Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,933
JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa limetoa ufafanuzi kufuatia kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa watuhumiwa wanne, akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA) Mkoa wa Iringa, Ibrahimu Myovella (33), wamepotea wakiwa mikononi mwa polisi.
Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amewataja watu wanaodaiwa kupotea kuwa ni Ibrahimu Myovella (33), Asajile Anthony (33), Anthony Mwasika (29) pamoja na Ally Kalolo (26).
Jeshi la Polisi limesema kuwa taarifa hizo si za kweli kwani watuhumiwa walikimbia polisi kwakuwa wanakabiliwa na tuhuma za mauaji na kwamba litaendelea kutoa taarifa rasmi ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka miongoni mwa wananchi.
Awali, kupitia taarifa yake kwa umma, Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA (BAVICHA) walieleza kusikitishwa na kile walichodai kuwa viongozi wao walishikiliwa kwa siku nane bila kupewa dhamana au kufikishwa mahakamani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Februari 18, 2026 walitakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Iringa Mjini na tangu waliporipoti hawakuonekana tena, hali iliyozua hofu kwa wanachama na familia zao.
BAVICHA ililitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua ya kuwaachia huru au kuwafikisha katika mamlaka za kisheria kwa mujibu wa sheria.