Polisi na mahabusu wapoteza maisha ajalini Mwanza

Polisi na mahabusu wapoteza maisha ajalini Mwanza

Magari yanayotoka magereza huwa Yana Kasi
Asa mtuhumiwa Yuko chini ya ulinzi mwendo Kasi was Nini na gari bovu
 
Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na mahabusu wawili - waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya kigaidi pamoja na mauaji, wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 katika Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Sengerema.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la polisi aina ya Toyota Landcruise yenye namba za usajili PT 3798 lililokuwa likitokea mkoani Mwanza, kukata ‘sterling rod’ na kuhama kutoka upande wake na kwenda upande mwingine na kugongana na Lori aina ya Scania lenye tela namba. T.865 mali ya kampuni ya Nyanza Botling.

Ajali hiyo pia imejeruhi watu wanne na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita huku miili ya askari hao wawili ikihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

View attachment 2203582
Wanajua kula rushwa ila kutengeneza magari huo mda hawana,wao ni kukimbiza tu
 
hili issue ya 'ku-overspeed + reckless driving' kwa madereva wa magari ya serikali limekuwa ni kaburi kwa wasio kuwa na hatia na kibaya Zaidi hakuna kiongozi yoyote anaye likemea, ona sasa yaani askari mzima ana overtake kwenye 'blind corner' sehem ambayo hajui mbele yake kuna anaenda kukutana na nini na siku ya mwisho jeshi la polisi wanamkamata na kumfungulia mashitaka aliye gongwa, pole kwa mahabusu/ watuhumiwa walio fariki ….
Gari limekata Steering rod haina ujanja hio.
 
Yaani sterling rod ndio libondeke gari lote hivyo? Wacheni kuteteana kuweni fair mupate kubarikuwa
Ila poleni kwa wote kabisa
 
hili issue ya 'ku-overspeed + reckless driving' kwa madereva wa magari ya serikali limekuwa ni kaburi kwa wasio kuwa na hatia na kibaya Zaidi hakuna kiongozi yoyote anaye likemea, ona sasa yaani askari mzima ana overtake kwenye 'blind corner' sehem ambayo hajui mbele yake kuna anaenda kukutana na nini na siku ya mwisho jeshi la polisi wanamkamata na kumfungulia mashitaka aliye gongwa, pole kwa mahabusu/ watuhumiwa walio fariki ….
Wao wanakuwaga na visingizio ila raia akipata ajali sababu ni moja tu, uzembe wa dereva.
 
Gari haina kitu kinaitwa STERLING ROD

Kamanda shule yake ni suspect, hatupaswi kuweka usalama wetu na maisha yetu kwenye vichwa vya watu kama huyu RPC

Gari ilikuwa na spidi ya mwanga na dereva alikuwa tingas, si ajabu
 
Gari limekata Steering rod haina ujanja hio.
ina maana hiyo sterling rod ya hilo gari ilikatika wakati dereva ana overtake kwenye 'blind corner' ikiwa kwenye speed ya ya kifo??, kingine ni huyo mkuu wa mkoa injia nani, yaaani kila mkoa anauongoza lazima pepo za maajali kwa watumishi wa idara za serikalini ziwaandame, kuna nini apo? tena huyo mkuu wa mkoa mwenyewe ni 'mlokoke', hawakemei au na yeye ana kagunduu ka ajali, au anawatoa nani??
 
ina maana hiyo sterling rod ya hilo gari ilikatika wakati dereva ana overtake kwenye 'blind corner'
Lakini kwenye hiyo report sijaona neno "overtake" soma vizuri bro.
 
ina maana hiyo sterling rod ya hilo gari ilikatika wakati dereva ana overtake kwenye 'blind corner' ikiwa kwenye speed ya ya kifo??, kingine ni huyo mkuu wa mkoa injia nani, yaaani kila mkoa anauongoza lazima pepo za maajali kwa watumishi wa idara za serikalini ziwaandame, kuna nini apo? tena huyo mkuu wa mkoa mwenyewe ni 'mlokoke', hawakemei au na yeye ana kagunduu ka ajali, au anawatoa nani??
MTU Yuko mwendokasi halafu unasema wanatolewa kafara

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Wakati naanza maisha 1991 nilipata ajira noremco moshi, same arusha namanga project sssa dogo mmoja msambaa much noo alikabidhiwa volvo tan 18 mpya, katika kazi kizembe zembe aliangusha lile tipa kizembe akakimbilia kukata sterling rod wazungu wakamwambia mshamba mkubwa utaoezea jela

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
[emoji1]

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Taarifa toka kwa wadau Gari lilikuwa linatokea Geita kwenda Mwanza sio Mwanza to Geita, jamaa walikuwa speed sana na walitaka kusababisha ajali mapema baada kuanza safari yao maeneo ya Shilabela walipiga bump na kutaka kupoteza muelekeo muda mchache baadae watu wanasikia ajali ya gari hilo hilo maeneo ya Ibanda.
 
Gari haina kitu kinaitwa STERLING ROD

Kamanda shule yake ni suspect, hatupaswi kuweka usalama wetu na maisha yetu kwenye vichwa vya watu kama huyu RPC

Gari ilikuwa na spidi ya mwanga na dereva alikuwa tingas, si ajabu
Dereva alikua kijana Faraj sikumbuki kumuona akiwa kalewa RIP Afande Faraj

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Kuna hizi gari za polisi na ambulance ni hatari sana kwa speed kali utafikiri wanaoendesha ni malaika hawakosei.
 
Back
Top Bottom