LGE2024 Polisi: Tusiwape nafasi wanaotaka kuvuruga amani ya Uchaguzi wa kesho Novemba 27, 2024

LGE2024 Polisi: Tusiwape nafasi wanaotaka kuvuruga amani ya Uchaguzi wa kesho Novemba 27, 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime amesema wamejipanga kudumisha amani na utulivu kesho katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, huku likitahadharisha wanaotaka kuuvuruga.

Misime amesema hayo leo Jumanne Novemba 26, 2024 kupitia video fupi iliyopakiwa katika mitandao ya kijamii ya jeshi hilo.

“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa kila Mtanzania kuhakikisha anadumisha amani, utulivu, upendo na usalama kipindi chote cha kupiga kura, kuhesabu kura, kutangaza matokeo na baada ya uchaguzi na kamwe usiwe chanzo cha uvunjifu wa amani kwani hutaonewa muhali, lazima utachukuliwa hatua za kisheria.

“Kamwe tusiwape nafasi, wala kusikiliza au kufuata matamshi na vitendo vya viongozi au wafuasi wao ambavyo lengo lake ni kutaka kuvuruga amani, utulivu na usalama wa nchi yetu,”amesema Misime.

PIA SOMA
- LGE2024 - Katavi: Jeshi la Polisi lawaasa Waandishi wa Habari kuepuka kuandika habari za kichochezi kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa

- LGE2024 - Kagera: Polisi waahidi "usalama" siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
 
Polisi ndio chanzo cha vurugu nchini kwa kuilinda CCM na kuwaonea wapinzani haki upande mmoja.
 
Back
Top Bottom