Polisi Tanzania wajengewa uwezo kwa kupatiwa mafunzo ya kisasa nchini Scotland

Polisi Tanzania wajengewa uwezo kwa kupatiwa mafunzo ya kisasa nchini Scotland

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katika kuhakikisha Jeshi la Polisi Tanzania linaendelea kutoa huduma bora na za kisasa kwa wananchi, limeendelea kuwekeza katika mafunzo ya ndani na nje ya nchi kwa maafisa na askari wake, lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi na huduma kwa wananchi katika ulinzi wa maisha na mali zao

Mmoja wa maafisa wanaopata mafunzo hayo ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Abel Paul ambaye kwa sasa yuko jijini Glasgow nchini Scotland akiendelea na mafunzo maalum juu ya utoaji wa huduma za Mipolisi na mbinu za kisasa za kudhibiti uhalifu

ameeleza kuwa Polisi Scotland wamepiga hatua kubwa katika kudhibiti uhalifu kutokana na matumizi makubwa ya teknolojia ya kisasa jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya uhalifu kwa haraka na ufanisi

Aidha, Mkaguzi huyo ameeleza kuwa ujuzi na maarifa mapya wanayoyapata Nchini humo, yataongeza thamani kubwa katika utoaji huduma za Kipolisi nchini Tanzania, hasa katika maeneo ya upelelezi na usalama wa raia

Mafunzo hayo yanatolewa katika kituo cha Police Greater Glasgow Division.kinachojihusisha na masuala ya upelelezi yamelenga kuimarisha uwezo wa kutambua na kutanzua uhalifu kwa kutumia mbinu za kiteknolojia

A/INSP Abel amepongeza Polisi Scotland kwa weledi wao na matumizi sahihi ya teknolojia katika kazi za kila siku za ulinzi na usalama

Vilevile, ameonyesha kufurahishwa kuona kuwa baadhi ya mikakati ya kiusalama inayotumika Scotland tayari imeanza kutekelezwa Tanzania, kama vile matumizi ya.kamera za AI (Artificial Intelligence) zinazotumika kutambua matukio ya uhalifu teknolojia ambayo tayari ipo katika baadhi ya miji mikubwa kama Arusha

Amesisitiza kuwa kupitia mafunzo hayo, atahakikisha anaboresha zaidi utekelezaji wa teknolojia hizo ili kuongeza imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi

A/INSP Paul pia amepongeza kuwa uhusiano mzuri kati ya wananchi wa Scotland na Polisi ambapo wananchi wanatoa taarifa kwa hiari kuhusu wahalifu, hali ambayo imekuwa chachu kubwa katika kudhibiti uhalifu jambo analotamani kuliona pia Tanzania

Katika hatua nyingine amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Camillus Wambura kwa kumpa fursa ya kujifunza nje ya nchi na akaahidi kuwa wananchi wa Tanzania watege
 
Waste of resources, wamekaa kisiasa sana, vichwa empty. Dawa ni kulifumua lote pamoja na viongozi wao wasio na weledi. Hilio sio jeshi la kuhudumia watanzania, ni jeshi la kuhudumia wahuni wachache.
 
Hapo ni mpaka mitaala ibadilke. Hii mitaala yao ya sasa ya kuchukua watoto wa kota wanaovuta bangi, na waliofeli mtihani wa kidato cha nne kwa kupata division four ya 28! Kamwe hauwezi kuwafanya kuwa watu werevu. Badala yake utaendelea tu kuwafanya kuwa watu wa kutumia nguvu nyingi zaidi, kuliko akili.
 
Back
Top Bottom