carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
MWANZA: Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewakamata watu 98 kwa tuhuma za kujihusisha na makosa mbalimbali ya jinai, yakiwemo hujuma dhidi ya miundombinu ya umeme, uvunjaji wa nyumba, wizi, biashara haramu ya pombe ya moshi na dawa za kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama mkoani humo leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika operesheni mbalimbali zilizoanza Oktoba Mosi, 2026, kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama.
Amesema operesheni hizo zimefanyika sambamba na doria, ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia na ushirikishwaji wa wananchi katika kubaini na kuzuia uhalifu. Kwa mujibu wa Mutafungwa, Jeshi la Polisi limewafikia wananchi takribani 120,000 kupitia mikutano na utoaji wa elimu kuhusu namna ya kushirikiana na vyombo vya dola katika kuzuia na kutanzua uhalifu.
Katika operesheni hizo, Mutafungwa amesema polisi wamekamata vifaa mbalimbali vinavyodaiwa kuhusishwa na hujuma dhidi ya miundombinu ya umeme na mawasiliano, vikiwemo Polymeric vinne, High Nuts 36, Tension Clamp 24, Distance Nail nane, Mid Span Joint 30, Fish 100 na vipande vya nyaya za umeme vyenye urefu wa mita 150.
Chanzo : Habari Leo