Katika siku za karibuni kumekuwa na habari mbalimbali zikiripotiwa kuwa Polisi wamefanikiwa kuyaua Majambazi kadhaa katika matukio ambayo yalisababisha kurushiana risasi.
Jambo linalonishangaza ni kuwa,
"Je, kunakuwa na ni nani hasa anatakiwa kuthibitisha maelezo yanayotolewa na Polisi?"
"Hivi inakuwaje ni Majambazi tu ndio wanauwawa na sio Polisi katika matukio ya kurushiana risasi?"
Nawasilisha.
Suala la msingi ili sheria ichukue mkondo wake na kuepusha wasio na hatia kuingia kwenye mkumbo wa kuuwawa
HAPA UMESEMA NA NDIO MSINGI WA THREAD HII
Hata wakati wa vita vile vya rifle, jeshi lenye askari wengi ndio lilifanikiwa kushinda vita!!
On the contrary jeshi linalotumia akili ndilo linaloshinda vita na si vinginevyo. Vivyo hivyo polisi wetu watumie akili na maarifa zaidi watafanikiwa
Serikali iongeze idadi ya askari polisi, iwapatie vitendea kazi na mafunzo ya kisasa ili kuweza kukabiliana na tishio hili la ujambazi kwa sisi Raia.
Hapo umena
Nakupa mfano mdogo tu wewe ulivyokuwa unaiba kitu na mtu akakukamata au kukuona ni nani mwenye wasiwasi??? kwahiyo Jeshi letu linapambana kikamilifu ili kurinda raia wake sasa wewe unataka wafe na wewe watakulinda nani shuuuuuuuuuu waini tulia acha kukurupuka tu futa hoja yako
Hili suala hata mimi linanipa wasiwasi,majambazi wanafanya vibaya kuua watu,lakini polisi wasijisifie kuyaua majambazi kwani wanahalalisha sheria mkononi. Kama kuna uwezekano wa kuyakamata yakamatwe.
Mkulu Ngambo Ngali,
Nilipozungumzia vita vya rifle, I was so specific. Kwenye vita vya rifle, risasi zikiisha, mnatumia singe (waijua singe weye?), na hapo ndipo wenye idadi kubwa ya wapiganaji huwa washindi. Na kipengele hiki ni somo la siku nzima katika mafunzo ya kijeshi kama ulipitia jeshini (JKT) lakini.
Ooooh nakumbuka kale kawimbo " ....singe mwana kalalila....."
Kindergaten solution to transatlantic problems,
I am not suprised.
Nadhani mshkaji swali lake ni la kimsingi. Ni kwamba in most cases(mara nyingi) unakuta polisi ndo majambazi wenyewe....kwa mfano muulize Zombe na wafanyabiashara wake wa madini alivyowauwa na kuwapora na akashinda kesi kisanii na kifisadi.
Kinachotokea ni kuwa wakishakosa kuleta 10% mara baada ya kupiga issue, au ikitokea wamepiga kwa kigogo kimakosa, au polisi wamelaumiwa sana na vyombo vya habari, hapo ndipo baadhi yao hutolewa muhanga.
Kwa hiyo wanapoandaa kupiga kwa kuwa ni timu ileile, wanazungukana kimtindo, sasa wale wasiokuwa na upolisi halali ndo huwa matatani kwa hiyo wanapigwa shaba kwa mfano wakiwa ndo wanajiandaa pengine Buguruni, unakuta kama watano hivi wanauawa, halafu maiti zinapelekwa Amana Ilala ili kuzuga kuwa wanahitaji matibabu kwa watuhumiwa wa ujambazi ambao wako mahututi. Inakuwa confirmed kuwa wamekufa.
Taarifa ya habari sasa......Watuhumiwa wa Ujambazi watano wameuawa na polisi baada ya kurushiana risasi na polisi huko eneo la kimara baruti. Kamanda wa Polisi kanda maalumu amethibitisha tukio hilo..............
Lakini yako matukio mengine huwa hayatengenezwi na katika haya pande zote mbili huwa zinapata madhara. Majambazi, wengi wao wana mafunzo ya kijeshi kwa hiyo si rahisi watano wakauawa bila madhara hata kidogo kwa askari watatu waliopambana nao...ebo!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Una uhakikaPolisi ni Proffessionals wa kutumia silaha unlike majambazi, ambao mostly hawana hata mahala pa kujaribishia silaha zao, ndio sababu wanashindwa kupambana na polisi. Hakuna jibu zaidi ya hilo.