Polisi: Tunachunguza tukio la Juma Elisha kuchukuliwa na watu wasiojulikana

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU KUTOONEKANA KWA ELISHA JUMA HASSAN
​
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linachunguza na kufuatilia kwa karibu tukio la mtu anayedaiwa kuchukuliwa na watu ambao hawajafahamika anayejulikana kwa jina la Elisha Juma, mkazi wa Mtaa wa Kadisi, Kata ya Katente, Tarafa ya Ushirombo, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita, ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili.

Taarifa ya tukio hilo zimefikishwa leo Agosti 21, 2025 majira ya saa 7:40 mchana katika Kituo cha Polisi Bukombe ikidaiwa kuwa Agosti 19, 2025 majira ya saa 10:00 jioni, Elisha Juma akiwa studio inayofahamika kwa jina la MAS J iliyopo Mtaa wa Kilimahewa, Kata ya Bulangwa alichukuliwa na watu watatu ambao hawakufahamika waliokuwa na gari yenye rangi nyeupe ambayo pia haikufahamika usajili wake na kuondoka naye kusikojulikana.

Aidha, wakati tukio hilo linatokea, watu wengine waliokuwepo katika studio na mazingira hayo hawakuweza kutoa taarifa sehemu yoyote mpaka zilipowasilishwa leo Kituo cha Polisi na baada ya kuwasilishwa, hatua za uchunguzi kuhusiana na tukio hilo zimeanza mara moja.

Tunatoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusiana na tukio lolote la uhalifu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa mara moja. Pia, tunaomba wananchi wawe watulivu wakati tukio hili linachunguzwa.

Vilevile kwa yeyote mwenye taarifa ya kuweza kusaidia kupatikana kwa Elisha Juma Hassan asisite kuziwasilisha ili zifanyiwe kazi.

Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Geita

Polisi.jpg
 
Nchi ngumu sana.polisi acheni drama nyny mnawafahamu wanaoteka na wote wanaotekwa ni wapinzani.sasa mtekaji hapo hafahamiki.JAMANI SISI CYO WATOTO JAMANI TUMECHOKA NA KAULI ZENU BORA MKAE KIMYA
 
Hapo sidhani kama kuna maswali mengine tena.
Hawa watu bila shaka wamedhamiria kuwamaliza watu wote wanaopinga utawala wa huyu mama! Hili jambo ni la hatari sana iwapo wananchi wataamua kujitetea au kujibu mashambulizi.
 
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU KUTOONEKANA KWA ELISHA JUMA HASSAN
​
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linachunguza na kufuatilia kwa karibu tukio la mtu anayedaiwa kuchukuliwa na watu ambao hawajafahamika anayejulikana kwa jina la Elisha Juma, mkazi wa Mtaa wa Kadisi, Kata ya Katente, Tarafa ya Ushirombo, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita, ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili.

Taarifa ya tukio hilo zimefikishwa leo Agosti 21, 2025 majira ya saa 7:40 mchana katika Kituo cha Polisi Bukombe ikidaiwa kuwa Agosti 19, 2025 majira ya saa 10:00 jioni, Elisha Juma akiwa studio inayofahamika kwa jina la MAS J iliyopo Mtaa wa Kilimahewa, Kata ya Bulangwa alichukuliwa na watu watatu ambao hawakufahamika waliokuwa na gari yenye rangi nyeupe ambayo pia haikufahamika usajili wake na kuondoka naye kusikojulikana.

Aidha, wakati tukio hilo linatokea, watu wengine waliokuwepo katika studio na mazingira hayo hawakuweza kutoa taarifa sehemu yoyote mpaka zilipowasilishwa leo Kituo cha Polisi na baada ya kuwasilishwa, hatua za uchunguzi kuhusiana na tukio hilo zimeanza mara moja.

Tunatoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusiana na tukio lolote la uhalifu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa mara moja. Pia, tunaomba wananchi wawe watulivu wakati tukio hili linachunguzwa.

Vilevile kwa yeyote mwenye taarifa ya kuweza kusaidia kupatikana kwa Elisha Juma Hassan asisite kuziwasilisha ili zifanyiwe kazi.

Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Geita

View attachment 3448413
Wenzako wamenawa mikono ili waanze kula, halafu unataka kuwashika mikono, shauri zenu, hawatanii eti.

Huyu sasa wamefika wangapi tangu 2021 Hadi leo 2025,, compared to 2015 - 2020. ????
 
Hawa watu bila shaka wamedhamiria kuwamaliza watu wote wanaopinga utawala wa huyu mama! Hili jambo ni la hatari sana iwapo wananchi wataamua kujitetea au kujibu mashambulizi.
Naamini vyombo vya ulinzi na usalama havitafanya kosa la kuruhusu mioyo ya raia ivikatie tamaa na kuamua kujilinda wenyewe. Polisi
Watabadilika kabla ya critical point ya uvumilivu. Ila kama wamekududia uharibifu wataruhusu ifike beyond control zone ili malengo yao ya uharibifu yatimie.
 
Back
Top Bottom