Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Synagog church of all nation.Natabiri watu kuzidi kuongezeka baada ya hill tukio...Mungu atupe macho ya kutambua which is kipi bila ya hivyo tutakuwa watumwa wa Dini mpaka siku ya parapanda
Sent using Jamii Forums mobile app
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limemtaka mtume Boniface Mwamposa kujisalimisha mwenyewe polisi kwa mahojiano kutokana na vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro jana usiku Jumamosi Februari Mosi, 2020.
Watu hao walifariki usiku wakati waliposhiriki kongamano la kidini uwanja wa Majengo, wakigombea kukanyaga mafuta ya upako yaliyomwagwa milango ya kutokea uwanjani.
Wakati Jeshi hilo likimsaka kwa udi na uvumba kiongozi huyo wa kiroho, Jeshi hilo linawashikilia watu saba akiwamo mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa kwa mahojiano.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Februari 2, 2020 amesema mchungaji huyo ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosi.
“Baada ya hilo tukio tumemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa ambaye ni maarufu kwa jina la Bulldozer bila mafanikio. Kupitia kwenu tunamtaka ajisalimishe kwa mahojiano,” amesema
Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, wawili wakiwa ni wa kike na watu wazima 16 wakiwamo wanawake 15.
Kwa mujibu wa Kamanda Hamduni, katika tukio hilo watu waliojeruhiwa ni 16 na wawili kati yao hali zao sio nzuri na kwamba kazi itakayoendelea kuanzia asubuhi ni kutambua miili ya marehemu iliyohifadhiwa Hospitali ya Mawenzi.
Mwananchi
Nabii feki anavaa chain ina nyokaNabii anatowekaje ???
Mtume wa Mungu anakimbia polisi ?????
Mbona akina Paulo walikuwa wanakaa gerezani ?? Akina Petro walifungwa Sana tuu inakuwaje huyu anakimbia ???
Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ni mchezo wa kutupoteza kuhusu Mada ya Makonda watuonyeshe hizo Maiti.tusikubali.Jeshi la Polisi nchini Tanzania limemtaka mtume Boniface Mwamposa kujisalimisha mwenyewe polisi kwa mahojiano kutokana na vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro jana usiku Jumamosi Februari Mosi, 2020.
Watu hao walifariki usiku wakati waliposhiriki kongamano la kidini uwanja wa Majengo, wakigombea kukanyaga mafuta ya upako yaliyomwagwa milango ya kutokea uwanjani.
Wakati Jeshi hilo likimsaka kwa udi na uvumba kiongozi huyo wa kiroho, Jeshi hilo linawashikilia watu saba akiwamo mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa kwa mahojiano.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Februari 2, 2020 amesema mchungaji huyo ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosi.
“Baada ya hilo tukio tumemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa ambaye ni maarufu kwa jina la Bulldozer bila mafanikio. Kupitia kwenu tunamtaka ajisalimishe kwa mahojiano,” amesema
Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, wawili wakiwa ni wa kike na watu wazima 16 wakiwamo wanawake 15.
Kwa mujibu wa Kamanda Hamduni, katika tukio hilo watu waliojeruhiwa ni 16 na wawili kati yao hali zao sio nzuri na kwamba kazi itakayoendelea kuanzia asubuhi ni kutambua miili ya marehemu iliyohifadhiwa Hospitali ya Mawenzi.
Mwananchi
Wataachaje sasa Kwani Wewe hupendi upako?Utakuta maaskari na wenyewe wanaomba mafuta ya upako.
Hawa jamaa wamewekeza kwenye ujasiriadini kule mbeya kuna kata fulani yaani kila baada ya nyumba tatu kuna kanisa hyo kata ipo baada ya mbalizi ukiwa unakuja mjini jina limenitokaDuh hivi hawa wanyakyusa wenzangu hawana uwekezaji mwingine zaidi ya dini,dah mara Mwamposa mara Mwambapa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Upepo wa kisulisuliWanawake mna nini, maana ndio mmejaa huko kwa Hawa matapeli.