Polisi msilete ubaguzi na uchonganishi, "Gaidi mfia dini" ndio nani?

Sasa gaidi gani anaeuwa polisi tu bila kuangalia dini ya mtu! Gaidi gani alieamua kuacha wananchi na alikuwa anauwezo wa kuwauwa..??!!
Jamaa Kama angetaka kuleta msiba wa taifa siku hiyo angeuwa watu wengi sana!,namalizia tu mtu hujikuna panapomuwasha! Hamza nae alifanya hivyohivyo!.
 
Nmeshindwa kuelewa uchunguzi wa polisi,"Hamza amejifunza ugaidi mtandaoni"
Then? Bado tumebaki na maswali mengi ambayo hayajajibiwa na huu uchunguzi
1.Nani yupo nyuma ya hamza "mdhamini"?
2. Kwann aue polisi tu?
3.Wapi alipojifunza,nchi au eneo,washirika wake ni kina nani?
4.Kusema amejifunza mtandaoni,kwenye site zp? Alidukuliwa before or after kupitia anachofanya akiwa mtandaoni au ni guessing tu?
Maswali ni mengi...
 
Hii kitu UGAIDI serikali ya Ccm na polisi wa Ccm wana ichukulia ni jambo rahisi sana. Lakini hili neno Gaidi ni baya sana. Sijui wana taka kuipeleka wapi Tz. Neno Gaidi sio sifa.
Nilimuamini sana Wambura lakini kwa hii kauli yake ya leo naomba niwe kinyume na yeye. Niseme Biiiiggggg No!!!!
 
Hiyo ndio aina ya viongozi tuliojaaliwa na mwendazake, roho ya marehemu iwekwe panapostahili, roho ya marehemu Hamza ipate Rehema kwa Mungu ipumzike kwa Amani Amina.
We mjinga sana mwendazake anahusika nini hapo?
 
Naona siku hizi magaidi wana roho za pekee sana. Wanachagua kabisa nani wamuue nani wamuache! [emoji848]
 
Bora angesema ni mccm mfia chama..
Kuliko kuhusianisha dini ya mwenyezi Mungu na ugaidi.
Kwa hili nasimama na uislamu
Wamesema mfia dini hawajataja dini

Kila mtu ana dini yake ya kibinafsi hamza alikuwa na dini yake ya kibinafsi yenye tafsiri anayoijua yeye

Kama ni uislamu alikuwa na wa kwake wa tafsiri yake aijuaye mwenyewe .Hiyo dini yake ndio kaifia

Polisi wako sahihi kabisa
 
Akajifunza mtandaoni hadi kuitumia bastola , akaendelea kutumia google hadi akafanikiwa kuua askari wawili kachukua Ak 47 akaingia tena google akajifunza kulenga kukoki kulala chini kutambaa, aisee haya DCI una akilio sana we mtu
 
Ndio alikuwa gaidi mfiadini ile dini ya haki,huko Nigeria, Somalia, Syria, Mozambique n.k ni wao tu wanapigania dini ya haki kwa kuuwa wengine wanaita jihad

USSR
 
Kwa uelewa wangu ametajwa Hamza kuwa ni gaidi mfia dini, haijasemwa kwamba waislam ni magaidi wafia dini, hapo ametajwa MTU Individual ! Sasa hapo kuna tatizo gani ? Acheni uchonganishi Bandugu !!!
 
Dahwa yao inachemka hawaoni mwenzao Ndugway kashaanza kubwabwaja , Haalbadir sio kitu cha mhezo , Inalillayih wa inayilaahiy Rajiuun Sirro+Wambura
hizo albadir whatever it is.. zingekuwa zinafanya kazi nadhan wangeshabadilika tabia.
the truth ia hawatobadilika ng'o
 
Kuna wale wanasema magaidi wote Ni waislam Ila waislam wote siyo magaidi.
Mf: Abubakar mbowe.
 
Akajifunza mtandaoni hadi kuitumia bastola , akaendelea kutumia google hadi akafanikiwa kuua askari wawili kachukua Ak 47 akaingia tena google akajifunza kulenga kukoki kulala chini kutambaa, aisee haya DCI una akilio sana we mtu
Yani bado ametuacha na maswali kibao
 
Kwa uelewa wangu ametajwa Hamza kuwa ni gaidi mfia dini, haijasemwa kwamba waislam ni magaidi wafia dini, hapo ametajwa MTU Individual ! Sasa hapo kuna tatizo gani ? Acheni uchonganishi Bandugu !!!
Shida yangu kama nilivyoitaja hapo kwenye comment yangu ni kwamba kwa kuwa Polisi walihisiwa na wananchi katika kuhusika kwenye sakata la bwana Hamza ilipaswa iundwe tume huru ya kuchunguza tukio hili na wala siyo polisi kujichunguza wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…