Polisi Temeke imarisheni ulinzi muda huu katika tamasha la Vuka na Chako kwani walioshindwa kuingia Wanaporwa na Vibaka

Polisi Temeke imarisheni ulinzi muda huu katika tamasha la Vuka na Chako kwani walioshindwa kuingia Wanaporwa na Vibaka

Cognizant

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2022
Posts
626
Reaction score
1,409
Mbele ya Msikiti unaotizamana na Petro Station iliyo Jirani na Mgulani Barracks kuna Vibaka hapo na wakipora wanakimbilia kule Makaburini.

Kwingineko ni huku kama unakuja ilipokuwa TCC kuelekea Kona ya Keko kuna Kipande hapo kina Giza Watu Wanaporwa.

Tafadhali kwakuwa Uwanja umejaa mpaka Pomoni waanrisheni Watu walioko Nje warejee Makwao kwani wakiendelea Kulazimisha kuwa hapo na Wengine kutaka Kuingia Cognizant (alias) Adorable Angel Mimi naiona Stampede na huenda hata Watu Kujeruhiwa au Kufa pia na ikamharibia Muandaaji wa Tamasha la Vuka na Chako leo.
 
Hivi kwa nini matamasha ya mwamaposa huwa hayana ulinzinwa kutosha? Ashajua ana waumini wengi basi akiwa anaandaa matamasha yake awe na plan nzuri ya ulinzi wa ndani na nje.
 
Hivi kwa nini matamasha ya mwamaposa huwa hayana ulinzinwa kutosha? Ashajua ana waumini wengi basi akiwa anaandaa matamasha yake awe na plan nzuri ya ulinzi wa ndani na njee
Sahih kbsa
 
Hivi kwa nini matamasha ya mwamaposa huwa hayana ulinzinwa kutosha? Ashajua ana waumini wengi basi akiwa anaandaa matamasha yake awe na plan nzuri ya ulinzi wa ndani na njee
Kazi ya ulinzi ni ya polisi chini ya wizara ya mambo ya ndani. Hata siku Simba na Yanga zinacheza usije taka hizo timu zije na walinzi wa mashabiki
 
LEO TUNAVUKA NA VYETU, Kama tayr Kuna watu wanaona kinachoendlea muda huu hapa nje basi ni bora wasisubiri kauli ya ma asrika wajiondokee warejee makwao
 
Kazi ya ulinzi ni ya polisi chini ya wizara ya mambo ya ndani. Hata siku Simba na Yanga zinacheza usije taka hizo timu zije na walinzi wa mashabiki
Anaepeleka maombi kwamba siku flan kuna tukio ulinzi uwepo ni nani km sio mwenye tukio
 
Nimewaza na kutafakari.. nimegundua ni shetani aliyebadilika na kuwa malaika wa nuru.. watu wanangamizwa
 
Matamasha mengi yanawekwa usiku harafu usalama hakuna kabisa miaka nenda miaka rudi hata mechi za usiku hapo kwa Mkapa sio salama ni vile wanaosimamia sheria hilo haliwahusu...
 
Anaepeleka maombi kwamba siku flan kuna tukio ulinzi uwepo ni nani km sio mwenye tukio
Unadhani hajapeleka maombi. Kibali amepewa na nani kwani, mpaka wanatoa kibali kufanya mkusanyiko wa maelfu usiku ujue washapanga suala la ulinzi. Huu ni uzembe wa polisi mtumishi asisingiziwe hata kama sijui anatapeli watu
 
Back
Top Bottom