Polisi: Sheikh Zuberi Hakutekwa Alikimbia Madeni, Akamatwa Kufikishwa Mahakamani

Hivi hawa jamaa wanatuona sisi mabwege sana? Unaweza kukuta hata huyo sheikh wao ndio walimpanga ionekane katekwa ili watengeneze hii drama. Sheikh adaiwe 500+m kwa biashara gani anayofanya?
Hivi chadema uwa mnawachukuliaje viongozi wa kiislam?
 
Kwa hiyo wewe unaamini hiyo taarifa ?
Tutajie mali alizonazo ili kufikia kudaiwa 500m...
Jifunze kufikiri nje ya box...

Hiyo ni staged case...sikufundishi fikiria zaidi
Hapo Singida wana chuo au shule nadhani ya Islamic Foundation, na kuna kipindi waliwahi kuchekechwa kwa kuhusishwa na ugaidi
 
Hivi hawa jamaa wanatuona sisi mabwege sana? Unaweza kukuta hata huyo sheikh wao ndio walimpanga ionekane katekwa ili watengeneze hii drama. Sheikh adaiwe 500+m kwa biashara gani anayofanya?
Wewe bwege, fuatilia hiyo stori, hapo Singida wana educational institution
 
Jeshi la Polisi limesema linamshikilia Sheikh Zuberi Said Nkokoo (53) mwalimu wa dini na kiongozi katika taasisi ya Islam Foundation mkoani Singida baada ya kutengeneza tukio la uongo la kutekwa ili kukimbia madeni aliyokuwa akidaiwa.

Taarifa ya polisi imesema Sheikh huyo anadaiwa shilingi milioni 521, na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika.
Source Swahilitimes
Sasa ni wazi polisi na serikali wanatuona Watanzania ni mabwege, mazezeta tusio na hata akili kidogo...

Kama ni hivyo, basi tunawataka na hawa ndugu zetu (kama walikimbia madeni kweli), basi Polisi ifanye hivyo hivyo iwakamate iwapeleke Polisi au mahakamani ili sisi ndugu zao tuje tuwakomboe tuwalipie madeni yao...!!!

1. Mdude Nyagali
2. Deusdedit Soka na mwenzake
3. Ben Saanane
4. Mzee Ally Kibao
5. Boniface Chaula + wengine makumi...

Honestly, impunity na ujinga wa viongozi wetu hawa na serikali kwa ujumla umefikia kwenye kiwango cha saturation point. Serikali hii inakwenda naturally ku - collapse...!

Huu upuuzi na ujinga wa kutuona watu wote ni wajinga na wapumbavu kama wao, HAUKUBALIKI...!!!
 
Jeshi la Polisi limesema linamshikilia Sheikh Zuberi Said Nkokoo (53) mwalimu wa dini na kiongozi katika taasisi ya Islam Foundation mkoani Singida baada ya kutengeneza tukio la uongo la kutekwa ili kukimbia madeni aliyokuwa akidaiwa.

Taarifa ya polisi imesema Sheikh huyo anadaiwa shilingi milioni 521, na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika.
Source Swahilitimes
Na uchunguzi wa Mzee Kibao bado tu!!
 
Hayo madeni alikopa kwa nani?

Nani alifungua kesi ya kumdai huyo shekhe?

Ripoti ya mchongo na wahusika katika kesi hiyo wamehongwa pesa za wananchi kutaka kujisafisha lakini damu haisafishiki kwa ulaghai.

This is a typical staged hypothesis
Naunga mkono hoja....
Hao wadai wasijitokeze siku zote hizo kumfikisha mahakamani ,eti wasubiri atoweke ndipo wadai waende polisi kudai wana deni naye.....
Ushahidi wa watu kutekwa na kuuawa uko wazi...
 
Jeshi la Polisi limesema linamshikilia Sheikh Zuberi Said Nkokoo (53) mwalimu wa dini na kiongozi katika taasisi ya Islam Foundation mkoani Singida baada ya kutengeneza tukio la uongo la kutekwa ili kukimbia madeni aliyokuwa akidaiwa.

Taarifa ya polisi imesema Sheikh huyo anadaiwa shilingi milioni 521, na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika.
Source Swahilitimes
Inawezekana mlimteka , mkatengeneza story hii
 
Jeshi la Polisi limesema linamshikilia Sheikh Zuberi Said Nkokoo (53) mwalimu wa dini na kiongozi katika taasisi ya Islam Foundation mkoani Singida baada ya kutengeneza tukio la uongo la kutekwa ili kukimbia madeni aliyokuwa akidaiwa.

Taarifa ya polisi imesema Sheikh huyo anadaiwa shilingi milioni 521, na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika.
Source Swahilitimes
Siwaaamini police kabisa
 
Back
Top Bottom