Polisi Tanzania, siyo watu wa kujenga ukaribu nao

Polisi Tanzania, siyo watu wa kujenga ukaribu nao

MBOKA NA BISO

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
766
Reaction score
792

​

Ni mhimu kujifunza hili ; POLISI SIO JAMAA YAKO kama umewahi kuambiwa polisi ni mtanzania mwenzako nadhani afya yako ya akili haipo sawa nenda kapimwe mkojo.

Ipo hivi, Polisi kabla ya kuwa POLISI lazima abadilishwe akili yake na kuwa kama Mbwa yani kule wanapopata mafunzo hubadilishiwa ubongo wao na ndio maana wakiwa mafunzo hawachangamani tena na raia wa kawaida wanakuwa wapo kama bandani.
Siku zote, Mbwa ukimfugia bandani, ukamfunza oda zako siku akitoka bandani sio sawa na mbwa wa mtaani, ndio maana Polisi unaweza kupiga naye stori kama mashikaji wako ila ndani ya saa moja akakubadikikia.

Polisi amefunzwa utiifu, na ndio maana asilimia 40% ya polisi wana shida ya afya ya akili_mental zao haipo sawa mdaa wote ameaminishwa kuna kukabiliana na raia hawapewi mafunzo ya ustarabu na ndio sababu hata ongea ya askari ni tofauti na mchungaji _ we call it command language ipo higher than polite.

Wastani, Ukiona polisi amefunika sura kajianda kutekeleza lolote mbele yake_ unapo kabiriana na polisi mbele yako tambua huyo sio mwenzako ni mwanadamu aliyebadilishwa kufwata utii, wa sheria au oda.

Hakuna kitu kigumu kama kudeal na Polisi hasa unapodai haki zenu, Polisi hawezi kuacha kuingia Field kuna watu wamejikusanya asioneshe kwamba alirusha hata mabomu ya machozi bila kufanya hivyo anakuwa amekiuka wajibu wa kipolisi.

Ningewasisitiza sana polisi, Kujitahidi sana sana kuepuka hisia za wananchi wenyewe ikiwemo kutenda haki na kuona haja kuwa watanzania sio adui zao, leteni rugu kwa wale wote wanaoteka raia na upatikane mwarobaini kwa wale wote wanao kwamisha taifa la Tanzania katika misingi ya haki na Polisi hao hao wasitumike kumwaga damu za watanzania, hili taifa la babu zetu halijawahi kukosa ustarabu ila ukiona watazania wenyewe wamechoka basi, zibebeni hisia zao katika misingi ya haki bila kulazimisha machafuko.

Kwa mfano, watu wakaandamana kutoka barabara A hadi B bila fujo bila kuvutana au kurushiana mawe_ Na polisi wakawa walinzi na mabalozi wa amani kipi kinashindikana hapo ni akili ndogo tu hutumika kuamini kuwa dawa ya moto ni moto.


Imeandikwa na

Dr William Mtanzania Wa USA America​


(Mwandishi wa haki)
 
Kama unajua kabisa wanafundishwa kufuata oda na wameapa kumlinda amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama unataka wasifuate amri then .....
Nb.polisi ni ndugu zetu, wakubwa zetu na mama zetu tupo nao kitaa japo tabia za kubadilika Ghafla na kuwa ka ulivyosema wanazo
 
Katiba ilitakiwa kuweka wazi kwamba jeshi la police halitatumiwa na Wanasiasa kufuata Amri ambazo ni haramu kama kupiga wananchi wakiwa wanatumia uwajibu wao kikatiba kama maandamano ya amani katiba yetu inaitaji kufutwa kabisa kuandika nyingine
 
Wale jamaa wakiwa kwenye operation zao ni hatar

Walinishangaza wakat wa uhamsho zanzibar waliingia na mabuti msikitini
 
Police jau sana hawa jamaa hawafai ata kidogo
Kataa urafiki na police
 
Ndio unajua leo bob?
Sikiliza majibu ya Yohana mbatizaji pale kwenye kijito akimbatiza Yesu manjagu aka polisi walivyomuuliza
 
Mbona kama umeshakua muoga? Au ndo unafanya usafi juu ya dari tarehe 29 ujifiche huko huku unaandamana online?
 
R I P shujaa Hamza hakika ulituheshimisha sana kunyoosha hawa mbwa wa CCM
Screenshot_20210825-132432.png
IMG_20210825_132011_040.jpg
 
Huu ni Uzi wa pili wiki hii kuonya watu wasijenge mazoea na polisi hata mtaani,Kwa hio kifupi polisi ni Majibwa koko usizoeane nao
 
Back
Top Bottom