Polisi Songwe: Hatujapokea malalamiko ya Green Guard kutishia Wapiga Kura kwa Mapanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga amezungumza na JamiiForums na kueleza kuwa hawajapokea malalamiko yoyote kutoka kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu Wanachama wao kutishiwa kwa mapanga katika Vituo vya Kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana Novemba 2024.

Kauli hiyo imetolewa baada ya awali, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa, Issakwisa Thobias Lupembe alisema “Kuna malalamiko mengi, Green Guard wanaenda kwenye vituo vya Kupiga Kura wakiwa na mapanga na visu wanatisha mawakala na Wanachama wetu na Wapiga Kura. Jeshi la Polisi lipo na sio mara ya kwanza kuwalalamikia kuhusu hali hiyo, ilianza wakati wa Uandikishaji na Uteuzi.”

Pia soma ~ CHADEMA Songwe: Green Guard walienda na mapanga kwenye Vituo vya Kupigia Kura kutisha Wanachama wetu
 
Kwani mliyopokea mmeyafanyia nini? Ben, azory, kibao, mdude, soka et al,
 
Back
Top Bottom