DOKEZO Polisi tunaomba msaada. Tunahisi dada yetu ameuawa na mume wake ambaye ni Polisi, inasikitisha sana!

DOKEZO Polisi tunaomba msaada. Tunahisi dada yetu ameuawa na mume wake ambaye ni Polisi, inasikitisha sana!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kutoka kwenye mtandao wa X, Akaunti ya Lisa Ildephonce (@LIldephoce)

“Tarehe 23/1/2023 Tulipata msiba wa dada angu alifariki katika mazingira ya kutatanisha aliolewa na kijana anaitwa Josephat Aron ambaye ni Police pale Ufundi (Kilwa Road) cheo Kopro

Kifo chake kilitupa mashaka kutokana na mgogoro wa ndoa waliokuwa nao na sababu hiyo hatujui mpaka leo hii dada yetu amekufa na tatizo gani kwani baada ya kufariki kijana huyo alitunyima kupima mwili pamoja na taarifa za hosptal juu ya kilichomuua dada yetu

Imefika hatua familia ya marehemu wanatishiwa na hawana amani

Siku ya kumuaga marehemu mdogo wa kike wa marehemu alinyimwa kwenda kumstiri dada yake badala yake alienda mume na kaka ake kumstiri dada yetu ndugu tulichukizwa na iko kitendo cha shemeji mtu kwenda kumstiri marehemu tukaingilia kati hilo mwisho wa siku wakamruhusu mdogo mtu kuingia lakini haikusaidia kwani mume na shemeji wa marehemu walikuwa wameshatangulia

Baada ya kuruhusiwa mdogo wa marehemu na mama zake wadogo wawili walinyimwa gloves kwaajili ya kumvalisha marehemu na walikuta dada yetu amezuriwa maeneo mengi

Ndugu wa mwanamke waliokuwa hospitalini walikatazwa kumuona mgonjwa aliyekuwa anaingia ni Josephat na ndugu yake anaitwa Mwinyi walimuamisha mochwari kutoka hospital alipofia (Hindu Mandal)na kumpeleka mochwari ya kazini kwao anapofanyia kazi ndugu wasiweze kupima mwili

View attachment 2860643
View attachment 2860644

View attachment 2860794
Hii ni siku ya msiba [Video] baada ya ndugu wa mwanamke kutaka mwili ukafanyiwe vipimo ili kujua ndugu yetu kwa nini amepatwa na kifo ila tukaletewa mapolisi waliokuja na mwili wakashika na mabunduki kutaka kuyafwatua baada ya wananchi waliokuja msibani kuwaambia tuuweni tu kama hamtaki tumpime ndugu yetu. Kijana huyo Josephat Aron akaamuru Polisi waingie ndani ya gari. Tulimzika ndugu yetu chini ya ulinzi wa mapolisi waliotoka Dar es Salaam kuja Rombo na mwili tukiwa na majonzi”
Camilius Wambura amekuwa anaongoza kwa mkono wa damu.
Wa chini yake wanaiahi kama bosi wao.

Mama anaendelea kufurahia utendani wa kikaburu wa mapolisi
 
Kama mshazika huyo chezeni nae makida tu. Binafsi ningehakikisha anabaki bila miguu wala mikono ili ajifunze.
 
Mmekua wazembe Sana
Sijui ni umasikini, ujinga au woga uliokithiri maana mngekua hata na chembe ya ujasir wakususia mazishi Hadi mwili ufanyiwe uchunguzi
 
Hiyo tarehe 23/01/23 ni sahihi kweli? Kama ni sahihi kweli siku zote hizo zaidi ya mwaka mzima walikuwa wapi hao ndugu wasipiganie haki ya marehemu ndugu yao? Ngoja niishiie hapa maana kwangu bado haiingi akili labda mleta habari atakuwa kakosea tarehe.
 
Unaleta umbea Tu usiokuwa na mashiko.

Vifo vyote vyenye utata ndugu hawawezi kuruhusu kuzikwa mpaka ifanyike postmortem itakayoshirikisha Wana ndugu.

Marehemu she is dead and buried, unataka JF tuanze kujadili umbea na illusions?

Pambana na January usirudishe muda nyuma.
Wewe utakuwa police
 
Back
Top Bottom