Polisi Tanzania yamkamata gaidi raia wa Uingereza!

Polisi Tanzania yamkamata gaidi raia wa Uingereza!

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
Saturday, July 5, 2013

Jeshi la Polisi nchini limemtia mbaroni mtu mmoja mjini Mbeya anayedaiwa kuhusika na vitendo vya ugaidi akiwa na hati mbili za kusafiria, na mwingine Mtanzania adakwa akidaiwa kusaidiana naye.

Mtu huyo aliyekamatwa wilayani Kyela, pia anatuhumiwa kuhusika na vitendo vya ugaidi nchini Uingereza.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alisema mtuhumiwa huyo alikuwa anatumia majina mawili tofauti kwenye hati za kusafiria na alikuwa akijaribu kuvuka mpaka wa Tanzania kuelekea Malawi.

Alisema mtuhumiwa huyo alitumia hati ya Tanzania yenye namba AB 651926 yenye jina la Adil Ally Patel na hati ya Uingereza yenye namba NO 51555382 yenye jina la Iqbal Hassan Ally.

Manumba alisema hati ya Tanzania aliyokamatwa nayo ni kati ya hati 26 zilizoibiwa kwenye Ofisi za Uhamiaji mwaka mmoja uliopita.

Alisema mshukiwa wa ugaidi alikuwa akisaidiwa na Mtanzania mmoja ambaye hakumtaja jina na baada ya kukaguliwa kompyuta mpakato (laptop) yake ilikuwa na maneno ya uchochezi ya kidini kuhusu imani tofauti.

Manumba alisema aliwasiliana na Serikali ya Uingereza kuhusu hati ya mtuhumiwa huyo na kuelezwa kuwa ni halali na kufahamishwa kuwa mtu huyo wanamtafuta kwa tukio la ugaidi nchini Uingereza.

Alisema kuna Mtanzania mwingine ambaye hakumtaja jina, alikamatwa kwa kuhisiwa kujihusisha na mtuhumiwa huyo wa ugaidi ambaye baada ya kukaguliwa pia alikutwa na kompyuta yenye maneno ya uchochezi dhidi ya dini isiyomhusu.

Alisema mtuhumiwa huyo alijitambulisa kuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo kimoja kilichopo nchini Sudan.

Manumba aliwataka wazazi kuwa waangalifu na vijana wao wanaokwenda kusoma nje ya nchi kwa kuwa baadhi yao hurubuniwa na kujiingiza katika mambo yanayohusiana na ugaidi.

Aliongeza kuwa polisi wana uhakika kwamba kuna baadhi ya vikundi vya kigaidi ndani ya nchi ambavyo vina mipango ya siri ya kutekeleza ugadi nchini.

Aliwataka Watanzania kuwa waangalifu wakati polisi ikifanya kazi yake ya uchunguzi na kuonyesha kuwa hali ya usalama si nzuri nchini kutokana na matukio ya kihalifu yanayoendelea.

Aidha, alisema polisi inaendelea na uchunguzi dhidi ya matukio ya mlipuko miwili ya mabomu iliyotokea mkoani Arusha na lile la kuuawa kwa Padri Evarist Mushi, Zanzibar.

Alisema matukio hayo yameonyesha sura mbaya kwa Tanzania ya kuwepo kwa tishio la ugaidi.

Alisema uchunguzi utakapokamilika washitakiwa watafikishwa kwemnye mikono ya sheria kuhukumiwa kwa makosa ya jinai.

Aliongeza kuwa taarifa zitakazokuwa zikitolewa na raia wema zitasaidia polisi kurahisisha uchunguzi na kuwakamata wahusika kwa wakati.

Manumba ametahadharisha kuwa ongezeko la uhalifu nchini limekuwa likihusisha baadhi ya wananchi kutumika vibaya na wavunjifu wa amani.

Alisema kufuatia matukio hayo, baadhi ya watuhumiwa wanashikiliwa na baada ya uchunguzi kukamilika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Hii ni sifa mbaya Watanzania wanapaswa kujiepusha na vishawishi vya aina yoyote vitakavyopelekea kuvunjika kwa amani iliyopo tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania, alisema.

Katika matukio ya kigaidi yaliyotokea siku za hivi karibuni watu watatu walikufa na zaidi ya 70 kujeruhiwa baada ya kurushwa bomu kanisani na mtu asiyefahamika katika kanisa la Katoliki Jimbo Kuu la Arusha wakiwa wamejumuika katika uzinduzi wa Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti.

Katika tukio jingine jijini humo, bomu lilipuka kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) eneo la Soweto kata ya Kaloleni mkoani Arusha.

Katika tukio hilo watu watatu walifariki dunia kutokana na mlipuko wa bomu wakati chama hicho kikiwa kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani.

Wakati huo huo Manumba alisema polisi jijini Dar es Salaam limekamata meno ya tembo 347 katika eneo la Kimara ambayo yanaamika yamepatikana kwa njia za kijangili katika mbuga za Tanzania.

Alisema mbali na nyara hizo, kuna meno mengine ya tembo 788 yalikamatwa nchini Malawi katika mji wa Mzuzu na kwamba inaamika kuwa yalisafirishwa kutoka Tanzania kama mzigo wa saruji kutoka katika kiwanda cha Saruji Mbeya.

Manumba alisema polisi nchini wanafanyakazi kwa kushirikiana na polisi wa kimataifa kuhakikisha kuwa ukweli wa matukio yanakuwa wazi na uchunguzi ukikamilika wahusika watafikishwa katika vyombo vya sheria.[/FONT][/SIZE][/COLOR][/FONT][/COLOR]
 
Inahitajika tafsiri mpya ya ugaidi sasa........wamekagua wamekuta maneno ya uchochezi wa kidini........huu nao ni ugaidi ....anyway.....
 
Hivi ukiwa mtanzania lazima ujue kiswahili?eti manumba anasema mtanzania gani hajui kiswahili!nakumbuka nilisoma na watoto waliorejea toka balozi za nje walikua hawajui kiswahili na huku ni watanzania 100%. Na kuwa na passport 2 ni kosa maana wahindi wana passport za india, tanzania, canada.
 
Kama kawaida Polisi-CCM wanatengeneza Muvi nyingine ya kuwasafisha!
tulishawazoea...yote haya yana mwisho wake!
 
Ni kazi waliyopewa na vyombo vya usalama vya UK, si rahisi kihivyo kumkamata mtu ndani ya UK au Ulaya ya Magharibi kwa kosa la ugaidi kutokana na sheria zao.

Ni kawaida sana kwa askari wa nje wakati wanamfuatilia Muislamu na wakikwama kumkamata kutokana na sheria zao au kuogopa backlash yoyote ile basi humsubiri atoke nje ya nchi kwenda "third world" akifika huko huwaagiza askari wa hiyo nchi ya third world kumkamata kwa sababu yoyote ile hata kama ni kwenda kinyume cha sheria zao wenyewe (hiyo nchi ya third world). Kazi ya nchi ya third world ni kumkamata tu lakini wao wamagharibu ndio wanaohusika na kumhoji, kupendekeza aina gani za adhabu apewe n.k

Wakati mwingine kama husafiri kuelekea nchi wanzozitaka basi hukusumbuasumbua mpaka uone kuwa kuna haja ya kutoka nje na kwenda kupumzika kidogo, hapo wakala wa tiketi hufanya kazi yake ya kukupa angalau transit katika nchi wanayoona inawafaa kukukamata.

..njaa mbaya sana!
 
usaniinkama kawaida ya policcm, lile zee ndugu la jk (ilunga) lililorekodi cd nyingi za uchochezi mbona hawaja muita gaidi au hadi waambiwe na uk? kesi iko ya ilunga wapi? nyie police wajinga tu
 
Kawaida ya polisi wetu kakamatwa na pasi mbili basi huyu ni gaidi, kwa vile wameshindwa kupata ukweli passi za tanzania zipo na zinapatikana kama njugu na inajulikana watu wa kutoka nje wanazinunua na huwa wanagongwa na mihuri pale airport wanaingia kama wa TZ ili wasilipe visa na pia wanakaa muda mrefu ni mchezo upo.

Hata wala ambao niwakimbizi kule UK pasi zao za TZ hawaja zirejesha wanazo na wanazitumia wakifika hapa kwa kujuana na uhamiaji, sasa tusubiri maana polisi wetu ikitokea ujambazi posta na kesho yake akikamatwa jamaa kwa kukimbizana na polisi basi huunganishwa kwamba ndie anahusika na wizi wa posta, huo ndio utendaji wao.
 
Kama kawaida polis Wameanza muvu zao! Mi siwaamini hata kwa punje, polisi wanmbambikia mwananchi FUVU LA KICHWA!!
 
Nilipokea taarifa hii kwa tahadhari sana. Najaribu kuangalia kinachotaka kutengenezwa!!! Nahisi kuna mazingira yanatengenezwa. Let's wait!!!
 
hivi ukiwa
mtanzania lazima ujue kiswahili?eti manumba anasema mtanzania gani hajui
kiswahili!nakumbuka nilisoma na watoto waliorejea toka balozi za nje
walikua hawajui kiswahili na huku ni watanzania 100%
.Na kuwa
na passport 2 ni kosa maana wahindi wana passport za
india,tanzania,canada

ni moja ya mbinu ya kumgundua asiye raia wa Tanzania mkuu, hata uhamiaji wanaitumia sana mipakani
 
Nilipokea taarifa hii kwa tahadhari sana. Najaribu kuangalia kinachotaka kutengenezwa!!! Nahisi kuna mazingira yanatengenezwa. Let's wait!!!
Tatizo mna akili sana,
Kwa hiyo mazingira gani yanatengenezwa? au polisi wasifanye kazi kabisa sasa?
 
if you Google both names...hutayaona...sasa kama ni gaidi anaetafutwa...basi...hayo majina uki search tu basi yangejitokeza hasa kama UK wamethibitisha kuwa wanamtafuta....manumba amerudi baada ya kupona..na stori zake.....naona alikosa kuwasingizia waislam ...alipokuja obama..so...anatafuta masifa..

Huyu ni mhanga tu.....chadema wanasema wanayo video ya arusha....na mashahidi wengi wanasema ..mhusika alilindwa na polisi...!!! mpaka leo polisi hawajakanusha madai haya.

Na kule arusha kanisani mtuhumiwa amekamatwa na hakuna ushahidi wa mhindi kuwapo huko arusha..zaidi ya warabu wa UAE NA SADIA WALIOCHIWA.

HAYA matokea yote yalitokea manumba hayupo kazini nadhani...lakini ..kwa vile ana ajenda na waislam basi angewabamiza sana lakini muugu mkubwa.

Kuna suala anazungumza kwa uongo..kuhusu.....vijana wa kitanzania waliokamatwa kuhusiana na matukio ya 1998...anasema wale walikwenda kusoma pakistani...ni uongo...inajulikana wazi wale vijana masikini walivamia wageni bila ya kujua kinachoendela....hakuna laiyewahi kusafiri kwenda hata kenya....lakini anasema kuwa wale kina ghailani na wenzake walikwenda kusoma ugaidi nje...ni uongo...manumba anachukia waislam na ana ajenda ya kina bush na wenzake....lakini Mungu Mkubwa...ukweli utadhihiri tu...
 
Yule ambaye video yake ya uchochezi kuhusu dini isiyo yake iko kwenye public domain (Youtube) bado hajakamatwa lakini huyu ambaye laptop yake ina maneno ya uchochezi kawekwa kolokoroni...duh Tanzania yetu.
 
Nilipokea taarifa hii kwa tahadhari sana. Najaribu kuangalia kinachotaka kutengenezwa!!! Nahisi kuna mazingira yanatengenezwa. Let's wait!!!

By Reuters
2:02PM BST 06 Jul 2013

Assan Ali Iqbal reportedly appeared before Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam on Friday charged with four counts, including the theft of 26 passports. He denied the charges and was remanded in custody. Four other people are facing similar counts.

The Foreign Office confirmed a British national had been arrested in Tanzania and they are offering consular assistance.

Several people have been arrested on terrorism charges in Tanzania since bombings killed at least eight people in May and June.

Authorities in Tanzania, one of the region's most stable countries, are concerned at the growth of an Islamist movement accused of indirect links to Somalia's al Shabaab rebels.

Tanzanian police said they had verified Mr Ali's British passport as being authentic. They said the Tanzanian passport he was carrying was a fake.
source: Briton arrested in Tanzania - Telegraph

Ni kweli taarifa ya Reuters ni fupi lakini inaeleweka zaidi ya taarifa za Polisi/Magazeti ya Tanzania hivyo inabidi kusomwa kwaumakini mkubwa
 
Mipaka ya Tanzania haiko salama kabisa huu ni uongo na mbinu za polisi kutaka ujiko usio na mbele wala nyuma. Ni raia wangapi wa kigeni wanaoingia nchini kama vile wanakwenda sokoni? Tena mipaka kati yetu na nchi zote zinazotuzunguka watu wanaingia kiholela tu na kufanya wanavyotaka, bila kusahau vurugu zilizotokea kwenye mpaka wetu na Zambia. Je wanaweza kuueleza umma fujo zile zilisababishwa na nini? Je, wanachukua hatua zipi kuona kwamba mipaka yetu inakuwa salama? Je, wanatumia mbinu gani kukagua magari ya abiria yanayosafiri kutoka nchi jirani na wameweza kuwanasa wageni wangapi na wanashirikiana vipi na wizara ya mambo ya ndani? Je, wanaweza kutueleza ilikuwaje raia kutoka Ethiopia oops sijui Somalia waliokufa kwenye kontena .. ..... ... hatua zipi zimechukuliwa tangu walipokufa wale marehemu?


BTW huyu jamaa kwa sababu ana passport ya Uingereza mtasikia wamemwachia na kupelekwa UK ambako hawatamfanya chochote kwa sababu hakuna hata chembe ya ushahidi. Hatujasahau jinsi Polisi wa Tanzania pamoja na Serikali isiyojali raia wake walipowaachia wale wanajeshi wa Uingereza walioshiriki kuwaua warembo wa kitanzania na kuwatupa baharini.
 
Back
Top Bottom