GE2025 Polisi Singida wahamasisha maafisa usafirishaji kulinda amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu

GE2025 Polisi Singida wahamasisha maafisa usafirishaji kulinda amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Maafisa wa usafirishaji wa Stendi ya Zamani, Singida wametakiwa kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika kulinda amani na utulivu, hususan kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa kuwa amani ni msingi wa maendeleo na si jukumu la vyombo vya dola pekee, bali la kila mwananchi

Wito huo umetolewa Oktoba 20, 2025 na Afisa Polisi Jamii Wilaya ya Singida, ASP Athuman Muna akishirikiana na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kata ya Majengo, Balum Saguda, walipokutana na maafisa usafirishaji katika stendi hiyo

Wamewataka kutumia nafasi yao kuwahamasisha abiria kuhusu umuhimu wa kudumisha amani, kwa kuwa bila utulivu hakuna biashara itakayoweza kufanyika kwa ufanisi

Aidha, wamewakumbusha kuepuka tabia na vitendo vinavyoweza kuchochea uvunjifu wa amani kama lugha za kejeli, maandamano haramu, au matumizi mabaya ya mitandao

Vilevile wamewasisitiza utoaji wa taarifa kwa vyombo vya usalama kuhusu vitendo au watu wanaohatarisha usalama wa jamii, na kuwaasa kutekeleza haki yao ya kupiga kura kwa utulivu, huku Jeshi la Polisi likiwa tayari kuhakikisha usalama

1761227087216.png

1761227243677.png


1761227299522.png
 
Mbona mmekazania hao wahuni wa bodaboda, halafu mnawaita maafisa, maafisa gani wanakaa vijiweni badala ya ofisini? Mnawaona ni tishio wanaweza kutekwa na upepo wa uvumi wa maandamano kiasi kwamba kila mara mmekazana kuwapa semina ya amani. Kwanza hawana elimu na hawafuatilii hali ya kisiasa inavyoenda. Hizo semina za amani pelekeni kwa wenye ufahamu wa mambo ya kisiasa na sio kwa makundi hayo yasiyoelewa kinachoendelea nchini. Mna hofu ya bure na kundi hilo, labda kwa kuwa mnawakuta wapo vijiweni na tabia zao huwa ni za kilevilevi mkajua kwamba ni rahisi kushiriki maandamano. Hao vijana wana njaa kali muda wa kuandamana hawana
 
Pelekeni hizo semina kwa vijiwe vya magazeti, kahawa na bao, huko yanaongelewa mambo mazito ya siasa za nchi. Au mnawaona ni wazee wapiga kura si rahisi kubebwa na upepo wa maandamano?
 
Wameona wapo wachache nini.
Hapa ni kama wasemavyo daima mbele kurudi nyuma mwiko.
 
Back
Top Bottom