Polisi ni janga la kitaifa

Polisi ni janga la kitaifa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ukweli askari polisi ni kero kubwa kwa wananchi. Ni kero kubwa kwa wakulima, wafugaji, wasafirishaji, wafanyabiashara na hata madereva barabarani. Kila jambo na kila kitendo wanachokifanya ni kwaajili ya kupata hela kwa njia ya rushwa au unyang'anyi kunakosababisha Wananchi wanakata tamaa ndani ya nchi yao wenyewe. Hizi mashine za kutozea watu faini wanazotembea nazo ndio silaha kubwa wanayoitumia kusumbua watu kuwabambikiza makosa watu kwa lengo la kuwafanya watu wavutike kulipa hela punguvu kuliko sh. 30,000 zinazotozwa kwakutumia vifaa hivyo vya mkononi, ni kero.

Naomba kwa kuanzia polisi wanyang'anywe hizi mashine za mkononi ambazo wanazitumia vibaya. Wanaigombanisha serikali na wananchi wake. Barabarani hawaachi pesa, wanapokea kuanzia sh. 2000 ili kusamehe tsh 30,000 za kubambikia au kosa la kweli.

Kwa wakulima na wafugaji, polisi wanashirikiliana na wakulima/wafugaji kujipatia fedha kwa makosa ya kubambikia. Huku vijijini kero ni kubwa sana kiasi cha watu kukata tamaa kwa vitendo vya polisi kwa "michongo" ya polisi kwa ushirikiano na baadhi ya wanavijiji.

Wasafirishaji wa mizigo na abiria wako hoi, vijana wanaosafirisha mizigo kwa kutumia pikipiki za magurudumu 3 wana shida sana barabarani, wanawindwa kama swala na jeshi la polisi.

Ukweli jeshi hili livunjwe ili lipangwe upya.
 
Ni nadra sana kubambikia kosa barabarani. Madereva wengi wanafanya makosa na ushahidi unakuwepo.

Kama kweli umefanya kosa nakusihi kuwa mzalendo lipa hiyo 30k.

Kama hauna kosa acha aandike lakini unao uwezo wa kwenda kuipinga hiyo faini.
hiyo sio kweli, polisi wanakusimamisha saa 1 asubuhi wakati wasafirishaji, wasafiri na madereva binafsi wanawahi kazini, wanasimamisha magari 10 halafu anapitia gari mojamoja kuhoji hili na lile asuhi ile. Lakini ukimpa 2000 kosa linayeyuka. Je, sh. 5000 inayeyusha makosa ya dereva au gari? Yaani dhamira haikuwa kupunguza ajali bali kujipatia fedha binafsi. Kule kijijini mfugaji au mkulima anawekwa mahabuhusu makusudi kwa tuhuma ambayo wana uhakika kuwa ni mchongo.
 
Kuna mmoja kidogo nimlambe makofi
Kaka mimi ninawatazama usoni hadi nijisikia aibu kwa taifa. Unaona kabisa kijana hakupaswa kuwa askari polisi, unaona kabisa huyu mtumishi hana usimamizi madhututi, hana hofu ya kile anachokifanya.
 
Kaka mimi ninawatazama usoni hadi nijisikia aibu kwa taifa. Unaona kabisa kijana hakupaswa kuwa askari polisi, unaona kabisa huyu mtumishi hana usimamizi madhututi, hana hofu ya kile anachokifanya.
Management ya jeshi la polisi haina çross chack machanism kwa utendaji wao. Hivyo ni kupiga deal tu
 
Ukweli askari polisi ni kero kubwa kwa wananchi. Ni kero kubwa kwa wakulima, wafugaji, wasafirishaji, wafanyabiashara na hata madereva barabarani. Kila jambo na kila kitendo wanachokifanya ni kwaajili ya kupata hela kwa njia ya rushwa au unyang'anyi kunakosababisha Wananchi wanakata tamaa ndani ya nchi yao wenyewe. Hizi mashine za kutozea watu faini wanazotembea nazo ndio silaha kubwa wanayoitumia kusumbua watu kuwabambikiza makosa watu kwa lengo la kuwafanya watu wavutike kulipa hela punguvu kuliko sh. 30,000 zinazotozwa kwakutumia vifaa hivyo vya mkononi, ni kero.

Naomba kwa kuanzia polisi wanyang'anywe hizi mashine za mkononi ambazo wanazitumia vibaya. Wanaigombanisha serikali na wananchi wake. Barabarani hawaachi pesa, wanapokea kuanzia sh. 2000 ili kusamehe tsh 30,000 za kubambikia au kosa la kweli.

Kwa wakulima na wafugaji, polisi wanashirikiliana na wakulima/wafugaji kujipatia fedha kwa makosa ya kubambikia. Huku vijijini kero ni kubwa sana kiasi cha watu kukata tamaa kwa vitendo vya polisi kwa "michongo" ya polisi kwa ushirikiano na baadhi ya wanavijiji.

Wasafirishaji wa mizigo na abiria wako hoi, vijana wanaosafirisha mizigo kwa kutumia pikipiki za magurudumu 3 wana shida sana barabarani, wanawindwa kama swala na jeshi la polisi.

Ukweli jeshi hili livunjwe ili lipangwe upya.
Kwanini utoe rushwa , hata kama sh 2,000 ambayo anakula traffic mmoja ,ni bora uandikiwe tu sh 30,000 pesa iingie Serikalini,pia hata hiyo sh 30,000 utakayolipa zinakusanywa yakifika mabilion wanaenda kula mafisadi wakina Chemba na wenzake ,kwa hiyo akili kumukichwa
 
Ukitaka kujua umuhimu wa hawa viumbe siku moja wafanye mgomo wa siku tatu nchi nzima
 
NAKAZIA! Bongo ukitaka kufanya biashara Kwa Amani hikikisha unatambea na ela ndogo ndogo 5K,2K , Polisi wengi wemegeuka kuwa walanguzi .
 
Kwanini utoe rushwa , hata kama sh 2,000 ambayo anakula traffic mmoja ,ni bora uandikiwe tu sh 30,000 pesa iingie Serikalini,pia hata hiyo sh 30,000 utakayolipa zinakusanywa yakifika mabilion wanaenda kula mafisadi wakina Chemba na wenzake ,kwa hiyo akili kumukichwa
Na huo ndio msimamo wangu mimi kavulata, niko tayari kulipishwa 30,000 kuliko kutoa 2000. Kinachokera mimi sana ni polisi kuomba leseni yangu akague, lakini baada ya kumpa leseni yangu anaiweka mfukoni kwake na kwenda kuhangaika na magari mengine 10 kwanza aliyoyasimamisha kisha ndio aje kwangu kunipa feedback, na ukimuuliza kwanini umenisimamisha anakwambia umepita kwenye taa nyekundu, unamuuliza barabara nzima imetifuliwa inajengwa barabara ya mwendo kasi, hakuna alama hata moja za barabarani hata moja, magari yote yanapita njia moja kwa usaidizi wa waongozaji njia na matofali yaliyowekwa barabarani na wewe polisi upo kwanini magari mengine umeyaruhusu kupita na mimi nisipite bila kusimamishwa kwenye mazingira hayohayo ya taa waliyopita wenzangu?

Anachokifanya polisi kwenye njia hizi zilizotifuliwa ambazo zimebakishwa angalaau taa chache za barabarani ni kuruhusu magari ya mbele yapite kwenye taa nyekundu halafu yeye anakaa pembeni bila kutoa ishara yoyote kusubiri magari ya nyuma yatakayoyafuata magari ya mbele aliyoyaruhusu kupita kwenye taa nyekundu ili ayasimamishe na kuyabambikia makosa ya kupita kwenye taa nyekundu. Anakuchelewesha na kukuzunguusha ili utoe chochote. Na wakati mwingine ukikomaa sana kuacha kumpa rushwa wakati hana kifaa cha kuandika na kutoa risiti ya adhabu basi atakwambia nitakuandikia control namba yako kamuulize traffic yeyote huko mbele ya safari akwambie. Yaani wakati mwingine unaandikiwa kosa bila kupewa namna ya kulipa kwakuwa hakukupa risiti ya kulipia. Ni usumbufu kwa wananchi wa mama samia.

Jeshi hili ni kero hakiyanani.
 
Ukitaka kujua umuhimu wa hawa viumbe siku moja wafanye mgomo wa siku tatu nchi nzima
Aaa huo ni upuuzi tu, Wao ni watumishi sawa na watumishi wengine nchini, hata daladala, walimu, watu wa afya, wenye maduka, wenye mabucha, wakulima, wafugaji, wazibua mitaro, na wanajeshi nao wakigoma pia hakutakalika. Hakuna watumishi muhimu kuliko wengine.
 
Ni nadra sana kubambikia kosa barabarani. Madereva wengi wanafanya makosa na ushahidi unakuwepo.

Kama kweli umefanya kosa nakusihi kuwa mzalendo lipa hiyo 30k.

Kama hauna kosa acha aandike lakini unao uwezo wa kwenda kuipinga hiyo faini.
Ndio maana wamekuja na hoja ya watu wapeleke vyeti ili kuwatambua madereva ingawaje mbinu yao ni mbovu ila wewe sio Dereva bhana...
 
Ndio maana wamekuja na hoja ya watu wapeleke vyeti ili kuwatambua madereva ingawaje mbinu yao ni mbovu ila wewe sio Dereva bhana...
Wangeanzia kuwafukuza na kuwafunga jela polisi wote waliowapa watu leseni kama njugu bila vigezo, kwani hawawajui? hawakuwaona? wanalinda nini kama hawakuwaona?. Kudai vyeti sasa ni kuwapuuza, kuwadharau na kuwahangaisha wananchi kwa uzembe wao.
 
Police wanalalamikiwa kwa sababu wanadili na watu masikini, zile taasisi zinazodili na matajiri huwezi sikia kelele za rushwa japo rushwa ni pale pale.
 
Wangeanzia kuwafukuza na kuwafunga jela polisi wote waliowapa watu leseni kama njugu bila vigezo, kwani hawawajui? hawakuwaona? wanalinda nini kama hawakuwaona?. Kudai vyeti sasa ni kuwapuuza, kuwadharau na kuwahangaisha wananchi kwa uzembe wao.
Mimi sipeleki cheti nisome harafu nianze kupeleka cheti kwao tena kwa makosa yao ntapeleka cheti wakati wa kuongeza muda leseni yangu...yaani wao wale rushwa wanisumbue bila sababu za msingi haitowezekana na wakiweka faini huko Road nadhani tutafika mahakamani mwaka huu...
 
Ila polisi wanapenda sana rushwa. Kama wale wa usalama barabarani ndiyo kabisaaa! Nadhani wasiojihusisha na hivyo vitendo watakuwa wanahesabika kwenye hilo jeshi.
 
Wengi huwa mnalaumu tu polisi lakini shida sio polisi, tatizo ni sheria zetu zimekaa kikoloni sana, sheria ni kali kiasi kwamba polisi wakisizimamia inaonekana wakuda ila akizipotezea kwa kupewa 2000 ndio tunalalamika. Sheria zipunguzwe makali uone kama kuna askari atapewa rushwa.
 
Back
Top Bottom