Polisi wa barabarani na weledi wao.

Nimecheka Sana ,Polisi Ni janga Sana ,Ni sawa kwenda mahakamani ukiamini umeshtakiwa kwa wizi wa kuku ghafla unasomewa kesi ya uhujumu uchumi πŸ˜‚πŸ˜‚lazima uhamaki na usipo kuwa na wakili mkojo huo unakuja kugonga kwenye nunda ya sanawariπŸ˜‚..

Polisi na Mpwayungu Ni kitu kimoja, enewei ... Huku kwetu wanaacha geti halafu wanakwenda kukaa porini Kama Nyani..... Enewei katika Taasisi isiyopokea rushwa Tz Ni polisi Tu
 
Kwa maelezo yako hayo, unadhani hapo mtenda kosa kakosea lipi kati ya hayo mawili?

Shuleni hua tunaenda kufanya nini hasa?
Upo sahihi, ikiwa mtafikishana mahakamani itabidi askari aeleze ni kosa lipi kati ya hayo lilifanywa na huyo dereva. Ila sasa kurahisisha uelewa hebu angalia makosa yalivyoandikwa katika Police Form No. 101 (PF. 101) na hayo ndiyo yamehamishiwa katika POS hivyohivyo yalivyo. PF 101 inapatikana kwenye PGO
 

Attachments

  • FB_IMG_1677997718335.jpg
    108.2 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1677997673508.jpg
    77.2 KB · Views: 2

Duh hii hatari sana!
 
Kubambikia wanafanya sana. Kosa linaweza kuwa lipo kwenye system lakini hujalifanya na akakuandikia. Bahati mbaya hizi POS hazitoi nafasi ya kukataa kosa yaani ukiandikiwa maana yake ulipe au uende kulalamika kwa RTO ambako nako una nafasi ndogo ya kusaidiwa. Wakati wa kutumia fomu ya karatasi mtu ulikuwa na option ya kukataa kosa na ufikishwe mahakamani, sasa hivi hakuna na polisi hawataki kupelekana mahakamani, wanakulipua tu kosa ulipe faini.

Hapa panatakiwa kurekebishwa, maana walichofanya ni kuwa polisi wamekuwa juu ya sheria na wanafanya kazi ya mahakama kutia watu hatiani, kitu ambacho kisheria hakijakaa sawa.
 
Kuna siku jamaa alitaka kuniandika kisa mtoto wa miezi-11 hajafunga mkanda, nikamwambia MFUNGE MKANDA ukimtosha niandikie
 
Kitu kingine ambacho kina shida ni uelewa wa alama za barabara na namna ya kutafsiri.

Kuna siku nilikuwa Mbeya, tulisimama getini pa shule ya Aggrey kumshusha mwanafunzi, mita 100 mbele askari akatusimamisha na kutuambia kuwa tumevunja sheria ya barabara kwa kusimama mahali pasiporuhusiwa. Tukamuuliza akama ya kutuzuia kusimama iko wapi, akatuonesha upande wa pili wa barabara (uelekeo wa uyole kwenda mbeya mjini) kuna alama imechorwa kienyeji (ni kama temporary sign). Kibao kimechorwa basi halafu kuna ile alama ya kulikata katikati, tulimwambia sasa sisi tunatoka mjini tunaionaje hiyo alama wakati haipo upande wetu?? Pili tukamwambia, akama ikiwa na aina ya gari specific maana yake inahusu gari hilo tu, iweje useme inatumika kote? Kwa alama hiyo maana yake mabasi ndiyo yamezuiwa na sio magari mengine, akawa mkali tukabishana na akatuandikia faini. Hatukukubali, tukatafuta namba ya DTO akasema anatuma mtu aje, ila tutapoteza muda kumsubiri ni bora tulipe tu faini. Tukaondoka zetu.

Sasa tukiwa Ilembula nikapiga picha ya vibao vinavyohusu gari maalumu. Pichani utaona kuna stendi ya mabasi tu na pia kuna stendi kwa ajili ya malori, maana yake hizo zipo kwa gari maalum pichani. Ukizoom utaona mbele kuna stendi ya malori
 

Attachments

  • 20210613_153814.jpg
    596.3 KB · Views: 2
Kosa ambalo nilisimamishwa halina uhusiano kabisa na hayo ya helmet na mkanda, haswa ndiyo kitu kilichonikera zaidi.
Mdau hebu weka bayana kosa walilokusimisha kwalo na kuishia kukuhukumu kwa kosa lingine.

Kuweka wazi huu uozo wa hawa viumbe kutapunguza shombo zao.
 
Inawezekana kwenye mashine yao kuna changua A au B yeye akachagua yote...
 
Mdau hebu weka bayana kosa walilokusimisha kwalo na kuishia kukuhukumu kwa kosa lingine.

Kuweka wazi huu uozo wa hawa viumbe kutapunguza shombo zao.
Ilikuwa hiviii....... Niko njiani naendesha. Mbele nikakutana na daladala aina ya coaster. Ile daladala ilikuwa njiani inaenda huku ikitafuta abiria. Nadhani unajua Mwendo wa hawa jamaa wakiwa barabarani huku wanavizia abiria, ni taratibu sana. Nikaenda nae hivyo hivyo. Na hii barabara katikati kuna mstari siruhusiwi kumpita. Nikawa namfuata huku napiga honi akisimama barabarani. Mwisho uvumilivu ukanishinda Nikasema nimpite. Ile nampita, police hawa hapa. Akanisimamisha akaniambia Kosa langu la kupita sehemu isiyoruhusiwa. Sikubisha ila Nikamuuliza..... Unaona inachokifanya ile daladala, bahati nzuri ile coaster ilikuwa mbele inaendelea taratibu. Police akanijibu....." Mtu kama huyo ni kumpuuza tu" . Dah! Yaani niliishiwa pose. Akaniomba leseni, akaandika kwenye kitabu chake. Halafu akaniambia..... "mtandao umecheza, ukirudi nitakuandikia Kosa lako*. Nikaondoka, kwenda kuangalia ili nilipe si ndio nakutana na mambo ya mkanda na helmet. Nilichoka kabisa.
Hapo kama ni wewe, mawazo jumuishi yatakuwaje.???
Hilo ndio tukio lenyewe.
 
Sijui wanaofanya usaili kabla ya kuajiri hawa jamaa wanatumia vigezo gani.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…