Polisi VS Majambazi

Polisi VS Majambazi

Mkulu Ngambo Ngali,

Nilipozungumzia vita vya rifle, I was so specific. Kwenye vita vya rifle, risasi zikiisha, mnatumia singe (waijua singe weye?), na hapo ndipo wenye idadi kubwa ya wapiganaji huwa washindi. Na kipengele hiki ni somo la siku nzima katika mafunzo ya kijeshi kama ulipitia jeshini (JKT) lakini.

Ooooh nakumbuka kale kawimbo " ....singe mwana kalalila....."
 
Katika siku za karibuni kumekuwa na habari mbalimbali zikiripotiwa kuwa Polisi wamefanikiwa kuyaua Majambazi kadhaa katika matukio ambayo yalisababisha kurushiana risasi.

Jambo linalonishangaza ni kuwa,
"Je, kunakuwa na ni nani hasa anatakiwa kuthibitisha maelezo yanayotolewa na Polisi?"

"Hivi inakuwaje ni Majambazi tu ndio wanauwawa na sio Polisi katika matukio ya kurushiana risasi?"

Nawasilisha.

Nakupa mfano mdogo tu wewe ulivyokuwa unaiba kitu na mtu akakukamata au kukuona ni nani mwenye wasiwasi??? kwahiyo Jeshi letu linapambana kikamilifu ili kurinda raia wake sasa wewe unataka wafe na wewe watakulinda nani shuuuuuuuuuu waini tulia acha kukurupuka tu futa hoja yako
 
Suala la msingi ili sheria ichukue mkondo wake na kuepusha wasio na hatia kuingia kwenye mkumbo wa kuuwawa

HAPA UMESEMA NA NDIO MSINGI WA THREAD HII


Hata wakati wa vita vile vya rifle, jeshi lenye askari wengi ndio lilifanikiwa kushinda vita!!

On the contrary jeshi linalotumia akili ndilo linaloshinda vita na si vinginevyo. Vivyo hivyo polisi wetu watumie akili na maarifa zaidi watafanikiwa


Serikali iongeze idadi ya askari polisi, iwapatie vitendea kazi na mafunzo ya kisasa ili kuweza kukabiliana na tishio hili la ujambazi kwa sisi Raia.

Hapo umena

Tatizo kubwa hawa wanaoshiriki katika jeshi letu ni form IV failures na ndio watendaji wa kila siku (operations)



Nakupa mfano mdogo tu wewe ulivyokuwa unaiba kitu na mtu akakukamata au kukuona ni nani mwenye wasiwasi??? kwahiyo Jeshi letu linapambana kikamilifu ili kurinda raia wake sasa wewe unataka wafe na wewe watakulinda nani shuuuuuuuuuu waini tulia acha kukurupuka tu futa hoja yako

Nahisi wewe ni miongoni mwao. Kudadadeki, nitakufwata!
 
Hili suala hata mimi linanipa wasiwasi,majambazi wanafanya vibaya kuua watu,lakini polisi wasijisifie kuyaua majambazi kwani wanahalalisha sheria mkononi. Kama kuna uwezekano wa kuyakamata yakamatwe.

Hiyo ndio njia nzuri ya kumaliza kesi mapema na kihalali. Wauwawe wote mpak waishekabisa. ukipeleka kesi mahakamani ni usanii tupu. siku 2 3 unamuona jamaa kaachiwa alafu anrudia kazi yake ya ualifu. POLISI MALIZENI HUKO HUKO ILA MSIUE WASIO NA HATIA KAMA WALE WAFANYABIASHARA WA MADINI.
 
Mara nyingi yanapouwawa majambazi, deal inakuwa imeleak. Na aliyetoboa ni mmoja wapo au mtu wa karibu, kuwa leo tunafanya tukio fulani mahali fulani!
 
Majmbazi wanachosha jamani nyie acheni kabisa.
 
Mkulu Ngambo Ngali,

Nilipozungumzia vita vya rifle, I was so specific. Kwenye vita vya rifle, risasi zikiisha, mnatumia singe (waijua singe weye?), na hapo ndipo wenye idadi kubwa ya wapiganaji huwa washindi. Na kipengele hiki ni somo la siku nzima katika mafunzo ya kijeshi kama ulipitia jeshini (JKT) lakini.

Ooooh nakumbuka kale kawimbo " ....singe mwana kalalila....."

Ninaijua singe, nilifundishwa halikuwa somo la siku moja kama unavyotaka niamini. Nimeitumia singe na mimi kwa taarifa yako mimi ni decorated soldier.

jambazi anayetumia singe sio jambazi hata siku moja, jambazi yoyote anataka kuiba na kukimbia na sio kupigana kwenye tukio. Kwenye kupanga ujambazi kitu muhimu ni escape route ya kutoka salama na mali zao kwenye tukio la ujambazi na hivyo polisi wanahitaji kucounter kuziba escape route bila kuwauwa nadhani somo limeeleweka.

kuuwa sio lazima na hakuna tija kukamata ni lazima na kuna tija.
 
Nadhani mshkaji swali lake ni la kimsingi. Ni kwamba in most cases(mara nyingi) unakuta polisi ndo majambazi wenyewe....kwa mfano muulize Zombe na wafanyabiashara wake wa madini alivyowauwa na kuwapora na akashinda kesi kisanii na kifisadi.

Kinachotokea ni kuwa wakishakosa kuleta 10% mara baada ya kupiga issue, au ikitokea wamepiga kwa kigogo kimakosa, au polisi wamelaumiwa sana na vyombo vya habari, hapo ndipo baadhi yao hutolewa muhanga.

Kwa hiyo wanapoandaa kupiga kwa kuwa ni timu ileile, wanazungukana kimtindo, sasa wale wasiokuwa na upolisi halali ndo huwa matatani kwa hiyo wanapigwa shaba kwa mfano wakiwa ndo wanajiandaa pengine Buguruni, unakuta kama watano hivi wanauawa, halafu maiti zinapelekwa Amana Ilala ili kuzuga kuwa wanahitaji matibabu kwa watuhumiwa wa ujambazi ambao wako mahututi. Inakuwa confirmed kuwa wamekufa.

Taarifa ya habari sasa......Watuhumiwa wa Ujambazi watano wameuawa na polisi baada ya kurushiana risasi na polisi huko eneo la kimara baruti. Kamanda wa Polisi kanda maalumu amethibitisha tukio hilo..............

Lakini yako matukio mengine huwa hayatengenezwi na katika haya pande zote mbili huwa zinapata madhara. Majambazi, wengi wao wana mafunzo ya kijeshi kwa hiyo si rahisi watano wakauawa bila madhara hata kidogo kwa askari watatu waliopambana nao...ebo!!!!!!!!!!!!!!!!!!

<<Hapo angalau umetoa changamoto zinazoendana kwa kiasi fulani na matukio ya ujambazi!!!!!! Matukio mengi yanatengenezwa na askari( askari police, jeshi) Tukio kama halikutengenezwa utaona uwajibikaji wake unakuwa mkubwa sana, na hata ukifuatilia maafisa wengi wa ASKARI wametajirika kwa kutimia njia hizo hizo. Uko sasa mkubwa wala hkkosea kwa hoja yako>> Ni mawazo wala tstafutane!!!!!!!!!!111
 
Yote semeni ila uadilifu wa jeshi letu la Polisi unatia mashaka. Askari wengi kwa muda mrefu wamekuwa na mahusiana na majambazi na hilo linafahamika huku mitaani na viongozi wa Polisi wanalijua hilo ila wamenyamaza. Tukio la Ukerewe ni moja ya mifano hai. Mtayasikia mengi toka huko.
 
Polisi ni Proffessionals wa kutumia silaha unlike majambazi, ambao mostly hawana hata mahala pa kujaribishia silaha zao, ndio sababu wanashindwa kupambana na polisi. Hakuna jibu zaidi ya hilo.
Una uhakika
 
Back
Top Bottom