Siwapendi polisi jaman, niliendaga siku moja kituo kimoja kikubwa kuulizia huduma ya sticker ya nenda kwa usalama, nimefika nimesalimia hata hajaitikia anasema sema shida yako, nilichukia yaani kwanza mshahara hanizidi, nimemuacha mbali kielimu hanifikii yaani nilimdharau nikasema hizi ndude sijui zinajionaje kwa mfano,. Nakumbuka niliendaga Jwtz pale Mgulani enzi za duka la jeshi yaani niliulizwa kitu na nikajibiwa vzr, the same to magereza kwa kweli.
Baba yangu alikuwa polisi na hakuwa na tabia mbaya kama za makauli ya ajabu, alikuwa mtu wa watu na msaada kwa wale walioonea, siku moja mtu mmoja alipelekwa kituoni na akawekewa bangi mfukoni nakumbuka baba yangu aliwafokea sana wale watu na akataka kuwaweka rock up na yule mtu akaachiwa, yaani ile picha hadi leo hainitoki nilikuwepo pale sikuelewa kitu ila usiku nyumbani Baba alikuwa akielezea na kusikitika kwa uchungu namna yule mtu alivyotaka kuonewa. Kuna mahali Polisi huwa mnajisahau hamjui pia mtatukuta huku kwenye taasisi zingine sema mm sina roho mbaya so ningekuwa nalipiza lakini nimekula kiapo kwa kweli.
Polisi, nyinyi mjirekebishe kauli zenu kwa wateja wanaoleta malalamiko, lakini muangalie haki za watu sio mnawakandamiza kwa sababu hawana hela, Mungu atawalipa kwa kweli.
Ushauri wangu, mngekuwa nyie wenyewe mngeongeza speed hadi mia moja so msifanyiane hivyo maana hata course nahisi huwa mnakutana, nimechukizwa sana na hii kitu.