LGE2024 Polisi Rukwa: Vijana CCM hawakuwa na nia ya kuchoma nyumba ya Mbunge

LGE2024 Polisi Rukwa: Vijana CCM hawakuwa na nia ya kuchoma nyumba ya Mbunge

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
A
Wakuu,

Maake hapo kwanza ncheke!

===


Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limetoa ufafanuzi wa taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu vijana sita wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kukamatwa nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida Kenan wakiwa na petroli lita 20 kwa lengo la kuiangamiza familia ya mbunge huyo.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, imesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa vijana hao waliokamatwa na wafuasi wa CHADEMA, walifika nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali majira ya saa moja jioni wakiwa na pikipiki mbili na dumu lenye mafuta ya petroli lita 20, kwa lengo la kuchukua pikipiki zingine zilizokuwa hapo na kuziwekea mafuta.

“Kwa kuwa nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya na nyumbani kwa Mbunge ni karibu sana nyumba zao zikitenganishwa na barabara, ndipo vijana hao walipokamatwa na kutuhumiwa kwamba walikuwa na lengo la kuchoma moto nyumba ya Mbunge Aida,” imeeleza taarifa ya Polisi.

Swahili Times

Pia soma:
- LGE2024 - Nkasi: Wanaodaiwa kutumwa na DC kulipua nyumba ya Mbunge Aida Kenani usiku huu wakamatwa, wametumia pikipiki za Samia
Afande! Kumbe nyumba ya DC Nkasi ni karakana ya pikipiki za CCM kiasi zinakusanywa pale na kuletewa petroli kwenye madumu na vijana wa CCM? Mbona weledi unazidi kutokomea katika Jeshi letu la Polisi kwa kadri nchi inavyopaswa kuendelea? Viongozi msitupeleke gizani!

Na kiongozi au mtendaji unayefumbia macho vitendo kama hivi kwa kupindisha ukweli yafaa ujitafakari hata kama unafanyabhivyo kulinda kutumbua kwani siyo lazima uishi kwa nafasi hiyo ajira binafsi jama kilimo zipo tu!
 
Back
Top Bottom