Polisi: Tunamhoji Peter Madeleka kwa Tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu

Polisi: Tunamhoji Peter Madeleka kwa Tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema kuwa tarehe 14 Agosti 2026, saa 9:30 alasiri, eneo la Mikocheni B, Kinondoni, limemkamata na linamhoji Peter Madeleka kwa tuhuma za kudharau amri za Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu kama “Mahakama ya Mafisadi.”

Kwa mujibu wa Jeshi hilo, amri hizo zilitolewa na Mahakama tarehe 27 Julai 2026 na tarehe 13 Agosti 2026.

Soma > Malisa: Wakili Madeleka amekamatwa na watu waliojitambulisha ni polisi

Jeshi la Polisi limesema taratibu za kisheria zinaendelea kutekelezwa ili kumfikisha Madeleka kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa hatua zaidi.

Alichosema Wakili Madeleka kabla ya kukamatwa > Madeleka: Si kosa wakili kuongea na wanahabari mahakamani

IMG_0350.jpeg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo tarehe 14 Agosti, 2026, saa 9.30 alasiri, limemkamata Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka, akiwa katika eneo la Mikocheni B, Kinondoni. Madeleka amekamatwa akiwa katika viunga vya Mahakama ya Uhujumu Uchumi (maarufu kama Mahakama ya Mafisadi) wakati akitekeleza majukumu yake ya kitaaluma.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, Madeleka anashikiliwa na kuhojiwa kwa tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi iliyotolewa tarehe 27 Julai, 2026 na tarehe 13 Agosti, 2026.

“Lilimkamata na linamuhoji Peter Madeleka, kwa tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi “Mahakama ya Mafisadi” iliyotolewa tarehe 27 Julai, 2026 na 13 Agosti, 2026. Taratibu za kisheria zinatekelezwa ili kumfikisha kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa hatua zaidi”, imeeleza polisi.

Kukamatwa huku kumetokea saa chache baada ya Wakili Madeleka kufanya mkutano na waandishi wa habari akitangaza nia yake ya kufungua kesi kupinga zuio la Msajili wa Mahakama Kuu linalowazuia mawakili kufanya mahojiano na vyombo vya habari mahakamani. Taarifa za awali kutoka kwa Wakili Gideon Mathew zilieleza kuwa wakati wa ukamataji huo, watu waliojitambulisha kama polisi walichukua pia gari la Madeleka, fedha, na nyaraka mbalimbali alizokuwa nazo.

Aidha, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilieleza kupokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kikitoa wito kwa mawakili waliopo Dar es Salaam na maeneo ya jirani kufika Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) ili kutoa msaada wa kisheria na kuhakikisha Wakili Madeleka anapata usaidizi unaostahili

“Chama cha Wanasheria Tanganyika kinaendelea kusimamia na kutetea haki, utu na uhuru wa mawakili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kitaaluma kwa mujibu wa sheria,” imeeleza taarifa ya TLS iliyotolewa na Baraza la Uongozi.
 
Kama wakili kakamatwa na analala mahabusu siku tatu Yani Leo ijumaa,kesho jumamosi na jumapili aiseeee sishangai Mimi wale mapolisi wa Central mbeya Ile jirani na rufaa walinikamata nikalala wiki nzima tena nikanyimwa mawasiliano nisiwasiliane na ndugu zangu mixer kichapo
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema kuwa tarehe 14 Agosti 2026, saa 9:30 alasiri, eneo la Mikocheni B, Kinondoni, limemkamata na linamhoji Peter Madeleka kwa tuhuma za kudharau amri za Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu kama “Mahakama ya Mafisadi.”

Kwa mujibu wa Jeshi hilo, amri hizo zilitolewa na Mahakama tarehe 27 Julai 2026 na tarehe 13 Agosti 2026.

Soma > Malisa: Wakili Madeleka amekamatwa na watu waliojitambulisha ni polisi

Jeshi la Polisi limesema taratibu za kisheria zinaendelea kutekelezwa ili kumfikisha Madeleka kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa hatua zaidi.

Alichosema Wakili Madeleka kabla ya kukamatwa > Madeleka: Si kosa wakili kuongea na wanahabari mahakamani

View attachment 3650444
Mbona Katugwa na wenzake hajawakamata kwa kudharau amari ya mahakama kuu ya kushindwa kuleta mashahidi kama walivyo amriwa zaidi ya mara tatu sasa.
 
Back
Top Bottom