KERO Polisi Mtwara acheni tamaa mnatukwamisha, sisi pia tupo kazini na tuna familia

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Inasikitisha sana siku hizi polisi kama nchi ni ya kwao kabisa.! As if Serikali imeshawapa ruhusa ya wanachokifanya. Mikoa mingine sijui, hapa Mtwara Kilimanjaro kuna hawa polisi wanatoza tu hela kwa wenye magari hata kama huna kosa sijui tuwaite watoza ushuru au polisi maana mauza uza uza tu.

Kuna hawa wa Mitengo yaani wanataka hela kwa lazima sh 5,000 kila bajaji kweli!

Sasa bajaj kutoka Mkanaled mpaka Mikindani bajaj inaingia abiria wanne ambao ni elfu 4 halafu utoe elfu tano bila kosa lolote huu ni uonevu wa hali ya juu na huku ni kujinufaisha wao tu.

Kuna hawa wengine hapa Mangamba njiani kama unaenda ziwani, hawa askari hapa imekuwa kama upatu kila gari la mchanga wanachukua elfu 5 na hii ni kila siku. Hata kama huna kosa lolote na wanakuambia kabisa tukuandikie kosa elfu 30 au utoe elfu 5.

Tumerudi zama za kikoloni mno

Tunaomba msaada Mtwara askari wanatajirika kupitia madereva

Askari wa Mangamba, Mitengo, na Kilimanjaro wanatunyonya mno

Siku yake nitakuja na picha na videos za hawa askari wetu.
 
Mkuu huna kosa unatoa pesa ya nini???
Si ukubali kwenda kituoni kisha mahakamani ukatetee haki yako??,kama unahisi huna muda basi malalamiko yako yote yanakosa maana hapa maana unatoa kwa hiyari yako.

Polisi wanatumia uzembe na mapuuza yenu kujinufaisha.
 
Njia ya kuondoa Huu ni polisi avae camera muda wote ili chochote anachofanya kionekane Kwa umma na kuwashughulikia kirahisi.tuwaige wa marekani na wanywarwanda
 
Naam hili nalo ni idea, kama wanavyofanya marekani. Nadhani itakomesha kama si kupunguza tabia mbaya kama hizi
 
Mkuu huna kosa unatoa pesa ya nini???
Si ukubali kwenda kituoni kisha mahakamani ukatetee haki yako??,kama unahisi huna muda basi malalamiko yako yote yanakosa maana hapa maana unatoa kwa hiyari yako.

Polisi wanatumia uzembe na mapuuza yenu kujinufaisha.
Kaka kama hujawahi drive kwa safari za kila siku au ndefu , hawa jamaa japo si wote wana njaa isiyo elezeka. Arusha walikuwepo wa mianzini, wale huwa wanafanya kama ni biashara kabisa, tena wana confidence kabisa as if ni halali
 
Ni Mwendo wa malalamiko na waliopewa dhamana ya kuleta ustawi wa jamii nao wamo humo, CCM hii si nzuri.
 
Pole sana,hao jamaa ni changamoto sana.

Maeneo mengi nchini wanawalalamikia na Serikali ni kama imewaruhusu maana yake hakuna hatua yoyote inayochukuliwa kutatua changamoto kama hizo za wananchi.

Vitu kama hivi ndivyo vinavyosababisha wananchi wasiwe wazalendo kwa nchi yao.

Nchi hii ina mambo mengi ya ajabu sana!!
 
Mkuu huna kosa unatoa pesa ya nini???
Si ukubali kwenda kituoni kisha mahakamani ukatetee haki yako??,kama unahisi huna muda basi malalamiko yako yote yanakosa maana hapa maana unatoa kwa hiyari yako.

Polisi wanatumia uzembe na mapuuza yenu kujinufaisha.
mkuu upo serious kwamba dereva bajaji apelekane na polisi mahakamani. hujui huo ni upotevu wa muda na hiyo bajaji si yake na inahitaji marejesho. mahakamani which? hujui huko unaweza endesha kesi hata miaka miwili. ipo siku utaambiwa hakimu kaenda likizo ya uzazi hadi arudi
kutoa tu ushahidi mahakamani ni kero ,kila ukienda kesi imeahirishwa
 
Kinachoniuma sana ni hawa wanaojiita PCCB hawa utendaji kazi wao mie siuoni kwa zile asilimia hata 50. Haya malalamiko yapo kila siku.. miaka nenda rudi.. kwanini wasimalize hiii shida?

Ingawa ktk ripoti TAASISI inayoongoza kwa rushwa ni Polisi namba moja. Iko wazi

Sasa mlinzi wa Raia ndio huyo huyo mla rushwa. Tutafika kwel?
 
Isitoshe ukienda polisi hutoki kwa hiyo elfu 5 tena, na ukifika kule kesi inabadilishwa. Kuna mtu alikamatwa na pikipiki ndogo alivyofika polisi kesi ikaandikwa amekamatwa barabara ya mwendo kasi , akabaki anashangaa.
 
Samahani ndugu acha kuufananisha ukoloni na upumbavu.
Enzi za ukoloni haki na maadili kwa wafanyakazi vilikuwa juu.
 
Kinachoniuma sana ni hawa wanaojiita PCCB hawa utendaji kazi wao mie siuoni kwa zile asilimia hata 50. Haya malalamiko yapo kila siku.. miaka nenda rudi.. kwanini wasimalize hiii shida?

Ingawa ktk ripoti TAASISI inayoongoza kwa rushwa ni Polisi namba moja. Iko wazi

Sasa mlinzi wa Raia ndio huyo huyo mla rushwa. Tutafika kwel?

PCCB na polisi ni mtu na dadake, ni wale wale.
 
Isitoshe ukienda polisi hutoki kwa hiyo elfu 5 tena, na ukifika kule kesi inabadilishwa. Kuna mtu alikamatwa na pikipiki ndogo alivyofika polisi kesi ikaandikwa amekamatwa barabara ya mwendo kasi , akabaki anashangaa.
Wanakukomoa kusudi siku nyingine uamue kumalizana nao kabla ya kufika kituoni.
 
Kero namba moja ya maendeleo bongo Polisi. Zamani ilikuwa TRA ila kwa mbaaaaaaaali wana afadhali
 
mkuu upo serious kwamba dereva bajaji apelekane na polisi mahakamani. hujui huo ni upotevu wa muda na hiyo bajaji si yake na inahitaji marejesho. mahakamani which? hujui huko unaweza endesha kesi hata miaka miwili. ipo siku utaambiwa hakimu kaenda likizo ya uzazi hadi arudi
kutoa tu ushahidi mahakamani ni kero ,kila ukienda kesi imeahirishwa
Jifunze kudai haki kwa vitendo,hizi kwaya za kila siku hazisaidii.

Niliishawaambia kama unaona elfu 2 unazompa ni nyingi au zinakuumiza,lipia fine kwa kosa ulilofanya uisaidie serikali.

Kila ukikamatwa na polisi ukasomewa kosa una namna tatu za kuchukua hatua,kulipa fine tajwa,kukataa kosa kesi iende mahakamani au kumalizana na askari.hizo option mbili juu ukiruka ukachukua ya 3 usilalamike ni unafiki.
 
Back
Top Bottom