Polisi: Tunamhoji Peter Madeleka kwa Tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu

Hao wahuni wa policcm wasichojua ni kuwa Mawakili wa Mahakama Kuu ni Maafisa wa Mahakama na Wana wajibu wa msingi wa kuisaidia mahakama kutenda haki na kusimamia sheria, na ndicho alichofanya Wakili msomi Peter Madeleka kupitia Tamko lake..
 
Hivi hawa jamaa hawajifunzi mpaka sasa ?Polisi hawa
 
Wamemkamata Ijumaa baada ya saa za kazi ili akae ndani mpaka Monday
 
This is too much now, Mbaka sasa tuna asilimia 52% tupo kwenye dictectorship country
 
Polisi wamekua mahakama wanamhoji kwa kauli alizokua anatoa wiki kadhaa zilizopita ukidharau mahakama wao ndio wanakuhumu pale pale sio jinai hiyo..
Wamezunguka mlango wa nyuma kwenye kitu kinachojulikana wamechukua gari nalo lina kosa gani..
 
Basi wengi hatujui tunawkamatwa Ijumaa tunashikiliwa mpaka Jumatatu kwa kisingizio kuwa weekend haruhusiwi kutoka mtu
Watanzania wengi hawana hiyoelimu, na polis wanatumia huo mwanya kuwakomoa

Elimu hiyo ingekuwa inatolewa tokea shule za msingi ingesaidia sana watanzania
 
Mtu anapokiuka maagizo au amri ya mahakama, chombo kipi kina wajibu wa kumshurutisha mhusika kutii amri ya mahakama?
Inatakiwa MAHAKAMA ndio itoe AMRI
Amri ikitoka MTEKELEZAJI ni polisi

Mfano
Mahakama yatoa Amri fulani afikishwe mahakani…..
Mahakama yatoa Amri mali za fulani zitaifishwe

Kwa jinsi habari ilivyo inaonekana ni kama Madereka kafanya kosa la JINAI na polisi wamemkamata wanafanya uchunguzi ili kumpeleka mahakamani

Mahakama ikitoa AMRI kazi ya polisi huwa ni kumkamata na kumpeleka mahakani direct
 
Hapa kuna kuchanganya mambo, wakili madeleka ni afisa wa mahakama kisheria, sasa ugomvi wa tafsiri ya sheria au kanuni za mahama na afisa wa mahakama polisi anaingiaje?
 
Polisi hawana cha kujifunza mtu ni public figure, ajaua wala nini, kumpelekea barua tu ya wito inatosha, sasa hadi inafikia mnaleta taharuki na taswira mbaya kila siku ya kunyakua watu kama kuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…