Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Kama kuna watu wanaotakiwa kusoma alama za nyakati vizuri basi watu hao ni polisi wetu.
Kwa muda mrefu wamejiweka juu ya sheria kwamba wanaweza kuvamia popote na kumkamata mtu yeyote bila kufuata sheria. Hawatoi vitambulisho, hawawatumii viongozi wa eneo husika, wanatumia, maguvu bila sababu, ukitaka maelezo kwanini unakamatwa wanakwambia utajibu kituoni au wanakugeuzia kibao kuwa ulikuwa unawazuia kufanya kazi yao.
Matukio ya watu kukamatwa kwa mtindo huu na kisha kutoweka na kutoonekana tena na wengine kukutwa wameuuawa baada kukamatwa na polisi yamebadilisha taswira nzima waliyokuwa nayo wananchi juu ya polisi na sasa wameanza kuungana taratibu kupingana na polisi kuhusiana na staili yao ya ukamataji na hivyo wananchi wameamua kujilinda wenyewe sasa baada ya kuona polisi hawaaminiki tena.
Sasa hivi ni moshi tu unafuka wa moto walioukoka polisi wenyewe wa kutumia maguvu hata pasipostaili kutumia maguvu au mabavu. Kama polisi hawajagundua kuwa nao ni binadamu ambao wanaweza nao kumwaga damu zao kama raia wakawaida wajue uvumilivu wa raia imeshaanza kufikia mwisho kitakachofuata ni kuwa watakwenda na maguvu yao kukamata kwa nguvu pasipohitajika nguvu halafu wananchi nao wakaamua liwalo na liwe watajiluta nao hawatarudi nyumbani.
Matukio ya Mwanza na Dar es Salaam yawe ni funzo kwao kwamba kidogo kidogo wameanza kuwafumbua na kuwaunganisha raia dhidi ya polisi.
Polisi ni chombo cha serikali cha ulinzi wa raia na mali zao. Lakini kwa matendo yao wananchi wameanza kuona kuwa hawapo salama kabisa wawapo mikononi mwa polisi.
Juzi wakiadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa jeshi lao wamefanya onesho lao ka jinsi wanavyokabiliana na raia wasiokuwa na silaha yoyote yaani waandamanaji kwa amani. Hapa mtu angetegemea wafanye onesho linaloonesha jinsi wanavyokabiliana na wahalifu na namna wanavyotoa ulinzi na usalama kwa raia. Wenye akili tumejua onesho hilo lililenga kuwatishia wananchi wanaokusudia kuandamana Jumatatu 23/09/2924 Kwa kufanya hivyo hawajui kuwa wamejenga taswira mbaya kuwa polisi kazi yao ni kuzuia na kukandamiza haki halali za kikatiba za wanachi. Yaani kwa ufupi wao wameonesha kuwa kazi yao ni kuwasaidia watawala kusigina haki za raia zilizomo katiba ya nchi.
Ni muhimu polisi wetu wabadilike sasa na kuwa chombo cha jamii badala ya kuwa adui wa jamii. Katika usitaarabu wa sasa kuna raia wanaoweza kuitwa kituoni na wakaenda wenyewe bila kufuatwa lakini polisi watafunga safari na magari na mitutu ya bunduki utadhani wanakwenda kupambana na majambazi. Nadhani kwenye mafunzo yao wafundishwe pia elimu ya mawasiliano kwa umma na mbinu za mawasiliano yaani communication skills.
Polisi wetu hawana uwezo wa kujieleza na kuelezea mambo ndiyo maana wakifika hawatoi maelezo yoyote na ukiwauliza ndio unawatia hasira wanakubeba kama gunia la mkataa. Yaani polisi ukitaka maelezo ndio unawapandisha hasira mara utasikia usitufundishe kazi au unajifanya mjuaji. Kitakachofuata ni virungu na kubebwa mzobe mzobe.
Wakishakuweka kwenye gari wanakugeuza mzigo wanasimama juu yako yaani wewe ndiye unageuka kuwa sakafu ya gari yao. Kusema kweli hawana ubinadamu kabisa. Wabadilike sasa. Mwenye masikio na asikie.