Polisi Tanzania 1-1 Yanga SC | Sheikh Amri Abeid Stadium | VPL

Kama shida ni yeye ni kweli its time heri aondoke tu.Nadhan inatakiwa sasa mtu awajibike.What the f***k are they doing timu ina players wazuri lakini inajikokota tu.
Players wazuri hamna huwa mnadanganywa tu, wale kina Tuisila ni wakalia benchi wa Vita Club ambayo Simba iliwatandika pale nyumbani kwao.
 
Wana Yanga wenzangu timu hatuna na tusitegemee lolote kwenye msimu tu cha msingi tusubirie msimu ujao.

Mpaka sasa
1.Viongozi washapaniki.
2.Mashabiki wamepaniki.
3.Wachezaji wamepaniki leo kwa kifupi timu nzima imecheza ovyo.
4.Kocha nae kapaniki,dk ya 75 una mtoa Niyonzima unamuingiza Mauya akakabe yaani tuna wahofia mpaka hawa polisi,matokeo yake tukawapa nafasi polisi wakachomoa.Kocha ana hofu,muoga,hajiamini na hawaamini wachezaji wake.

Cha msingi tujilaumu hasa upande wa usajili,wenzetu wamesajili bunduki sisi tumesajili mikuki niki mtoa Mukoko na Tk Master hizi sajili nyingine za nje zote hovyo na sizani kama huwaga tunawafuatilia hao wachezaji wa nje naona tunachukua chukua.

So sitegemei mabadiliko kwani tutamaliza ligi na mikuki yetu hii,cha msingi tuvumilie timu hatuna msimu uishe tuanze upya kwani timu nzima haijiamini.
 
Hii timu hivi wako serious kweli hawa wap...uzi.
They are f****cking crazy hawa wachezaji and useless piece of trashes.
Nimekwazika kwa kweli kwa mambo haya wanayofanya wachezaji
Njoo Simba unywe maji ya uzima na hutoona kiu tena! Nchi ya maziwa na asali, ondoka Misri njoo kaanani ww, nchi ya Ahadi
 
Pole mtani, ila nimependa tu hapo mwishoni hivi umeandikaje vile
 
Hiyo itakua sheria yako na labda sio mfuatiliaji wa mpira. Mkisha kuwa wachezaji wa timu moja zaidi ya mmoja mmewatoka mabeki hata mpiagiane pasi elfu kumi hakuna Offside hapo.

Angalia goli la pili la Tp Mazembe utajifunza kitu hapo.

Angalia AZAM SPORTS 1 Wameonesha ni offside,kama kungekuwa na VAR basi wachambuzi wanasema lisingekuwa goli!
 
Hili goli walilofunga yanga kama wangefungwa wao lilitosha kuitisha kikao kulalamikia waamuzi.

Na hii kadi nyekundu ilikuwa ni ticket ya wao kujitoa kwenye ligi waende Zanzibar kama walivyokuwa wakisema.

Ila Mungu si athumani,kubebwa wamebebwa wao kwa goli la offside na point wamedondosha 2 tena
 
Ili utoo awe na matumain ya ubingwa inabidi simba apoteze game tatu
Kitu ambacho ni kigumu mno.
Hawa dawa yao tuwabebe Klabu bingwa & Shirikisho timu ziende nne then tuwaombe CAF tuanze nao mtoano,japo ni ngumu kutokea(Kama watakuwa wa pili, maana Azam Anakuja) , tuwapige nje ndani humu humu nchini then sisi tunasonga mbele kutoka nje ya mipaka ya Tanzania, wenyewe waishie humu humu.
 
Pole mtani, ila nimependa tu hapo mwishoni hivi umeandikaje vile
Kwa mwenendo huu wa timu, tusahau tu kuhusu Ubingwa msimu huu! Kuna wakati tunatakiwa tu kusema ukweli.

Timu yenu hainaga utani dhidi ya hivi vitimu vidogo! Sasa timu yetu sisi wachezaji wanarukaruka tu!

Wamefunga kagoli kamoja, wote wanarudi nyuma kukaba! Tangu lini ushindi wa goli mija ukalindwa!! Mechi na Mbeya City walifanya hivi hivi na kuambulia sare! Sasa utasema tuna kocha kweli!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…