Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Saa chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji kesho Jumatano tarehe 27 Novemba, 2024 Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe mapema leo Novemba 26, 2024 limefanya doria za magari na miguu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Songwe ikiwemo mji wa Tunduma wilaya ya Momba, Isongole na Itumba wilaya ya Ileje pamoja na kata ya Vwawa na Mji Mdogo wa Mlowo wilaya ya Mbozi ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ulinzi na usalama.
Akizungumza baada ya doria hiyo, Mkuu wa Operesheni mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Nicholaus Livingstone amesema kuwa doria hiyo ni sehemu ya kuimarisha ulinzi katika maeneo ya mkoa wa Songwe na viunga vyake.
ACP Livingstone amesema kuwa doria katika vitongoji, vijiji, mitaa na kata mbalimbali ndani ya mkoa wa Songwe zinazofanywa na Jeshi hilo ni sehemu ya kujua changamoto za kiusalama zinazowakabili wananchi na kuchukua hatua za haraka za kuzitatua ili mkoa huo uendelee kuwa salama.
Vilevile ACP Livingstone amewataka wananchi wa mkoa huo kuendelea na shughuli zao za kujitafutia kipato bila wasiwasi wowote kwani Jeshi lao la Polisi mkoani humo lipo imara kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao unaendelea kuwepo wakati wote.
Ikumbukwe kuwa magari hayo ya doria na vitendea kazi vingine ni sehemu ya juhudi ya Serikali ambayo imekuwa ikitoa vifaa mbalimbali kwa awamu ili kuboresha utendaji kazi wa Polisi.