mnyama na natumia hasira kama silaha na motivation ukinisogelea basi lazima mmoja kati yetu aende chini na ukichangia ni mtu wa mazoezi na malezi yangu ni vita tosha. Ila siku moja nikikamata mmoja kati ya hawa nguruwe nitamtoa macho kwa mikono yangu miwili.

Wale lone wolfs basi utafanya kila kitu mwenyewe kudadadeki au ukishindwa kwa kuwa ni mayai mayai umelegea kama kamasi basi kajifiche chini ya uvungu wa kitanda au subiri kubutuliwa mpaka ufe au kesho uamkie hospitali mahututi. Nilichogundua ni watanzania ni waoga sana ila hiki yoyote ataweza kufanya akiwa ndani kwake.
Ila siku moja nikikamata mmoja kati ya hawa nguruwe nitamtoa macho kwa mikono yangu miwili.

Serikali na Majeshi yote tafadhali fanyeni wajibu wenu la sivyo nchi itateketea kwa kundi la watu wachache.
 
Kamanda wa Police DSM,MKUU WA MKOA NA WILAYA .. kwa kweli hili jambo linatuumiza kweli mpaka aibu nchi jirani ikitokea siku panya road wanamiliki hata bastola 3 hapo police, mgambo,sungusungu na wengine hawataliongelea hili swala hivi kwanini juzi watu wanapiga simu kuomba msaada kuwa panya road wameingia ninyi mpo kimya jamani hata kuomba vijana wa jkt mgurani hapo, au ma kamanda gongo la mboto , na kwingine Kuja kusaidia raia hamfanyi mwisho Dada yetu anapoteza maisha kizembe na watu wanamuangalia tu inauma Sana hata Kama police mafunzo yenu kama hamyaamini ombeni msaada jeshini Kuna servicemen wanakiu na ajira hatari wakisikia Kuna insue hapo ndo wanataka watu majina kufa na kupona inauma kwa kweli NA KUMILIKI SILAHA SHERIA NI NGUMU MLIZOZIWEKA
 
nlisikia mpangaj akisema eti , panya road waliambiana muda umeisha muda umeisha then walipoondoka , dk 20 mbele ndo wanakuja polisi , its like a plan eti kutuzuga
Ni mradi wa maaskari wa Dar kupiga Pesa...siwaamini Askari kabisa yaani wanajua wanachofanya hao panya road na polisi wanawajua vzr tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom