Polisi: Tunamhoji Peter Madeleka kwa Tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu

Polisi: Tunamhoji Peter Madeleka kwa Tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu

Mbona Katugwa na wenzake hajawakamata kwa kudharau amari ya mahakama kuu ya kushindwa kuleta mashahidi kama walivyo amriwa zaidi ya mara tatu sasa.
Jaji kaajiriwa na serikali
Wakili wa serikali
Wote wanalipwa na serikali
Hivyo wakiomba airisho lazima wapewe ila wewe kajamba nani sema hujaleta shahidi na uombe airisho uonee
 
Kama wakili kakamatwa na analala mahabusu siku tatu Yani Leo ijumaa,kesho jumamosi na jumapili aiseeee sishangai Mimi wale mapolisi wa Central mbeya Ile jirani na rufaa walinikamata nikalala wiki nzima tena nikanyimwa mawasiliano nisiwasiliane na ndugu zangu mixer kichapo
Utakua wapi Leo tupooze machungu kwa ugimbi mkuu!?
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema kuwa tarehe 14 Agosti 2026, saa 9:30 alasiri, eneo la Mikocheni B, Kinondoni, limemkamata na linamhoji Peter Madeleka kwa tuhuma za kudharau amri za Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu kama “Mahakama ya Mafisadi.”

Kwa mujibu wa Jeshi hilo, amri hizo zilitolewa na Mahakama tarehe 27 Julai 2026 na tarehe 13 Agosti 2026.

Soma > Malisa: Wakili Madeleka amekamatwa na watu waliojitambulisha ni polisi

Jeshi la Polisi limesema taratibu za kisheria zinaendelea kutekelezwa ili kumfikisha Madeleka kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa hatua zaidi.

Alichosema Wakili Madeleka kabla ya kukamatwa > Madeleka: Si kosa wakili kuongea na wanahabari mahakamani

View attachment 3650444
Polisi inamhoji mtu kwa kudharau mahakama?

Hivi polisi ni taaluma ya wapumbavu kiwango hiki?
 
Inatakiwa MAHAKAMA ndio itoe AMRI
Amri ikitoka MTEKELEZAJI ni polisi

Mfano
Mahakama yatoa Amri fulani afikishwe mahakani…..
Mahakama yatoa Amri mali za fulani zitaifishwe

Kwa jinsi habari ilivyo inaonekana ni kama Madereka kafanya kosa la JINAI na polisi wamemkamata wanafanya uchunguzi ili kumpeleka mahakamani

Mahakama ikitoa AMRI kazi ya polisi huwa ni kumkamata na kumpeleka mahakani direct
Asante kwa majibu mazuri ya kitaalamu.

Kupitia jibu lako tunaweza kusema Polisi wamekurupuka kama kawaida yao.
 
Polisi inamhoji mtu kwa kudharau mahakama?

Hivi polisi ni taaluma ya wapumbavu kiwango hiki?
Ukiwa askari polisi unatumia akili za mkubwa wako wa kazi. Ni marufuku kutumia profeshenolism
 
Ukiwa askari polisi unatumia akili za mkubwa wako wa kazi. Ni marufuku kutumia profeshenolism
Justifiable and reasonable actions.

Kila sheria ina exceptions zake, sembuse amri?

Wanajikusanyia laana
 
Justifiable and reasonable actions.

Kila sheria ina exceptions zake, sembuse amri?

Wanajikusanyia laana
Nafikiri kwenye mafunzo yao kuna vitu wanalishwa vinavyowaondolea uwezo wa kawaida wa kutenda na kufikiri kama binadamu wa kawaida.
 
Kwani Polisi waliagizwa wamhoji au wamkamate wampeleke Mahakamani kujjibu tuhuma? Why wanafanya kinyume?
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema kuwa tarehe 14 Agosti 2026, saa 9:30 alasiri, eneo la Mikocheni B, Kinondoni, limemkamata na linamhoji Peter Madeleka kwa tuhuma za kudharau amri za Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu kama “Mahakama ya Mafisadi.”

Kwa mujibu wa Jeshi hilo, amri hizo zilitolewa na Mahakama tarehe 27 Julai 2026 na tarehe 13 Agosti 2026.

Soma > Malisa: Wakili Madeleka amekamatwa na watu waliojitambulisha ni polisi

Jeshi la Polisi limesema taratibu za kisheria zinaendelea kutekelezwa ili kumfikisha Madeleka kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa hatua zaidi.

Alichosema Wakili Madeleka kabla ya kukamatwa > Madeleka: Si kosa wakili kuongea na wanahabari mahakamani

View attachment 3650444
Ivii

Mbona tuna watu WAJINGA WAJINGA NAMNA HII IVII

MADEREKA KAONGEA BAYA GANIII??!
 
Mbona Katugwa na wenzake hajawakamata kwa kudharau amari ya mahakama kuu ya kushindwa kuleta mashahidi kama walivyo amriwa zaidi ya mara tatu sasa.
Kuna ma askari walipiga watu na kuwavunja miguu na mikono mbele ya mahakama na hawakufanywa kitu.

NB. Mahakama za kidunia kwenye utoaji haki ziliaminikaga... Kwa Sasa mahakama ya TANZANIA NI KAMA TOILET PAPER 🗞️

UNAITUMIA KUFUTIA KINYESI NA KUITUPA.. MAANA JAJI, HAKIMU NI MAKADA WA CCM

BPP NAE NI KADA WA CHAMA CHA MAPINDUZII UTAMSIKIA DPP ANASEMA MAMA ANAUPIGA MWINGI

HUWEZI PATA HAKI KWENYE MAHAKAMA YA FISI KONDOO HAWAWEZI KUPEWA HAKI
 
Wamemkamata mtu mahakamani kwa kosa la kuzarau mahakama ivyo anahojiwa ili apelekwe mahakaman (patamu apo)
Mkuu kuieweka vizuri zaidi sentensi yako ni,

Wamemkamata afisa wa mahakama mahakamani kwa kosa la kuizarau mahakama ivyo anahojiwa ili apelekwe mahakamani kwa kuwa kafanya kazi yake ya kimahakama.
 
Back
Top Bottom