Mkuu,njaa,kiu,usongo ama urafi wa polisi ni kitu halisi sio ndoto.Kaka kama hujawahi drive kwa safari za kila siku au ndefu , hawa jamaa japo si wote wana njaa isiyo elezeka. Arusha walikuwepo wa mianzini, wale huwa wanafanya kama ni biashara kabisa, tena wana confidence kabisa as if ni halali
Probably sijui mazingira yake yakoje, ila mimi limenikuta arusha, moshi, tanga, singida, even pwani. Mara ya kwanza nililalamika baadae nikaambiwa usipowatoa watakubana mahali. By then nilikuwa natembelea chuma kipya. Asipokuluta na kosa, atakwambia hela ya chai. Imezoeleka japokuwa ni kinyume na sheriaMkuu,njaa,kiu,usongo ama urafi wa polisi ni kitu halisi sio ndoto.
Mtu kusema alikamatwa akiwa hana kosa,huu ni unafiki wa wazi,huna kosa unatoa rushwa ili wasikuue ama??
Ukitaka kujua akili za wabongo ni za hovyo kuliko traffic,mtu analalamika kwanini polisi anajificha kichakani kupiga tochi!!!!huu ni utoto kiwango cha juu.
Yaani nia yake akimbie mwendo anaoutaka popote tu.
Mtu akifikiria danadana atazopigwa polisi na makosa atayobambikiwa akigoma kutowa hiyo elfu tano, anaona ni heri atowe huku anasononeka.Mkuu huna kosa unatoa pesa ya nini???
Si ukubali kwenda kituoni kisha mahakamani ukatetee haki yako??,kama unahisi huna muda basi malalamiko yako yote yanakosa maana hapa maana unatoa kwa hiyari yako.
Polisi wanatumia uzembe na mapuuza yenu kujinufaisha.
Hakuna jambo jipya hapa ambalo umeongea!Inasikitisha sana siku hizi polisi kama nchi ni ya kwao kabisa.! As if Serikali imeshawapa ruhusa ya wanachokifanya. Mikoa mingine sijui, hapa Mtwara Kilimanjaro kuna hawa polisi wanatoza tu hela kwa wenye magari hata kama huna kosa sijui tuwaite watoza ushuru au polisi maana mauza uza uza tu.
Kuna hawa wa Mitengo yaani wanataka hela kwa lazima sh 5,000 kila bajaji kweli!
Sasa bajaj kutoka Mkanaled mpaka Mikindani bajaj inaingia abiria wanne ambao ni elfu 4 halafu utoe elfu tano bila kosa lolote huu ni uonevu wa hali ya juu na huku ni kujinufaisha wao tu.
Kuna hawa wengine hapa Mangamba njiani kama unaenda ziwani, hawa askari hapa imekuwa kama upatu kila gari la mchanga wanachukua elfu 5 na hii ni kila siku. Hata kama huna kosa lolote na wanakuambia kabisa tukuandikie kosa elfu 30 au utoe elfu 5.
Tumerudi zama za kikoloni mno
Tunaomba msaada Mtwara askari wanatajirika kupitia madereva
Askari wa Mangamba, Mitengo, na Kilimanjaro wanatunyonya mno
Siku yake nitakuja na picha na videos za hawa askari wetu.
Hilo haliwezekani kwasababu wao pia wamepewa target na mabosi wao! Na mabosi wao pia wamepewa target na mabosi wao,ni chain inaenda hivyo hivyo mpaka juu kabisa! Sijui umenielewa?Njia ya kuondoa Huu ni polisi avae camera muda wote ili chochote anachofanya kionekane Kwa umma na kuwashughulikia kirahisi.tuwaige wa marekani na wanywarwanda
kila mwananchi akiwa na mtizamo huu,basi hakuna maana ya maisha.Mtu akifikiria danadana atazopigwa polisi na makosa atayobambikiwa akigoma kutowa hiyo elfu tano, anaona ni heri atowe huku anasononeka.
Pipa na mfunikoPCCB na polisi ni mtu na dadake, ni wale wale.
Kwanza hakuna askari polisi tajiri, labda wanawanyonya nini.... madushe?Inasikitisha sana siku hizi polisi kama nchi ni ya kwao kabisa.!
Tunaomba msaada Mtwara askari wanatajirika kupitia madereva
Askari wa Mangamba, Mitengo, na Kilimanjaro wanatunyonya mno
Siku yake nitakuja na picha na videos za hawa askari wetu.