Polisi: Tunamhoji Peter Madeleka kwa Tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu

Polisi inamhoji mtu kwa kudharau mahakama?

Hivi polisi ni taaluma ya wapumbavu kiwango hiki?
Kazi yao ni kupokea order za CCM, hayafikirii tena jeshi limejaa wapumbavu watupu, kuteka,kuua, kuiba chaguzi na kesi fake ndio majukumu yao sasa
 
Ulifanya nini mpaka ukakaa siku zote hizo pale Central na kipigo juu mkuu?
 
No one is safe
 
Ivi mfano ukikataa kukamatwa kwakuwa hujaelezwa kosa lako au ukakataa kwakuwa waliokuja kukukamata hawajafuata taratibu, utakuwa umefanya kosa?

Na huwa najiuliza kama umekamatwa na ukapigwa alafu ukawa hujafanya kosa kuna fidia yoyote huwa inatoka?

Na mpaka umekamatwa inamaana si uchunguzi unakuwa uko tayari kuwa unakosa? maana mtu akisema umeua kwa mfano na ukawekwa ndani labda mwezi au miezi na vitu vyako vyote huko nje vikaharibika na kesi ikawa sio kweli ukaachiwa huwa kuna utaratibu wowote huwa unachukuliwa?

Msaada hapo wa majibu maana huwa nakuwaga na maswali ambayo nakosaga majibu huenda kuna siku majibu yake yanaweza kuja nisaidia.
 
Kama wanadhani ana makosa ya kisheria ambazo amezivunja, basi wampeleke mahakamani, waache kutupigia kelele zisokuwa na msingi. Mapolisi ni majitu yenye akili za kitutusa.
 
Binafsi nitasema ni uonevu wa polish kama ilivyozoeleka ni kawaida yao kwa wenye mawazo ya kuikosoa CCM na sirikali iliyoundwa nao.
 
Sasa huyu madeleka si ni kijana wao!...mwenzao!, mtu wa mfumo...wanamuhoji nini sasa!...kipepeo mweusi!


Wanatuona sisi ng'ombe eti!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…