Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Kuna taarifa zinazotengenezwa na kusambazwa katika makundi sogozi yenye nia ya kudanganya ili kuleta taharuki kwa umma kumhusu Franco Kashaija Ruhinda kuwa haijulikani alipo toka alipowasili nchini akitokea Dubai.
Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa Franco Kashaija Ruhinda alikamatwa alipowasili nchini Novemba 3,2024 kwa tuhuma za kujihusisha na Uhalifu wa kupanga na bado anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi ili kukamilisha yaliyokuwa yamesalia katika uchunguzi ili hatua zingine za kisheria zifuate.
Imetolewa na:
David A. Misime - DCP Msemaji wa Jeshi la Polisi Dodoma, Tanzania.