Polisi Tanzania yamkamata gaidi raia wa Uingereza!

Polisi Tanzania yamkamata gaidi raia wa Uingereza!

Halafu anashitakiwa kwa wizi wa hati za kusafiria na ameunganishwa na washitakiwa wengine wa wizihuo. hili la ugaidi hakushitakiwa nalo. Mapolisi wetu hupenda sifa za kijinga zinazoitia sifa mbaya nchi.
 
Hii nchi mradi tunaamka tu,haieleweki inakwenda mbele au inarudi nyuma
 
Inahitajika tafsiri mpya ya ugaidi sasa........wamekagua wamekuta maneno ya uchochezi wa kidini........huu nao ni ugaidi ....anyway.....
Kuwa na passport zaidi ya 1 huku ukiwa na ya Tanzania ni kosa maana Tanzania haitambui uraia wa nchi 2..Kama unataka uraia wa Tz lazima ukane uraia wa mwanzo...hii ni kwa mujibu wa sheria though mick mouse zipo sana tu watu wa immigration watatuletea magaidi
 
Hizi passport ziliibiwa lini? Na mbona hawakusema chochote huo wizi ulipotokea? This is really worrying kama kuna uwezekano wa mtu au watu kuingia uhamiaji na kujichukulia tu passport, ninaamini this is almost impossible kama mwizi hakushirikiana na watu wa ndani. Sasa kwanini hatuambiwi ukweli? Huyu jamaa ndio kakamatwa na passport fake lakini kuna watu wa ndani waliompa na watakua walivuta hela nzuri, sasa hao wa ndani wamefanywa nini? Tuondoe chanzo cha tatizo kwanza.
 
Tatizo mna akili sana,
Kwa hiyo mazingira gani yanatengenezwa? au polisi wasifanye kazi kabisa sasa?

Ni Polisi wepi unaowatetea? Hawahawa wachumia tumbo na makuwadi wa CCM wakiwemo kina Manumba, Chagonja, Kamuhanda, Mgulu, Saidi Mwema n.k. Au unazungumzia wengne?
Polisi wa Tanzania ni corrupted, wamepofushwa na rushwa iliyoshamiri hadi Makao Makuu yao wakidaiana rushwa wao kwa wao! Unapotokea uhalifu wenye mkono wa Polisi utamsikia Bosi wao (Kada wa CCM) akizuga kuunda Tume ya watu walewale kwenda "kuchunguza" (Soma kupoteza ushahidi) kisha hakuna lolote!
Shame on them and their masters - CCM!
 
Hapo nami sijaona kosa lake la ugaidi!kama pass yake ya Tanzania iliibiwa sio kosa lake!vipi akionyesha docs zoote alizoombea hiyo pass?ukiwa na '....uchochezi wa dini ingine'kwenye laptop sidhani pia kama ni kosa!maana hajashikwa akisambaza au akihubiiri!maana movie zote ziko youtube!hawa polisi wamechemka!hawana chao hapo!!watulizane!ugaidi sio hivyo!
 
Ni kazi waliyopewa na vyombo vya usalama vya UK, si rahisi kihivyo kumkamata mtu ndani ya UK au Ulaya ya Magharibi kwa kosa la ugaidi kutokana na sheria zao. Ni kawaida sana kwa askari wa nje wakati wanamfuatilia Muislamu na wakikwama kumkamata kutokana na sheria zao au kuogopa backlash yoyote ile basi humsubiri atoke nje ya nchi kwenda "third world" akifika huko huwaagiza askari wa hiyo nchi ya third world kumkamata kwa sababu yoyote ile hata kama ni kwenda kinyume cha sheria zao wenyewe (hiyo nchi ya third world). Kazi ya nchi ya third world ni kumkamata tu lakini wao wamagharibu ndio wanaohusika na kumhoji, kupendekeza aina gani za adhabu apewe n.k Wakati mwingine kama husafiri kuelekea nchi wanzozitaka basi hukusumbuasumbua mpaka uone kuwa kuna haja ya kutoka nje na kwenda kupumzika kidogo, hapo wakala wa tiketi hufanya kazi yake ya kukupa angalau transit katika nchi wanayoona inawafaa kukukamata. ..njaa mbaya sana!

Mkuu mbona Waingereza hawana utani na mambo ya Ugaidi, hawaogopi backlash wala nini - wanafatilia kwa karibu mpaka sleeper cells za magaidi na kuwatia mbaroni wahusika kabla hawaja tekeleza maovu yao.

Taifa linalo aminika duniani katika nyanja za upelelezi/ujasusi wa ndani na nje aliwezi kumwachia RAIA wake anaye hisiwa ni GAIDI atumie passport halali ya TAIFA hilo bila ya kumtia mbaroni!! Hii si kawaida ya Waingereza.

Mimi si amini kama Taifa hilo linaweza kumtoa kafara RAIA wake ili akamatwe kwenye third World Country kwa kuogopa backlash nchini mwao, Waingereza ni majasiri sana hawawezi kufanya usanii katika mambo ya ugaidi, wana amini kwamba a good GAIDI ni yule aliyekufa! huyo tu ndiye hawezi kuleta madhala ndani ya TAIFA lao.

Mafisa wa usalama wakikutilia mashaka wanakupiga risasi popote pale hata ukiwa barabarani au usafiri wa underground, kuna kijana wa Argentina au Brazil sikumbuki vizuri aliwahi kupigwa risasi na afisa wa usalama kwa kushukiwa ni GAIDI. Nawapongeza POLISI wa Tanzania kwa kufanikisha kuwatia mbaroni wahusika, lakini hili la mtu huyo wa Uingereza kupatikana na pass ya kusafiria ya Tanzania zinazo semekana zilihibiwa Tanzania mwaka jana, hapo hapo jamaa huyo ana passport ya UK na "anatafutwa" kwa kujihusisha na mambo ya ugaidi! Swali ni je alikuwa anatafutwa na Uingereza kweli au wanataka backlash ihamie kwetu.
 
Wapitie JF mbona yamejaa hayo "maneno ya uchochezi ya kidini kuhusu imani tofauti".
 
Ndio maana wengine hatusomi magazeti yetu haya.
Hii habari magazeti yamepotosha tena makusudi nahisi kwa maelekezo maalum.
Ukisoma mashirika ya nje hii habari imeandikwa tofauti kabisa!
Hatuna vyombo makini vya habari!
 
Amini usiamini hii ni movie nyingine ya polisi, kutaka kupotezea,matukio ya mabomu mawili yaliyolipuka Arusha. Lile la kanisani Olesiti na lile la kwenye mkutano wa Chsdema,ambapo hadi sasa polisi,hawajafanikiwa kuwakamata watuhumiwa wowote.

Kwa kweli watanzania hivi sasa tushazoea sana staili yao jeshi la polisi,la kuua soo kiaina.

Si mnakumbuka issue ya kutekwa Dr Ulimboka? Namna kamanda Kova alivyojitokeza kwa mbwembwe kwenye vyombo vya habari na kuwaaminisha waTZ,kuwa wamemkamata mtu aliyemteka Ulimboka,yule chizi Mkenya?

Si kila mtu anajua kuwa hata hiyo kesi yenyewe ya yule mkenya,imefutwa kimya kimya na yule chizi mkenya,amerejeshwa kwao?!

Sasa kwa mazingira hayo,huyo Manumba anategemea mtanzania gani ataliamini jeshi la polisi,wakati ushahidi wa mazingira unaonyesha kuwa jeshi hilo ndilo linapanga matokeo hayo ya kigaidi?!

Hivi inawezekanaje katika matokeo yote ya utata yanayotokea ya ugaidi,ambapo jeshi la polisi nao ni watuhumiwa,wakati wote wanalazimisha,wao pekee,ndiyowawe wachunguzi wa matukio hayo?!

Ni kwa nini jeshi la polisi na JK wao wameendelea kukataa katakata,kuondoa mzizi huu wa fitina kwa kuundwa chombo huru cha uchunguzi cha Judiciary inquiry commission.

Hivi jeshi la polisi na JK wao,hawaoni kuwa kwa kukataa kwao kuundwa kwa chombo huru cha uchunguzi wa matukio hayo,wanawapa ushahidi usio na vmashaka yoyote kuwa jeshi hilo na vyombo vingine vya dola vya nchi hii ndiyo wahusika wakuu wa matulio yoteya ugaidi yanayotokea ndani ya nchi yetu!
 
Mkuu mbona Waingereza hawana utani na mambo ya Ugaidi, hawaogopi backlash wala nini - wanafatilia kwa karibu mpaka sleeper cells za magaidi na kuwatia mbaroni wahusika kabla hawaja tekeleza maovu yao.

Taifa linalo aminika duniani katika nyanja za upelelezi/ujasusi wa ndani na nje aliwezi kumwachia RAIA wake anaye hisiwa ni GAIDI atumie passport halali ya TAIFA hilo bila ya kumtia mbaroni!! Hii si kawaida ya Waingereza.

Mimi si amini kama Taifa hilo linaweza kumtoa kafara RAIA wake ili akamatwe kwenye third World Country kwa kuogopa backlash nchini mwao, Waingereza ni majasiri sana hawawezi kufanya usanii katika mambo ya ugaidi, wana amini kwamba a good GAIDI ni yule aliyekufa! huyo tu ndiye hawezi kuleta madhala ndani ya TAIFA lao.

Mafisa wa usalama wakikutilia mashaka wanakupiga risasi popote pale hata ukiwa barabarani au usafiri wa underground, kuna kijana wa Argentina au Brazil sikumbuki vizuri aliwahi kupigwa risasi na afisa wa usalama kwa kushukiwa ni GAIDI. Nawapongeza POLISI wa Tanzania kwa kufanikisha kuwatia mbaroni wahusika, lakini hili la mtu huyo wa Uingereza kupatikana na pass ya kusafiria ya Tanzania zinazo semekana zilihibiwa Tanzania mwaka jana, hapo hapo jamaa huyo ana passport ya UK na "anatafutwa" kwa kujihusisha na mambo ya ugaidi! Swali ni je alikuwa anatafutwa na Uingereza kweli au wanataka backlash ihamie kwetu.
Hujui kinachoendelea!
 
Ni kazi waliyopewa na vyombo vya usalama vya UK, si rahisi kihivyo kumkamata mtu ndani ya UK au Ulaya ya Magharibi kwa kosa la ugaidi kutokana na sheria zao.

Ni kawaida sana kwa askari wa nje wakati wanamfuatilia Muislamu na wakikwama kumkamata kutokana na sheria zao au kuogopa backlash yoyote ile basi humsubiri atoke nje ya nchi kwenda "third world" akifika huko huwaagiza askari wa hiyo nchi ya third world kumkamata kwa sababu yoyote ile hata kama ni kwenda kinyume cha sheria zao wenyewe (hiyo nchi ya third world). Kazi ya nchi ya third world ni kumkamata tu lakini wao wamagharibu ndio wanaohusika na kumhoji, kupendekeza aina gani za adhabu apewe n.k

Wakati mwingine kama husafiri kuelekea nchi wanzozitaka basi hukusumbuasumbua mpaka uone kuwa kuna haja ya kutoka nje na kwenda kupumzika kidogo, hapo wakala wa tiketi hufanya kazi yake ya kukupa angalau transit katika nchi wanayoona inawafaa kukukamata.

..njaa mbaya sana!

"Kutokana na sheria zao". Inaonekana hizo "sheria zao" ni nzuri sana; huwapa hata magaidi haki ya kutamba jinsi wanavyotaka bila kubugudhiwa na "sheria hizo".
 
"Kutokana na sheria zao". Inaonekana hizo "sheria zao" ni nzuri sana; huwapa hata magaidi haki ya kutamba jinsi wanavyotaka bila kubugudhiwa na "sheria hizo".
Dudus!
Mfano mtu mwenye kuchangisha sadaka na wanamtlia mashaka huko anakozipeleka au mwenye kutoa maneno kwenye mihadhara ambayo wao wanaona mtu huyu anaelekea kwenye ugaidi, sanasana watamshitaki mtu huyu kwa uchochezi na hata kama akifungwa kwa uchochezi baada ya muda mfupi tu yupo mitaani anadunda!

Hapo ndipo njia nyingine zinapotumika , Marekani kwao wao ukitoka nje ya Marekani wanakuweka kwenye non flying list na hakuna shirika litakalo kuchukua kurudi Marekani! utabaki "kusaidiwa" aina ya msaada mwingine na ubalozi wao kama kuna ubalozi katika hiyo nchi.
 
"Manumba alisema hati ya Tanzania aliyokamatwa nayo ni kati ya hati 26 zilizoibiwa kwenye Ofisi za Uhamiaji mwaka mmoja uliopita."

Polisi walifuatilia wizi huo wa pasi za kusafiria? walimkamata nani? kama walishindwa waseme nini kilikuwa kikwazo? ina maana kweli wameshindwa kujua na hata alisababisha uzembe hadi zikaibwa? Hivi hati zikiibiwa na namba zake si zina julikana kwanini hazikutangazwa kuwa zisitumike kwa serikali mbalimbali?

....?

Maswali ni mengi mno!
 
Manumba acha kuuchukia waislam na uislam!
Usitutajie jina la huyo mtanzania uliemkamata ila tujulishe hayo maneno ya kichochezi yaliyotajwa kwenye hiyo cd.
Manake mlishamfunga DIBAGULA kwa kusema YESU SI MUNGU eti anawakashifu wakristo wakati kwa imani ya waislam na QUR AN inasema YESU SI MUNGU.
Mwarabu na muislam anaetimiza imani yake kikamilifu lazima ataambiwa kuwa yeye ni gaidi, hata kule arusha walikamatwa waarabu kwa sababu ya uarabu wao tu.
Ndo maana tunasema katika vurugu za kidini serikali inachangia sana mgawanyiko wa kidini kwa sababu za kijinga kama hizi.
Hata tukisema kuwa serikali inawapendelea wakristo kwa kuwapa mabilioni ya walipa kodi wa tanzania ambao ni dini tofauti, utasikia kuwa huu ni uchochezi.
Inamana kusema ukweli ndio uchochezi?
Serikali mnatuumiza sana waislam kwa hili, yaani waislam wa tanzania wamekuwa kama watumwa katika nchi yao.
Muislam mnaemtaka ni yule siku mojamoja anakula nguruwe! Analewa, mzinifu n.k.
Ila mungu yupo!
INSHAALLAH katika hili ALLAH awalipe kinachostahili kwa uonevu huu kila ambae anahusika!
 
Tuwape polisi fursa ya kutimiza wajibu wao.

Je kama na wao ni sehemu ya watuhumiwa wanaweza kutimiza wajibu wao kweli?

Maneno ya uchochezi wa kidini nao ni ugaidi
 
Mkuu mbona Waingereza hawana utani na mambo ya Ugaidi, hawaogopi backlash wala nini - wanafatilia kwa karibu mpaka sleeper cells za magaidi na kuwatia mbaroni wahusika kabla hawaja tekeleza maovu yao.

Taifa linalo aminika duniani katika nyanja za upelelezi/ujasusi wa ndani na nje aliwezi kumwachia RAIA wake anaye hisiwa ni GAIDI atumie passport halali ya TAIFA hilo bila ya kumtia mbaroni!! Hii si kawaida ya Waingereza.
Taifa unalolisifia namna hii kwa upelelezi na ujasusi limezidiwa akili na "gaidi" mmoja tu! amefanikiwa kutoka ndani ya mipaka ya Uingereza bila ya kujua mpaka wanakuja kuzindushwa na polisi wa Tanzania! ha ha!

"Manumba alisema aliwasiliana na Serikali ya Uingereza kuhusu hati ya mtuhumiwa huyo na kuelezwa kuwa ni halali na kufahamishwa kuwa mtu huyo wanamtafuta kwa tukio la ugaidi nchini Uingereza".

Watanzania wasifurahie! inaonyesha kuwa kuna mengi nyuma ya pazia! ni kitu cha kusikitisha sana kuwa Tanzania inafikia hali hii na bado tutakuja kuwaona Wasomali wakati watakapochokwa Ulaya na Marekani watahamishiwa Tanzania kama tafsiri ya mikataba ambayo Tanzania yenyewe imesaini
 
The police force is trying to hide their mess under the carpet, Mbowe has the video what is the move about, That sick man has come up with a fake movie
 
Back
Top Bottom