mkulimamiwa
JF-Expert Member
- Mar 4, 2025
- 2,591
- 5,315
Wakati polisi wakiwa mabarabarani kwa hasira kusubiri waandamanaji wa kuzuia uchaguzi ili kuwafyatulia maji ya washawasha na lisasi za moto, naamini haitakuwa hivyo!
Watu watakwenda kwenye vituo vya kupigia kura kwa amani na salama kabisa na bila kujulikana ni kina nani watahusika katika kukwamisha uchaguzi huo
Katikati ya upigwaji kura, Wazuwia uchaguzi wakiweza kuanzisha sekeseke hapo itakuwaje? Kitatokea nini kama siyo jeshi la police kuhamaki, nawaza tu!
Mimi nafahamu, ikitokea hilo, mtu wa kwanza kuzuia huo uchaguzi ni polisi, bila hekima ya kutosha, watapiga mabomu tu, na watu wote kwenye vituo vya kupiga kura hawatabaki, lazima watasambaratika kwa kukimbia, na ndio itakuwa mwisho wa kupiga kura siku hiyo
Je, huo utakuwa ni uchaguzi kweli?
Nani atakwenda majumbani kwa watu kuwarudisha raia waje kuendelea kupiga kura?
Naomba, kwa hekima za viongozi wetu wa nchi, wakubaliane tu wayazungumze yaishe
Maana itakuwa rahisi mno kuzuilika kwa uchaguzi