Polisi VS Majambazi

Ki polisi neno "kurushiana risasi" lina tafsri pana kuliko huko uraiani linavyoeleweka.


Kwao jambazi au whichiever person ambaye analeta ukaidi au kuonekana sugu kwenye majalada ya polisi ni mtu hatari anapaswa kuthibitiwa kwa gharama zozote hata kuuwawa kama sio kuharibiwa vioungo vyake vya mwili hata ikwa "nyeti" macho, ubongo, nk....huo ndo usalama wa raia bana!.

Unategemea, polisi waseme, tumeaua tu jambazi halikuwa na silaha au kujibizana risasi???. Kaulize habari ya Kamanda Laurian Sanya kule Mbeya, Kamanda Chiko kule Kilimanjaro, Kamanda Tossi na Msika kwa Kagera nk. Vyeo vya Polisi haviji pasipo rekodi ya matukio ya kutoa roho za watu bana!.
 
kweli watanzania tumelogwa na alotuloga kafa so atuwezi pata tiba kwani uko nyuma majambazi yalikuwa yakiiba free usikii police walirushiana risasi kwani walikuwa wakifika baada ya dk 15 or 30 baada ya tukio na utakuja kusikia baada ya mawiki or miezi police wameua majambazi siku zinaenda mpaka ilipokujabainika kwamba waliokuwa wanauwawa si majambazi ni raia wema tukaanza kulalamika leo hii majambazi atakabla hayajafanya tukio police wameshawai na kushambuliana na police bado tunataka kuhoji kama ni majambazi kweli au la wewe unaeona wanafanya comedy ngoja tumwombe mwema uruhusiwe kwenda front utupe majibu.
ebu tubadilike bana aha
 
Hili suala hata mimi linanipa wasiwasi,majambazi wanafanya vibaya kuua watu,lakini polisi wasijisifie kuyaua majambazi kwani wanahalalisha sheria mkononi. Kama kuna uwezekano wa kuyakamata yakamatwe.

Utamkamata vp mtu ana risasi lazima nawe utumie risasi, wale wakikuwahi wanakuua wewe, tusipende kuwaweka katika risk askari wetu jamani
 
Nashukuru wote kwa michango yenu. Ila swali bado halijapata jibu.

Unapozungumzia swala la kujibizana kwa risasi hii inamaanisha ni mapambano ya kutetea uhai. La kushangaza na nielewavyo mimi kuwa jambazi kama jambazi ni mtu ambaye anakuwa amejiandaa vilivyo ili kutimiza azma yake.

Naomba nitoe mifano ya kujibizana risasi ambapo jambazi hakuuwawa, Kumbukeni tukio la ubungo junction, pale mapambano yalikuwa ni dhahiri ila jamaa hakuuwawa.

Haya matukio mengine kama ya Dodoma (last year) na Moshi (recently) yamenipa wasi wasi mpaka nikaona ni vyema tujue ukweli kuhusiana na visa hivi.

Inakuwaje jambazi anapigwa risasi ya kichwa katika majibizano au ina maana askari wanashabaha pasi mfano, au jambazi anapigwa risasi mgongoni. Jamani eeh, tutafute ukweli wa mambo
 

Hiyo mbona simpo kuna majambazi baada ya kuona mapambano yamekuwa makali huwa yanaamua kukimbia/kulala mbele pale ndipo polisi huyatungua kwa nyuma, hiyo possible kabisa wala haina shaka, na ujue hapo kulikuwa na resistance flani ya hatari ya kuuana hivi.
 

Kumbuka wale majambazi kutoka Kenya walivyouwawa maili sita moshi
 

Hadithi kutoka kwa majambazi wastaafu zinadai kwamba kuna masharti yaliyobarikiwa na polisi kwa majambazi. Iba lakini usiue. Toa taarifa unaenda kuiba wapi. Hakikisha kundi la kijambazi liwe na msimamo mmoja bila kuzikana mafao, tena polisi wapelekewe chao haraka.

Wanaendelea kusisitiza kwamba ndio maana hata kipiga sim kuita msaada wa mapolisi watajivutavuta kupitisha muda na baadaye wanakuja kwenye eneo la tukio wakiuliza maswali ya kiajabuajabu kutimiza wajibu tu, wakati huo tayari wanakuwa wameambiwa na majambazi wamevuna nin na watarajie nini mafao yao. Utaambiwa ukaandikishe polisi. Maelezo yako ya kipolisi yanawasaidia polisi to verify kama kweli mafao waliyoambiwa watapata ni "haki" au la.

Ikitokea hawana habari na tukio la ujambazi linalotarajiwa sehemu husika wanapenda kuwahi haraka wajue nani kaingia kwenye anga zao bila kibali. Wakiwatambua au majambazi yakijieleza kutoa taarifa kituo kingine basi mapolisi wanathibitisha hilo halafu mchezo unaisha. Ndio maana utasikia majambazi yamekamatwa na kesho unayakuta mtaani huru.

Wakati mwingine wanafanyiziana tu, kama siku za nyuma hawakutimiziana chao basi wanategesheana. Safari hii wwanbishana wee, kisipoeleweka wanatumana, ndio unasikia majambazi yameuawa. Majambazi nayo yakishituka yanawatuma wenzao ambao ndio wanaenda kuuliwa na yenyewe yanabaki huru.

ANgalia ukitoa taarifa za kiuhalu polisi inategemea taarifa hiyo imemkuta nani, wakati mwingine unatoa taarifa, wanakuuliza wewe uko wapi, wanpata maelezo yako na kuwajulisha majambazi ambao wnakushughulikia ipasavyo. Wapo polisi serious, sio woteni wahalifu. Lakini kumjua polisi serious sio kazi ndogo, saa nyingine wanajuana utakuta wananyoosheana vidole, wachapa kazi wazuri wanafanyiwa kila hila ili wakosee na watimuiwe au wauliwe.

Polisi wakati mwingine sio watu hawa. Hata wenyewe wanajua ukweli huo. Waliwahi kunifanyia hila hizo mimi mwenyewe nimewaogopa kiasi kwamba siamini polisi mpaka nimfahamu vizuri. Alikuja polisi mmoja kwenye kijiwe changu akitaka kupiga simu bure tena sio ya kikazi. Alipokataliwa akaahidi kabisa kwamba tutamtambua yeye ni nani sio muda mrefu. Kweli hatukukaa sana pakabomolewa na kuibiwa. Taarifa ilipopelekwa kituoni wala hawakuja kwenye eneo la tukio mpaka siku mbili baadaye walipofika na kusemasema kimzaha. Ati, 'Ah hawa wezi bwana, waliiba nini na nini? msijali, mkimhisi mtu tuambieni" ikaa ndio mwisho.

Majambazi hawawezi kufanya vitu vitu vyao kibudu. Wanajulikana na wanajuana, hata aina ya silaha wanazotumia zinajulikana. Ukisikia jambazi kauawa ujue kavunja mwiko wa mitandao inayowahusisha mapolisi. Mchapa kazi mwaminifu hadumu kwenye mapambano ya kipolisi na majambazi.

Leka
 

Hii mada tulishaiongelea sana mwaka jana rudi nyuma utaikuta
 
Hivi mkisikia police wameuliwa na majambazi mtafurahia eeh cause watakuwa wameshindwa kujihami?

hii mijambazi yenyewe inatuingilia usiku inatuua kikatili bila huruma ,inafanya mambo mengi ya kutisha
 

heh mshangao !
 
duh, Leka umenifumbua macho na hii hadithi ya majambazi wastaafu. Nimeishiwa nguvu kabisa. Kumbe basi hata hawa polisi baadhi yao ni majambazi!
 
duh, Leka umenifumbua macho na hii hadithi ya majambazi wastaafu. Nimeishiwa nguvu kabisa. Kumbe basi hata hawa polisi baadhi yao ni majambazi!

yaani mie nipegwa na mshangao
 
Kwa kweli kila tukio la kijambazi huwa linahusisha polisi.

Majambazi wengi huwa ni wale polisi waliofukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu, hivyo basi huwa wanaendeleza upolisi haramu mitaani na watu wanaouwawa kwa visingizio vya ujambazi ni raia wema kabisaa.

Tunaliomba jeshi la polisi liwe linatuwekea hadharani picha za wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wananchi tuwatambue.
 

Huko kwenye bold ni mashaka makuu!
 
polisi wanapewa mafunzo na wanajua namna ya kutumia silaha lkn majambazi waliowengi kwanza hawana elimu na hata utumiaji wa silaha ni kubahatisha kwahiyo ndio maana mara nyingi majambazi wanauliwa!
 

Kindergaten solution to transatlantic problems,
I am not suprised.
 
Lyatonga Augustine Mrema enzi zake alipitisha zoezi la uchaguzi wa majambazi, wakati majambazi yote yalipigiwa kura za maoni. Wakapatikana kibao, lakini ulishasikia mambo yaliishia wapi? Ikaonekana kumbe syndicate inahusisha majina makubwa kwelikweli, Lyatonga akatimua mbio kwenda kijijini kwake Moshi, akaagiza wanaotaka kujieleza kwa hiari wamfuate huko ndani ya siku saba. Yule ni msalama wa Taifa, alishajionea hatari mbele yake. Lakini wapi, akafanyiwa hilana kuteleza akajikuta yuko nje ya system yeye mwenyewe.

Vita yoyote ni lazima iwe ya pamoja, huwezi kuipiga vita peke yako ukafanikiwa. Siku zote mwenye haki huwa na maisha machungu mno, tena maisha yake yenyewe huwa mafupi sana. Kimsingi mwache aliyeshika mpini atawale maisha ya watu, lakini hataweza kutawala roho zao, maana hata ukimuua roho yake huipati, inaenda kwa aliyempatia roho hiyo.

Sasa mnashangaa kwamba polisi wanawajua majambazi, mbona hushangai wanaposema wamelikamata jambazi sugu? wameujuaje usugu wake? Nchi za wenzetu kadhaa ukimwona polisi unajisikia salama sana, lakini hapa kwetu omba Mungu ukutane na askari wa Jesh la Wananchi utakuwa salama zaidi. Kina Kova wanasubiri ripoti tu ambayo hupikwa vizuri kuwafurahisha, hali halisi wanakumbuka kidogo sana. Mbaya zaidi kina Mwema ambao wameingia upolisi kwa kuanzia vyeo viubwa na hawakupitia vyeo vya mitulinga vilivyojaa misions for survival.

Kuna mapolisi waliokata tamaa kabisa, maana amekuwa Private miaka 30 na hategemei kuachana nao angalau awe koplo. Wanajifanyia watakavyo tu. Nilifiwa na mamangu mzazi siku moja akiwa nyumbani, kiutaratibu ilikuwa niende kutoa taarifa polisi wanipe form fulani ili nikauhifadhi mwili wa kipenzi mama yangu wakati napata akili nisafirisheje katika ukapa huu. Kituoni polisi mmoja aliyeko zamu akasema, form hizo zimeisha, nenda kachukue taxi uende kituo kingine. Alikuwa anasema maneno hayo akiwa amekalia kigogo nje akiota jua asubuhi. Mwenzake aliposikia maelezo hayo akashituka, akamwambia mwenzake, nenda kaangalie pale juu bwana zimeishaje? Mtu amekwambia kafiwa na mamake unamwambia akodi taxi, ndio nini hiyo? Wala yule jamaa hakujali. Akaenda huyu aliyeshituka, akaniletea form na kunihoji ili kjaza form akaniuliza nafanya kazi wap, nilipomwambia anashusha pumzi, lo! pole bwana, watu wengine hawajui wanamhudumia nani wanafyatuka tu kichwani, halafu kesho tu ajikute anataka sana msaada wako wewe mwenyewe, ukisita wanalialiaaaa!

Nikamshukuru kuelewa hilo, na kwa nunisaidia pasipo kunifahamu kwanza. Polisi wengi wa Bongo sasa wanashindana na Mgambo wa Jiji kujikusania mafao yasiyo halali na hawako tayari kusaidia mkono mtupu. Wamebarikiwa sana polisi wenye roho za kimungu ndani yao.

Nilienda mahali pengine siku nyingine, jamaa mlevi aliigonga gari niliyokuwa naendesha, halafu akakimbia. Niliyekuwa naye akasoma namba za gari ile na tukaanza kumfukuzia. Tukamkuta kakwama mahali sababu ya mvua nyingi. Tukamblock na akashuka akibembeleza. Tukampeleka polisi na kumkuta polisi aliyechukua maelezo. Gari yake yule jamaa likabaki pale nasi tukaruhusiwa. Akaahidi jamaa atatengeneza gari aliyoigonga kesho yake. Nilipoenda kesho kweli tuliondoka kwenda kwa mafundi wakamtajia kiwango, akatuacha pale akidai anaenda Benki. Kumbe akapotea tangu saa nne mpaka saa kumi tuliposhiuka. Polisi aliyetuandikisha jana hakuwapo, kumbe kuna polisi wa kike mmoja aklikua anajuana na mwenye gari iliyogonga wakadanganya na kuchukuwa funguo wakampa akapotea na gari ambayo ndio ilikuwa dhamana.

Nilikuja juu sana. Wakaenda kurudisha gari, mwenye gari kumbe siye aliyegonga, alimwazimisha rafiki yake. Akaanza kunitukana at hakitoki hata senti moja, bima yangu italipa au twende mahakamani. Nikashangaa imekuwaje hatukuafikiana jana hivyo. Polisi mla njama naye akaanza kunitishia ati hapa ni lazima mahakamani. Nikasema jaza form naenda makao makubwa, akagundua baadaye kwamba alikuwa anaongea na mtu ani baada ya kunipa form yangu nami nikampigia ofisa mmoja kule walikonituma kunitishia, nikaondoka.Nilipofika nyumbani tu nikapigiwa simu tena kutoka pale ati wanaomba nikubali pesa kidogo za kuwalipa mafundi. Nikagoma nami kwamba yule bwana alikubaliana na mafundi, hakipungui kitu au naendelea mbele. Wakasemezana na kuniita nikachukue pesa zote. Yule mama polisi mla njama aliniangalia kwa jicho la hatari sanaa, akasema maneno mengi kujibaraguza. Ndio polisi wetu hao.

Ujambazi katika kila masuala ya wananchi wasiojua msaada zaidi. Ukionyesha kutoelewa taratibu za haki ndio ulie tu, utapachikwa makes yasiyokuwa yako mpaka ufe.

Leka
 
polisi wanapewa mafunzo na wanajua namna ya kutumia silaha lkn majambazi waliowengi kwanza hawana elimu na hata utumiaji wa silaha ni kubahatisha kwahiyo ndio maana mara nyingi majambazi wanauliwa!
Majambazi mengi huwa yanauliwa kwenye mapambano kwa sababu ya kuzidiwa nguvu ya ziada ya polisi, wananchi na hali ya mfadhaiko kuwa huenda mwisho mwao umefika, na katika kufadhaika huko hushindwa kufikiri upesi na kufanya maamuzi ya kukimbia hovyo ili kuokoa maisha yao. Na hapo ndipo huwa target nzuri ya Polisi. Lakini wengi wa majambazi wana elimu hiyo hiyo labda kama ya polisi na wakati mwingine huwa ni askari wastaafu.

Pia, ni ngumu kuyakamata majambazi kwenye mapambano ya kutupiana Risasi kwa kuwa idadi ya polisi wanaokabiliana nao inakuwa karibu sawa na majambazi.

Suala la msingi ili sheria ichukue mkondo wake na kuepusha wasio na hatia kuingia kwenye mkumbo wa kuuwawa ni kuongeza idadi ya askari polisi na vitendea kazi, ili kwenye matukio ya kupambana na majambazi waweze kuwa "out number" na kuweza kuwakamata wakiwa hai na kuwafikisha kwenye vyombo vingine vya sheria.

Hata wakati wa vita vile vya rifle, jeshi lenye askari wengi ndio lilifanikiwa kushinda vita!!

Serikali iongeze idadi ya askari polisi, iwapatie vitendea kazi na mafunzo ya kisasa ili kuweza kukabiliana na tishio hili la ujambazi kwa sisi Raia.
 

you are more than right, na tabia zetu za tanzania za visasi halafu twashangilia trigger happy police hatujui tulisemalo na effect yake.
 
Suala la msingi ili sheria ichukue mkondo wake na kuepusha wasio na hatia kuingia kwenye mkumbo wa kuuwawa

HAPA UMESEMA NA NDIO MSINGI WA THREAD HII


Hata wakati wa vita vile vya rifle, jeshi lenye askari wengi ndio lilifanikiwa kushinda vita!!

On the contrary jeshi linalotumia akili ndilo linaloshinda vita na si vinginevyo. Vivyo hivyo polisi wetu watumie akili na maarifa zaidi watafanikiwa


Serikali iongeze idadi ya askari polisi, iwapatie vitendea kazi na mafunzo ya kisasa ili kuweza kukabiliana na tishio hili la ujambazi kwa sisi Raia.

Hapo umena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…