GE2025 Polisi: Tumewakamata Watu 10 Kibaha wakiwa wanaandaa njama za Uhalifu

GE2025 Polisi: Tumewakamata Watu 10 Kibaha wakiwa wanaandaa njama za Uhalifu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Jeshi la Polisi Tanzania lipo kwa mujibu wa sheria mama yaani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 147. Moja ya majukumu yake kwa mujibu wa sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi sura ya 322 kifungu cha 5 (1) ni Kulinda maisha ya watu na mali zao pamoja na Kubaini na kuzuia uhalifu.

Katika kutekeleza jukumu la kubaini na Kuzuia uhalifu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani tarehe 16/08/2025 lilipata taarifa za uwepo wa watu katika Ukumbi wa Mwitongo huko Mailimoja Shule, Wilaya ya Kibaha wanapanga njama za kufanya uhalifu.

Mara baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi lilichukua hatua za kufika eneo hilo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 10 waliofahamika kwa majina kama ifuatavyo:-

1. Upendo Winni Msechu, Anayeishi KCMC, Moshi

2. Upendo Parsons Mwalushwa, Anayeishi Mbezi, Dar Es Salaam

3. Pendo Raphael Mwasomola, Anayeishi Nzovwe, Mbeya

4. Focus Laurent Kasaka, Anayeishi Kisesa, Mwanza

5. Furaha Noel Mbise, Anayeishi Ubungo, Dar Es Salaam

6. Mzambia Amon Kabuje, Anayeishi Kijenge, Arusha

7. Mkombozi Emmanuel Hatibu, Anayeishi, Maili moja, Kibaha

8. Samson William Rabani, Anayeishi, Tangini, Kibaha

9. Abdallah Adam Mazengo, Anayeishi Mwanama, Arusha

10. Harouna Shanang Zangina, Anayeishi Goba, Dar Es Salaam

Jeshi la Polisi linaendelea kuwahoji kwa kina watuhumiwa hao na mara baada ya upelelezi hatua nyingine za kisheria zitafuata.

Imetolewa na:-
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Pwani.
View attachment 3444502View attachment 3444503
Chaumwa sii wahalifu,chaubwabwa sii wahalifu,Manyasi kijani sii wahalifu,na washirika wenu wa mchongo,ila Wazalendo wa taifa hili kwenu ni wahalifu aibu yenu kwa kuliangamiza taifa hili.
 
Kutoa taarifa ni muhimu isije kusemekana wametekwa.

Hongereni sana Polisi Tanzania kwa kazi nzuri ya KUBAINI, KUZUIA na KUPAMBANA na uhalifu. Sio wengi wanaweza kuelewa mnachofanya.
 
Reforms zinaitajika huko Mbeleni 2090 watakuja kuchapana maana Vyama vingi wameanza watu kuvistukia atakuja mtu hana chama ataanzisha yale Misri na Tunisia hata Mama tu Tuna bado nafasi ya kujisahihisha
Kama Mungu angekuwa anatusukiliza basi angelimrudisha Mwl.Nyerere aje tumwulize kwa nini aliruhusu mfumo wa vyama vingi jambo linalotugawa tu na kudharirisha watanzania.Leo kwa sababu ya vyama vya siasa kuna watanzania daraja A,B na C.

Nadhani kabla ya kuruhusu vyama vingi tulipaswa kujadiliana kwanza namna bora ya kuvitenga vyombo vya dola na siasa.

Leo Tanzania ni ngumu kujua jeshi letu la polisi au usalama wanamtii nani serikali au vyama vya siasa.Kama vinaitii serikali basi angalau tungeona usawa kwenye vyama na vyombo vya dola vingekuwa na jicho la kuwa observer tu bila kuwa sehemu ya siasa.
Ij
 
Kwa namna umeanza kujielezea inaonyesha wewe na jeshi lako mlikuwa mnafanya uhalifu kwa kuvamia raia ambao walikuwa busy na ratiba zao.

Hii inchi sasa ilipofikia ni sawa sawa na enzi za utawala wa mkoloni maana ilikuwa si ruhusa raia kukaa na kujadili mambo yao ya kitaifa bila kuingiliwa.

Hii nitabia mbaya na matumizi mabaya ya mamlaka ya kiserikali.

Kwann muwakamate watu bila kuwa na motive yoyote?

Sio vizuri.
 
watu wanapotekwa na kupoteza maisha wala hawanukuu sheria ya kuanzishwa jeshi la polisi ila linapokuja suala la vyama vya upinzani visivyo washirika wa ccm ndiyo uhuni kama huu unafanyika.
 
Waliokamatwa ni viongozi wa CHADEMA walikua kwenye kikao Cha Ndani Cha chama.


Sasa Hawa Polisi simewazoea ?? Ngoja tumalize Maombi kwanza.
 
Mimi sijawahi kuichukulia tanzania kama nchi ya vyama vingi
 
Back
Top Bottom