Polisi Tanzania wabana waachia, sherehe za Pasaka ruksa

Polisi Tanzania wabana waachia, sherehe za Pasaka ruksa

Haahaa Polisi inabidi irekebishwe sana, Mara nyingi wanatoa amri zinazovunja Katiba na Sheria
 
Taarifa ya Polisi kuhusu sikukuu ya Pasaka

Source:

IMG_20210402_191638.jpg
IMG_20210402_191640.jpg
 
Asante Jeshi la Polisi kwa kutuondolea lile wingu la awali
 
Serikali inaendelea na teuzi na tenguzi halafu wananchi wasishangilie Ukombozi wa Bwana Wetu Yesu Kristo

Walilogwa haswa na naniliiii
Pesa za kusherekea dada unazo? Nakukaribisha tuje tusherekee wote!
 
Leo unatoa taarifa leo, na siku inayofuata unakuja kuifafanua.
Je mmeelewa wajameni?
 
Polisi wetu wanazingua sana wakati fulani! Wamewakata watu kipindi kile walipo ulizia mzee yuko wapi!

Baada ya taarifa rasmi kutoka, baadhi ya wadau wakapiga zao ulabu! Wakaambiwa eti wanasherehekea kifo cha mzee! Wanapenda kweli kutumika kwa manufaa ya CCM, badala ya watanzania wote.
 
Tujikumbushe, yule mwendazake wa awamu ya tatu baada ya Mrema kushinda ubunge alisema: Temeke kunavurugu maduka yanachomwa moto! Waandishi wa habari wa wakati huo walipomhoji alikanusha katukatu kuwa aliwahi kusema hivyo!
 
kucheza na Kanisa Katoliki ni kucheza na moto. wakome.
Ni la kawaida sana tu. Sema mliopo humo huwa mnajidanganya kuwa Katoliki ndio kila kitu. Kuna nchi zinaweza kusema hivyo ambazo Katoliki ni 80+. Lakini kwa nchi yako sio kiviiiiile kama mnavyojidanganya.

Eti kucheza na Kabisa Katoliki ni kucheza na Moto
 
Kusema kweli na bila kumung'unya maneno, Jeshi la Polisi linatakiwa lifumuliwe lote haraka sana. Hili Jeshi halipo kulinda raia wa nchi hii na mali zao bali kupambana na raia wasio na hatia wanaotumia haki zao za msingi kama zilivyooanishwa kwenye Katiba.

Mara nyingi hili jeshi limekuwa likikurupuka na matamko ambayo mengi yameelekezwa kwa baadhi ya raia kwa lengo moja tu nalo ni kulinda maslahi ya baadhi ya viongozi. Badala ya kuwa na Jeshi linalolinda amani, tuna jeshi linalochochea uvunjifu wa amani.

Kwa sasa nitaachia hapo lakini yako mengi yametendeka na kutendwa na jeshi hili yanayoliondolea kabisa sifa ya kuitwa jeshi la haki na kuwa jeshi la uonevu. Jeshi hili limetumika kuwabagua Watanzania kwa kujenga chuki miongoni mwao na kuleta taharuki zisizo na maana.
 
Mara baada ya tangazo la kuzuia sherehe za Pasaka hapo jana, leo Polisi wameruhusu sherehe hizo. Swali: Kwanini wanakurupuka?
View attachment 1741336


View attachment 1741313

Tatizo la Polisi ni hiyo statement walivyoitoa mara ya kwanza,inaonesha kuwa hakuna mtaalamu wa habari ili aufanyie uchambuzi wa kimantiki kabla haijatolewa,sasa wanatoa a comfusing statement baafae ndio wanaanza kutafutana
 
Back
Top Bottom